Vifo vya Utata: Pumzika Job Yustino Ndugai

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,222
Reaction score
10,730
“Alikuwa na afya njema na tulipata naye chakula cha mchana. Alikuwa mcheshi sana. Siku moja tu akapoteza fahamu, wiki moja baadaye – baada ya kumpeleka hospitali akawa marehemu.”

Mnamo tarehe 12 Aprili 1984, taifa la Tanzania liligubikwa na majonzi makubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine. Ripoti rasmi ya Serikali ilieleza kuwa alifariki dunia katika ajali ya gari huko Dakawa, Morogoro. Hata hivyo, miaka zaidi ya arobaini baadaye, maswali bado yanaendelea kuulizwa: Je, Sokoine alikufa kwa ajali ya kawaida, au aliuawa kisiasa?

Ukisoma kurasa takribani 500 za kitabu cha Day of the Assassins: A History of Political Murder kilichoandikwa na Michael Burleigh mwaka 2021 utajikuta ukiona kuwa hakuna watu wanaoishi kwa hofu kubwa kama viongozi wa serikali haswa wale ambao tayari wanaonekana ni makandokando.

Viongozi ambao waliwahi kushiriki kuwaonea wananchi kisha baadaye kuhoji uhalali wa kuwaonea wananchi, viongozi hawa maisha yao huwa ni sawa na watoto wa bundi kwenye kiota cha Mwewe.

Katika historia ya kisiasa duniani na hata barani Afrika, vifo vya viongozi wa zamani wa serikali, wabunge waliowahi kushika nyadhifa kubwa au waliokuwa tishio kwa mifumo ya kisiasa ya wakati huo, vimekuwa vikizungukwa na giza nene la mashaka na hofu.

Ukishakosoa tu ni sawa na kuwasha taa nyekundu kuwa hatari inakufuata muda wowote na ili taa ya kijani ipate kuwaka ni pale ambapo roho yako ikiwa imeondoka duniani.

Moja ya njia zinazotajwa mara kwa mara ni sumu – aina ya sumukuvu ambayo huingia katika mwili wa binadamu kupitia chakula, maji au hata sindano ya kawaida, lakini huleta madhara makubwa baada ya siku au wiki kadhaa.

Mara nyingi, sumu hii hushambulia viungo kama ini, moyo, figo au mfumo wa neva, na husababisha kifo cha taratibu ambacho kinaweza kuonekana kama ugonjwa wa kawaida kama shinikizo la damu au kisukari.

Katika baadhi ya matukio, kumekuwa na tuhuma za kutumika kwa madawa kwa kiwango cha juu ama cha hatari, ambapo wengi wameipatia jina la “medical assassinations.” Hapa, mgonjwa huwekewa dawa ambazo huongeza matatizo badala ya kutibu tatizo.

1754495990088.jpg

Kuna madai ya baadhi ya maafisa wa afya wanaoshirikiana na idara za kijasusi au maafisa wa usalama katika kufanikisha mikakati hii kwa lengo la kumaliza ‘tishio’ fulani. Sio ajabu kuona kiongozi akisema kuwa ni heri aende kwa sangoma kutibia na kukataa kwenda hospitali za serikali ambazo hutoa huduma VIP kwa viongozi wake.

Mfano wa karibu ni kifo cha mwanasiasa maarufu aliyekuwa akipinga mabadiliko fulani ya kisiasa katika kipindi cha nyuma. Alilazwa hospitali kubwa ya kitaifa, akiwa na hali ya kawaida ya homa, lakini ndani ya siku tatu, hali yake ilizorota ghafla na akafariki huku madaktari wakionesha kuwa walipambana kuhakikisha wanamuokoa, ila hawasemi tatizo ambalo limeondoa uhai wa kiongozi huyo.

Ripoti ya uchunguzi wa kimataifa mara kadhaa zimeonesha kuwa kemikali aina ya thallium, sumu maarufu inayotumiwa na mashirika ya kijasusi duniani kama KGB na CIA, imekuwa mstari wa mbele kuondoa uhai wa watu ambao huonekana kama vipere kwa serikali.

“Tunaambiwa tumpe mgonjwa dawa fulani. Hakuna jina, hakuna maelezo. Kifurushi kinakuja kutoka ‘juu’. Ukikataa, unapotea au unapoteza kazi na kufutiwa leseni yako. Hii inazua maswali mengi kuhusu jukumu la hospitali za serikali, na usalama wa viongozi waliostaafu au walioko kwenye kambi za upinzani.

Pia kuna mbinu nyingine za “kuua bila kuonekana,” ikiwemo ajali za barabarani zilizopangwa (staged accidents). Viongozi waliokataa kukubaliana na mifumo ya kifisadi mara kadhaa wamepoteza maisha kwenye ajali zilizotajwa kuwa za bahati mbaya – lakini ukichunguza, gari lilivamiwa upande mmoja tu, hakuna alama za breki, na hakuna kamera zilizorekodi, mfano mzuri ni ajali ya Hayati Sokoine.

