Ndugu;
Siyo uchochezi, panapofuka moshi ujue kuna dalili ya moto. Na pia elewa kuwa si Waalimu tu, na watumishi wengine wote sekta zote Serikalini na binafsi.
Kama ni ugumu wa maisha haupo kwa wachache, hata na mimi niliyeajiriwa hapa katika Stationery inafikia wakati bosi wangu yabidi aniongeze posho, vinginevyo ....................................
MAdakitari na Wabunge siyo wanaojua kuishi vizuri peke yao. Mfumuko wa bei upo kwa watu wote na huu umetengenezwa na Serikali, mbona enzi za Uongozi wa B. Mkapa hakukuwa na mfumuko wa bei, kwa nini huyu tu???
AJIANDAE NA WENGINE TUPO NJIANI.
Walimu wameshatangaza wanataka mshahara wa 900,000/= na wametoa hadi July 2012. Subiri wasiposikiliza maombi yao mgomo wa waalimu tanzania nzima unakuja mwezi wa Sept au Oct. 2012. Ambao hautazimika mpaka kieleweke.
na wengine tupo jikoni tunaandaa sera na kiasi gani tupewe.
Mbunge yeye ni nani atafune keki ya Taifa peke yake, na sisi tunaipenda tunajua uchumi wa Tanzania unaruhusu.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!