jamani mweee mmerudisha ubishi ule uleeee!..
Guys hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa maskini! Umaskini huleta NJAA ya akili na tumbo. Nitarudia kusema kwamba Umaskini wetu ni Ugonjwa!.. unahutaji tiba basi, zaidi ya yapo hakuna! kwa sababu hao hao Waafrika wanapoishi nchi hizi za Ulaya mbona wanafanikiwa sana? tena wengi wamefanikiwa ktk muda mfupi sana kuliko hata wazawa wazungu ktk nchi zao. Je, mnajua kwamba microwave ilivumbuliwa na Mtanzania ambaye kaishi ktk mazingira tofauti. Kuna mifano mingi sana ktk mazingira mazuri na utawala mzuri hata hao wazungu huko Romania na nchi za east Europe wamechoka ile mbaya!.. taratibu wenzetu wameanza kuikubali dawa ya Umaskini sio sisi.
Kama nilivyowahi kusema ktk mjadala mmoja lokuwa ukifanana na huu. mali tulizokuwa nazo sisi ni sawa na sahani la pilau siku ya maulidi!...likishuka chini tu sahani ni tupu kwa sababu hapo mjomba ni Darwin na ujanja kupata sio kuwahi tena. Hivyo basi hata utawala wetu unakuwa hauna mpangilio mzuri utadhani siku ya maulidi na hadi wananchi tumesha adopt concept hiyo. Hii ndio system ya nchi zetu tofauti na wenzetu ambao hawana harka, hula kwa visu na Umma huku wamekaa mezani na kila mtu ana plate yake!.. hiyo ndio sikukuuu ya mzungu.
....maulid zile ilikuwa kiboko...siku hizi ni za kistaarabu!chakula si kipo!
....tukirudi kwenye mjadala! ni kweli elimu ni muhimu<utahitaji wahasibu,wahandisi,madaktari,wanasheria,n.k!>
....umasikini nao si mzuri kwani unatukwamisha kujenga vituo vya afya vya kutosha,kununua madawa,kusomesha madaktari bingwa wa kutosha...halafu watoto wetu wanakuwa wabuya dawa,wezi na majambazi,malaya,n.k....yaani tunazalisha kizazi hasara kwa nchi.
....tatizo letu kuu wala si rushwa<kwani rushwa ipo hata huko asia>sasa,nisieleweke vibaya,siitukuzi rushwa!.tunahitaji zaidi utawala wa sheria na sheria za nchi kufuatwa!
....tatizo ni kuwa,hatuna utamaduni wa kuendelea!tunaridhika na maisha ya kawaida yenye viwango vya chini kabisa vya ubora. hii inatokana na uvivu na vilevile utamaduni usioenzi uchapaji kazi!
....angalia mafundi wetu mbalimbali wanavyofanyakazi zilizo chini ya kiwango<hasa waashi na seremala>kisa,wanamjengea au mtengenezea mswahili mwenzao....sasa,we subiri hiyo kazi wapewe na mzungu au mhindi...utaona tafauti!.utamaduni huu ndio unaoturudisha nyuma kimaendeleo!
....halafu,tunapenda vitu vya mkatomkato<shortcuts>.angalia jinsi tusivyotaka kuwekeza na tunavyokimbilia kuwa wachuuzi<petty traders>yaani,hakuna mtu anayetaka kusota kidogo,wote tunataka faida za haraka haraka!
....hivi,hatuoni ajabu pale mzungu anapotoka kwao yuropa na kuja kuwekeza hapa kuzalisha bidhaa tunazotumia sisi na wala haziendi nje!.wachina hivi sasa wanakula tenda nyingi za kujenga majumba...ambayo sisi wenyewe tungeweza kujenga!
....ni kweli sisi wenyewe hatuwezi bila msaada wa wazungu!