Marekani kuondoa majeshi ya Iraq

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,614
15,942
Hii ndio habari ya hivi punde kutoka makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya marekani Pentagon. Marekani kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu imekua ikishambuliwa katika kambi zake za kijeshi nchini Iraq na Syria kutoka kwa kundi la Islamic resistance wanaopatiwa msaada na Iran.

Waziri mkuu wa Iraq ameitaka marekani kufungasha virago na kuiacha nchi ya Iraq kwa sasa kwakua kuna usalama wa kutosha.

Binafsi naona kutokana na mashambulizi ya hawa Islamic resistance wa Iraq Marekani kwa sasa amekata tamaa maana akigeuka kulia Yemen wamemtangazia vita, Israel hakukaliki moto unawaka, Ukraine napo hali ni tete, China na Taiwan napo hapajatulia huku Kiduku nae akitest makombora yake kila uchao. Hii ndio tabu ya kujifanya kijogoo mambo yote yamekuja kwa mpigo sasa kazidiwa.

Screenshot_20240125_192716_X.jpg
 
Haya mkuu, ukiingia katika jukwaa la international mwanzo mwanzo au kati kati utaukuta.
Nitag mzee
Ila Americant kuondoka mido ist kumewadia
Miaka mitano sidhanii kama itafika Americant akiwepo pale iraq na Syria sidhanii kwakweli
 
Hili suala Iran ilishasema US ataondosha kambi zake Middle East akiendelea na ubabe.

US kupitia wataalamu wa mambo ya kijeshi wamegundua Iran Wana missile zenye range na accuracy ya kupiga kambi yao yeyote pale Middle East,Hali ni tete na Hali ni mbaya.

Kwa machafuko yanayoendelea Middle East Kuna siku wanaweza kujikuta matatizoni kwa kambi zake kushushiwa kipigo cha karne na kupelekea vifo vya askari.
 
Back
Top Bottom