Waandamanaji waondoka eneo la ubalozi wa Marekani, Baghdad

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waungaji mkono wa makundi ya kijeshi nchini Iraq yanayoungwa mkono na Iran ambao walivamia maeneo ya viunga vya ubalozi wa Marekani na kurusha mawe katika maandamano ya siku mbili wameondoka jana(01.01.2020).

Hatua hiyo imewezekana baada ya Marekani kupeleka vikosi vya ziada na kutishia kuchukua hatua dhidi ya Iran. Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kuwa na athari za kudumu katika sekta tete ya usalama nchini Iraq pamoja na mahusiano ya kidiplomasia.


1577962466780.png


Waandamanaji, ambao wamekasirishwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya jeshi la Marekani dhidi ya kundi linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah ambapo kiasi ya watu 25 waliuwawa, walirusha mawe katika jengo la ubalozi wakati wanajeshi wa jeshi la Marekani waliokuwa katika mapaa ya jengo hilo wakifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.

Ilipofika mchana, wengi walionekana kutii wito wa kujiondoa kutoka katika eneo hilo, uliotolewa na kundi la wanamgambo wa Kishia linaloongoza vikundi vya umma vya mapambano PMF, ambalo lilisema ujumbe wa waandamanaji tayari umesikika.

Vijana walitumia matawi ya miti ya mitende kufajia mtaa mbele ya eneo la ubalozi wa Marekani. Wengine walikusanya vifaa hivyo na magari yaliwasili kuvichukua.

Trump hataki vita

Maandamano hayo yameonesha mabadiliko mapya katika kivuli cha vita kati ya Marekani na Iran vinavyotokea katika eneo la mashariki ya kati. Rais Donald Trump ambaye anakabiliwa na kampeni ya uchaguzi mwaka 2020, ameishutumu Iran kwa kuchochea ghasia hizo. Ametishia siku ya Jumanne kuchukua hatua dhidi ya iran lakini alisema baadaye kuwa hataki vita. Makamu ya rais katika taasisi ya Charles Koch anayehusika na utafiti na sera Will Ruger amesema hatua Marekani inazochukua kuibinya Iran hazitafanyakazi:

Wanajeshi wa Iraq wakilinda wakati wazima moto walijaribu kuuzima moto uliowashwa na wanamgambo na waungaji wao mkono mjini Baghdad
"Moja ya matatizo hapa ni kwamba sio tu shambulio la roketi la jeshi la Marekani ndio lililochochea mzozo huu, lakini pia kile tulichoshuhudia jana katika ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, nafikiri hii inaonesha kwamba kampeni kubwa ya shinikizo ambayo utawala wa Trump umekuwa ukitumia dhidi ya Inar haifanyikazi kupunguza wasi wasi. Na haifanyi Iran kutulia. Badala yake inaleta uhasama na changamoto nyingi kwa mahusiano."

Iran katika hali mbaya ya kiuchumi

Iran , ikiwa katika hali mbaya ya kiuchumi kutokana na vikwazo vya kuumiza vilivyowekwa na Trump, imekana kuhusika. Ghasia hizo zilitokana na mashambulizi ya anga siku ya Jumapili dhidi ya vituo vya kundi la Kataib Hezbollah kwa kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya makombora ambayo yalisababisha kifo cha mkandarasi wa Marekani kaskazini mwa Iraq wiki iliyopita.

Marekani imesema wanadiplomasia wako salama na inapeleka mamia ya wanajeshi wa ziad katika eneo hilo. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema jana kuwa waziri wa mambo ya kigeni Mike Pompeo ameamua kuahirisha ziara yake kwenda Ukraine, Belarus , Kazakhstan, Uzbekistan, na Cyprus na kubakia mjini Washington ili kufuatilia hali nchini Iraq.

Pompeo alizungumza jana Jumatano na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul mahdi, emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu , wizara ya mambo ya kigeni imesema.

Pompeo aliandika katika ukurasa wa Twitter kuwa Abdul Mahdi alikubali kuwa Iraq "itaendelea kuheshimu jukumu lake la kuyapa usalama majeshi ya marekani na kuyaondoa makundi yanayoungwa mkono na Iran kuyapeleka maeneo ya mbali.
 
Back
Top Bottom