1754496007169.jpg
Aidha, kuna ripoti za kutumia watu wa karibu – wake, waume au ndugu – ambao wanahongwa au kushinikizwa kutumia njia za ndani kama sumu kwenye chakula cha nyumbani. Hili limeonekana mara nyingi kwa viongozi waliostaafu na kuwa “watu wa kawaida,” lakini bado walikuwa na taarifa nzito kuhusu mikataba, matumizi ya fedha au matendo na mienendo ya kifisadi ya serikali zilizopita.

Wapo viongozi wakubwa wa zamani waliokataa kulazwa hospitali za serikali ndani ya nchi za Kiafrika. Mmoja wao aliwahi kusema kwa kejeli:

“Ukilazwa hospitali fulani pale Dodoma, huondoki ukiwa hai. Bora niende India au Nairobi ama Marekani.”

1754495906103.jpg
Kauli hii imezua mjadala mpana, kwani inaonesha kutokuaminiana baina ya mfumo wa afya na wale waliowahi kuutumikia.

Kwa mujibu wa sheria, viongozi wastaafu wanapaswa kulindwa na serikali – ikiwa ni pamoja na huduma za afya, usalama wa makazi na maisha kwa ujumla. Lakini kinachoonekana ni tofauti.

Viongozi wengi wanajihifadhi kimya kimya, wengine wakikimbilia ughaibuni, huku wachache wakikumbwa na vifo vya kutatanisha vinavyopotelea kwenye vitabu vya kumbukumbu kama “ugonjwa wa ghafla.”

Ikiwa taifa linaanza kuona wastaafu na viongozi wake kama tishio badala ya hazina ya maarifa, basi pana hitaji la mjadala mpana kuhusu demokrasia, haki ya kuishi na uadilifu wa mifumo ya afya na usalama. Vifo hivi siyo tu vinakatisha maisha ya watu, bali vinaondoa imani ya raia katika taasisi nyeti za taifa.

“Nchi isiyojali maisha ya viongozi wake wa zamani, haiwezi kujenga msingi wa amani wa viongozi wa kesho.”

PUMZIKA MAHALA PEMA PEPONI MZEE WA CAPERNAUM, MSALIMIE SANA HAYATI MORINGE SOKOINE NA BABA WA TAIFA.
 
“Alikuwa na afya njema na tulipata naye chakula cha mchana. Alikuwa mcheshi sana. Siku moja tu akapoteza fahamu, wiki moja baadaye – baada ya kumpeleka hospitali akawa marehemu.”
View attachment 3434098
Mnamo tarehe 12 Aprili 1984, taifa la Tanzania liligubikwa na majonzi makubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine. Ripoti rasmi ya Serikali ilieleza kuwa alifariki dunia katika ajali ya gari huko Dakawa, Morogoro. Hata hivyo, miaka zaidi ya arobaini baadaye, maswali bado yanaendelea kuulizwa: Je, Sokoine alikufa kwa ajali ya kawaida, au aliuawa kisiasa?
View attachment 3434099
Ukisoma kurasa takribani 500 za kitabu cha Day of the Assassins: A History of Political Murder kilichoandikwa na Michael Burleigh mwaka 2021 utajikuta ukiona kuwa hakuna watu wanaoishi kwa hofu kubwa kama viongozi wa serikali haswa wale ambao tayari wanaonekana ni makandokando.
View attachment 3434100
Viongozi ambao waliwahi kushiriki kuwaonea wananchi kisha baadaye kuhoji uhalali wa kuwaonea wananchi, viongozi hawa maisha yao huwa ni sawa na watoto wa bundi kwenye kiota cha Mwewe.
View attachment 3434101
Katika historia ya kisiasa duniani na hata barani Afrika, vifo vya viongozi wa zamani wa serikali, wabunge waliowahi kushika nyadhifa kubwa au waliokuwa tishio kwa mifumo ya kisiasa ya wakati huo, vimekuwa vikizungukwa na giza nene la mashaka na hofu.
View attachment 3434102
Ukishakosoa tu ni sawa na kuwasha taa nyekundu kuwa hatari inakufuata muda wowote na ili taa ya kijani ipate kuwaka ni pale ambapo roho yako ikiwa imeondoka duniani.

Moja ya njia zinazotajwa mara kwa mara ni sumu – aina ya sumukuvu ambayo huingia katika mwili wa binadamu kupitia chakula, maji au hata sindano ya kawaida, lakini huleta madhara makubwa baada ya siku au wiki kadhaa.
View attachment 3434102
Mara nyingi, sumu hii hushambulia viungo kama ini, moyo, figo au mfumo wa neva, na husababisha kifo cha taratibu ambacho kinaweza kuonekana kama ugonjwa wa kawaida kama shinikizo la damu au kisukari.

Katika baadhi ya matukio, kumekuwa na tuhuma za kutumika kwa madawa kwa kiwango cha juu ama cha hatari, ambapo wengi wameipatia jina la “medical assassinations.” Hapa, mgonjwa huwekewa dawa ambazo huongeza matatizo badala ya kutibu tatizo.
View attachment 3434103
Kuna madai ya baadhi ya maafisa wa afya wanaoshirikiana na idara za kijasusi au maafisa wa usalama katika kufanikisha mikakati hii kwa lengo la kumaliza ‘tishio’ fulani. Sio ajabu kuona kiongozi akisema kuwa ni heri aende kwa sangoma kutibia na kukataa kwenda hospitali za serikali ambazo hutoa huduma VIP kwa viongozi wake.

Mfano wa karibu ni kifo cha mwanasiasa maarufu aliyekuwa akipinga mabadiliko fulani ya kisiasa katika kipindi cha nyuma. Alilazwa hospitali kubwa ya kitaifa, akiwa na hali ya kawaida ya homa, lakini ndani ya siku tatu, hali yake ilizorota ghafla na akafariki huku madaktari wakionesha kuwa walipambana kuhakikisha wanamuokoa, ila hawasemi tatizo ambalo limeondoa uhai wa kiongozi huyo.
View attachment 3434099
Ripoti ya uchunguzi wa kimataifa mara kadhaa zimeonesha kuwa kemikali aina ya thallium, sumu maarufu inayotumiwa na mashirika ya kijasusi duniani kama KGB na CIA, imekuwa mstari wa mbele kuondoa uhai wa watu ambao huonekana kama vipere kwa serikali.

“Tunaambiwa tumpe mgonjwa dawa fulani. Hakuna jina, hakuna maelezo. Kifurushi kinakuja kutoka ‘juu’. Ukikataa, unapotea au unapoteza kazi na kufutiwa leseni yako. Hii inazua maswali mengi kuhusu jukumu la hospitali za serikali, na usalama wa viongozi waliostaafu au walioko kwenye kambi za upinzani.
View attachment 3434103
Pia kuna mbinu nyingine za “kuua bila kuonekana,” ikiwemo ajali za barabarani zilizopangwa (staged accidents). Viongozi waliokataa kukubaliana na mifumo ya kifisadi mara kadhaa wamepoteza maisha kwenye ajali zilizotajwa kuwa za bahati mbaya – lakini ukichunguza, gari lilivamiwa upande mmoja tu, hakuna alama za breki, na hakuna kamera zilizorekodi, mfano mzuri ni ajali ya Hayati Sokoine.
View attachment 3434104
Aidha, kuna ripoti za kutumia watu wa karibu – wake, waume au ndugu – ambao wanahongwa au kushinikizwa kutumia njia za ndani kama sumu kwenye chakula cha nyumbani. Hili limeonekana mara nyingi kwa viongozi waliostaafu na kuwa “watu wa kawaida,” lakini bado walikuwa na taarifa nzito kuhusu mikataba, matumizi ya fedha au matendo na mienendo ya kifisadi ya serikali zilizopita.
View attachment 3434105
Wapo viongozi wakubwa wa zamani waliokataa kulazwa hospitali za serikali ndani ya nchi za Kiafrika. Mmoja wao aliwahi kusema kwa kejeli:
View attachment 3434099
“Ukilazwa hospitali fulani pale Dodoma, huondoki ukiwa hai. Bora niende India au Nairobi ama Marekani.”
View attachment 3434098
Kauli hii imezua mjadala mpana, kwani inaonesha kutokuaminiana baina ya mfumo wa afya na wale waliowahi kuutumikia.

Kwa mujibu wa sheria, viongozi wastaafu wanapaswa kulindwa na serikali – ikiwa ni pamoja na huduma za afya, usalama wa makazi na maisha kwa ujumla. Lakini kinachoonekana ni tofauti.
View attachment 3434100
Viongozi wengi wanajihifadhi kimya kimya, wengine wakikimbilia ughaibuni, huku wachache wakikumbwa na vifo vya kutatanisha vinavyopotelea kwenye vitabu vya kumbukumbu kama “ugonjwa wa ghafla.”

Ikiwa taifa linaanza kuona wastaafu na viongozi wake kama tishio badala ya hazina ya maarifa, basi pana hitaji la mjadala mpana kuhusu demokrasia, haki ya kuishi na uadilifu wa mifumo ya afya na usalama. Vifo hivi siyo tu vinakatisha maisha ya watu, bali vinaondoa imani ya raia katika taasisi nyeti za taifa.

“Nchi isiyojali maisha ya viongozi wake wa zamani, haiwezi kujenga msingi wa amani wa viongozi wa kesho.”
View attachment 3434101
PUMZIKA MAHALA PEMA PEPONI MZEE WA CAPERNAUM, MSALIMIE SANA HAYATI MORINGE SOKOINE NA BABA WA TAIFA.
Wasio Wanasiasa kufa ruksa ila wakifariki Wanasiasa ni vifo vya utata Kwa kuwa wao hawatakiwi kufariki au Wana vifo vyao spesho ama?
 
Back
Top Bottom