Wakili Albert Msando aachiwa kwa dhamana. Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Arusha, Claud Gwandu aitwa Polisi

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
578
1,000
Wakili maarufu Albert Msando hatimaye ameachiwa huru kwa dhamana Mara baada ya kushikiliwa na polisi jijjni Arusha na kuhojiwa kwa Masaa kadhaa tangu Jana

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa, Moita Koka, amesema kuwa wakili huyo ameshikiliwa kupitia Video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii inayoonyesha kwamba mtuhumiwa anaeleza kwamba hali ni mbaya sana Arusha juu ya ugonjwa wa Corona wakati hana mamlaka ya kueleza lolote juu ya ugonjwa huo .

’’Ukweli ni kwamba na ninasema bila kuficha hali ni mbaya kwa Arusha ndugu waandishi nyinyi lazima mfike mahali muweke miguu chini mseme ukweli ili wananchi, serikali na kila anayehusika atambue kwamba tupo katika hali mbaya ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua mkirudi nyuma na kuogopa kusema tutazikana.

Kamanda Koka, amesema kuwa mtuhumiwa alitoa kauli hiyo April 27 wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati alkigawa vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona eneo la Kaloleni katika ofisi ya Chama cha waandishi habari mkoa wa Arusha.

Aidha ikumbukwe kwamba serikali ilitoa maelekezo kuwa wenye mamlaka ya kutoa taarifa juu ya ugonjwa huo ni Waziri mkuu ,Waziri wa afya maendeleo ya Jamii jinsia na watoto au mganga mkuu wa serikali.

Katika tukio lingine jeshi la polisi linamshikilia Agnes Ndimu Shinji (49) Mkazi wa Lemara jijini Arusha kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Amesema mnamo April 9, mwaka huu ,mtuhumiwa kupitia group la Whatsap liitwalo Football for life,alituma taarifa kwamba mtangazaji wa TBC 1, aitwae Gloria Maiko, amefariki dunia mkutokana na ugonjwa wa Korona kitu ambacho si kweli hali iliyozua taharuki kwa ndugu na jamaa.

Amesema kuwa mara baada ya jeshi la polisi kubaini uzushi wa taarifa hiyo lilianza kumfuatilia na April 29 lilimkamata ambapo katika mahojiano amekubali kulifahamu tukio hilo la kutuma taarifa ya kifo cha mtangazaji huyo bila kuwa na uhakika .

Aidha Kamanda Koka, amesema anatoa onyo kwa viongozi wa siasa pamoja na wananchi kwa ujumla kutokuwa wasemaji wa serikali na wanapaswa kutii amri na maelekezo yanayotolewa na viongozi wakuu wa serikali badala ya kwenye kinyume kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na wate watakaofanya hivyo watakamatwa .

Hata hivyo wakili Msando ameachiwa kwa dhamana mchana wa leo baada ya kulala mahabusu na yupo huru na kutakiwa kuripoti hapo kesho

Ends...
=====

UPDATES
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Arusha (APC) Claud Gwandu ameitwa polisi kutoa maelezo kuhusu tuhuma za wakili Albert Msando kutoa kauli za uchochezi kuhusu ugonjwa wa corona
 

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,150
2,000
Huyu si ndie alie waandikia barua Wamarekani kuwaeleza waache kuingilia mambo ya Tanganyika na kwamba Bashite aendelee kuondoa haki za raia kuishi ? Shetani hanaga rafiki ajue. Wakili msomi Tundu A. Lissu aliwaambia msidhani mko salama. Hivyo vigelegele mnavyo mpigia lbilisi havita dumu na sasa yanatokea kwa mmoja mmoja mpka tutaongea lugha moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,941
2,000
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Aabari-Arusha (APC), Claud Gwandu ameitwa Polisi kutoa maelezo kuhusu tuhuma za Wakili Albert Msando kutoa kauli za uchochezi kuhusu #COVID19

Wakati hayo yakijiri, Albert Msando yeye ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa tangu jana

Albert Msando anakabiliwa na tuhuma za kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa #COVID19 ambapo alidai kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Ngoja Wamshaughulikia... Maana Anajifanyaga yeye Ndio Ana dhamana ya Kuisemea Tanzania Kimataifa pale inapokumbana na Kiganja cha Chuma (Marekani and EU)...
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,361
2,000
Sijui, labda niulize; gavana wa Dar alitahadhalisga Watanzania wa mikoani kua wasije Dar kwasababu watu wanapukutika sana, sasa na yeye mbonahakua na mamlaka hiyo but again idadi ya vifo hadi siku anatoa hiyo, kulikua na vifo 10, mbona hakukamatwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom