Waafrika ndivyo tulivyo?

Dondola,
Sijui kama nimekuelewa vizuri lakini nadhani una maanisha kuwa sisi rangi yetu ndio nuksi yenyewe au sio?.....

Hapana ndugu yangu sii rangi yetu isipokuwa sisi Waafrika kilichotuangusha hadi leo ni kama nilivyotaja hapo juu. Mbali na fikra binafsi nadhani mchango mkubwa wa udhaifu wetu umetokana na ULIMBUKENI. Katika mataifa yote unayoyafahamu ebu nambie race hata moja ililopoteza kabisa culture zake na kubeba za kigeni?...hakuna...

Waafrika peke yetu bob na kibaya ni kwamba hatukubaliki na hao tunaowaiga. Wale waliotawaliwa na Mfaransa basi hao hujifanya Wafaransa kuliko hata Wafaransa mwenyewe. Na tunaamini kabisa kuwa hatuwezi kukubalika bila kujifunza culture za hawa watu. Huyo Mmarekani mweusi imechukua karne nzima kuweza yeye kukubali kuwa ana asili na Afrika tena baada ya wazungu kuwatema. Huko South ndio kabisa hawakubali kama Maspanish, bado tu wameshikilia kuwa wao ni maspanish!...hawataki kabisa kujishirikisha na Afrika. Lakini huyaoni haya ktk race nyinginezo, Mchina amebaki Mchina popote pale alipo hata kama atazungumza lugha yako fluent. Na atafanya juu chini uanze kula wali kwa vijiti, kumwabudu Budha na hata ujifunze Kung fu na Karate.

Tazama Kariakoo, si wamejaa Wachina hao wamachinga lakini subiri sii muda Chinese food itakavyoanza kupata soko!.. they sale Chinese product! Mtu mweusi tunaona Uafrika ni uchawi tu unatia kiza! Wahindi vile vile leo hii chakula chetu kikuu cha kumkamatia mgeni utasema Biryani... tumeiga wapi?

Tazama, Hata taifa la zamani kihistoria kama Misri wamepoteza kabisa lugha na culture zao zoteeee! leo hii wanajullikana Wamisri kama Waarabu hakuna tena Mu - Misri wala culture zake zaidi ya kusimuliwa hao akina Pharaoh.

Ulimbukeni mshikaji na leo hii kiswahili kinaonekana choo kabisa tena tumeanza hata kukiwekea mashaka kuwa ni lugha ya utumwa maadam tu Kiingereza kipate nafasi ya kwanza tujisikie nasi binadamu - wazungu.

Kifupi sidhani kama matatizo yetu yanatokana na laana ya rangi. Isipokuwa mambo muhimu hapo juu yakichangia na Kushindwa kusamehe Utumwa kama ni jambo lililokwisha tokea na tuangalie mbele. Wagonjwa wa Dipresheni huendelea kudhoofika kila siku wanaposhindwa kusamehe matukio yaliyopita ili wapate mwanzo mpya. Na wengine hufa bila gonjwa kwani wakipimwa hospital huonekana wazimaaa! basi Afrika ndio maradhi yetu hayo!
 

Well, niliposema 'colour', ndani yake nilikuwa nimebeba maana ya culture. Kwa hiyo nakubaliana nawe kuwa ni hiyo culture yetu ya ulimbukeni.🙂 Kuhusu culture za kigeni, tofauti yetu waafrika na wengine ni kuwa tunaiga culture badala ya kuiga maarifa. Wengine huwa na lengo la kuiga maarifa, kama ili kupata maarifa inambidi aige culture, basi atafanya hivyo kwa lengo hilo tu, lakini mwishoni atabaki na culture yake, kama walivyofanya wajapani. Kwanini waafrika tunang'ang'ania kuiga culture bila kuiga maarifa? Kweli ni ulimbukeni
 
Great points Mkandara. Kifupi: kinachotuangusha sisi watitu ni ubinafsi, kutojiamini, ulimbukeni, nk.

Kila ninaposoma magazeti ya Bongo, sikosi maelezo ya namna hii: Raisi au Waziri mkuu akiwa ziarani ughaibuni akutana na mkuu wa nchi fulani na kujadiliana uhusiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbali mbali. Raisi ameahidiwa msaada wa kujengewa daraja, au shule au zahanati au pump za maji au piki piki 10 na vitu vingine vidogo vidogo vya namna hivyo.

Viongozi wetu wapo makini kweli? Tunataka kiongozi anayejiamini kwamba watanzania wenyewe wanaweza kujiletea maendeleo au walao kuondokana na umasikini kwanza.
 
Invicible hayo matatu ndio hasa yanayotulet down, hasa la ubinafsi na kukosa uzalendo. Ndio maana leo hii kila mtu Tz anataka uongozi be it udiwani, ubunge etc, ote ni kwa manufaa binafsi!
 
dondola,
tofauti yetu waafrika na wengine ni kuwa tunaiga culture badala ya kuiga maarifa.
.
Mwanaume haya maneno na siku tutajifunza kuiga maarifa basi ndio mwanzo wa safari utakapo anza.

Invincible,
Haswaaa mwanangu umesema, jamani hata shule za msingi, Zahanati na eti madaraja lazima tupate msaada toka nje tena kwa ziara ya rais ama Waziri mkuu?...

Jana tulikuwa na baadhi ya viongozi toka Bongo, mshikaji kila PENDEKEZO wao wanalo jibu!...(Pendekezo sio swali)
Sasa nambie ikiwa mtu atapendekeza kuwa nchi yetu iwaandae vijana Kielimu ili kwenda sambamba na uwekeshaji...atapewa jibu kutokana na hoja fupi iliyodai kuwa nchi yetu ipo nyuma kielimu. Hapo utasikia shule vyuo na University ngapi zimefunguliwa na hata idadi ya wanafunzi wanaohitimu.

Njia za Mawasiliano kuboreshwa utaambiwa hesabu ya simu za mkononi n.k.. Hali swala zima ni kwamba Tanzania inahitaji kuwaanda vijana wake mapema kwa kila mradi unaokusudiwa. Sio kuwapa elimu baada ya mradi umeisha funguliwa jambo ambalo linawafanya wageni wawekeshaji kuwa na kila sababu ya kuchukua watu toka nje.

Kisha basi ukiuliza kuhusu sababu ya watu wa nje kuchukua kazi zetu, utaambiwa hatuna elimu ama ujuzi, well sasa hizi University na vyuo tunavyojisifia kufungua vina toa elimu gani?..

Yaani hata haielezeki zaidi ya mtu kutazama kinachoendelea.

MTz,
nakubaliana nawe kabisa! nadhani hii ya Wataalam wetu kugeuka kuwa wanasiasa pia inazidi kuchangia sana. Na ndio maana kila swala linapata jibu la mkato. Utajibiwa kisiasa ama kitaalam na mhusika hali akijua HALI halisi ya nchi yetu haipo hivyo kabisa.
 
Mkandara,

Kaka tupe yaliyojiri in brief ktk ziara ya Lowassa huko, au hamkupata nafasi ya kuongea naye pamoja na msafara wake?

Je, wameongelea lipi jipya?
 
Hakuna mpya ndugu yangu!...hakuna mpya isipokuwa tunasubiri matokeo. Tulichonacho ni hiyo HOPE!

Ujumbe mzima Unaitangaza nchi kwa kutumia sana vitabu na statistics hali hali halisi inajulikana....hatuna UMEME. Kwa hiyo wamekutana na hao wawekeshaji wanaoifahamu TZ na sijui kama kweli message imefika kwa wengineo ambao hawaifahamu nchi na wapenda haki bila ULAJI.

Wewe unafikiri mkutano uliodhaminiwa na Barricks na Wahindi unategemea kipya?

Kama unakumbuka ya Mzee ES, Ukitaka kuonana na Bush lazima zikutoke wewe..he had no time kwa wabongo bob na wala haikuwa kusudio laziara yake.
 
mimi naamini muafrika hana akili ni buburu tu.

 
Kinyikani,
Jiulize tu what happened to people like P.W. and Hitler. History proved them wrong.Ukikubaliana nao ni kama una suffer from self hate.
 
Dondola,
Lakini hiyo emotional incompetence imesababishwa na nini? Years of humiliation, deprivation, and subjugation under apartheid. You see what happened in New Zealand with the Maoris, the Aborigines of Australia, the natives of North America, the genocide that was perpetrated by the white man against people of other colour and then you can talk about emotional incompetence. Acha bwana!
 

Jasusi, ngoja nikufafanulie kwanini nimeafiki emotional incompetence:
Wewe hapa umetoa mifano ya jinsi race nyingine zilivyoonyesha emotional incompetence dhidi ya waafrika, hiyo mimi siiti emotional incompetence, hiyo kwa mtazamo wangu ni temporary emotional incompetence ambayo ni matunda ya conflict fulani (ni kama aina fulani ya vita). Emotional incompetence ninayoiongelea mimi ni pale tutakapofanya comparison ya emotional incompetence ya:
-Waafrika wenyewe kwa wenyewe
-Wazungu wenyewe kwa wenyewe
-Waarabu wenyewe kwa wenyewe
-Waasia wenyewe kwa wenyewe
etc

Hebu chunguza hapo na unambie ni jamii gani yenye kiwango cha chini cha upendo.
 
Dondola,
Mbona unanipa mtihani mzito ndugu yangu? Ngoja basi nijaribu. Wazungu wakati wa conquest of empires hawakuwa na upendo miongoni mwao. Walishindana na kuibiana mali ( si unakumbuka stori za maharamia wa baharini? Pirates) Hawa walikuwa wazungu kwa wazungu. Hatimaye wakakubaliana kushirikiana. Wakagawana nchi--kv Afrika, Latin Amerika n.k na wakawekeana mipaka. French colony, British Colony, Portuguese colony.etc. Sisi Waafrika tumekuwa product ya divide and rule, na ndio maana mpaka leo mpaka kesho ukabila umejaa Kenya, Nigeria, South Africa, n.k. Sasa ndugu zetu Waarabu nawaweka kapu moja na sisi Waafrika. Matatizo yao ni kama yetu. Sisi ukabila, wao tofauti za Usunni na Ushiya. Badala ya kujiona Waarabu wanaona Usunni wao kwanza na Ushiya. Ni kama sisi. Ukabila kwanza halafu Uafrika wetu. Mpaka hapo tutakapotambua kuwa Uafrika wetu ni muhimu kuliko kabila na kwamba common enemy wetu ni hili gwanda tulilovishwa kutoka nje, i.e colonial mentality hatutaweza kuwa na mshikamano unahohitajika kujikwamua. Sijui umenielewa?
 
Dondola,

Huyu ndugu yetu Kinyikani kaanza na kusema kuwa anakubaliana na hotuba ya Botha!.... Hii inatisha sana ikiwa mmoja kati yetu anakubali jinsi tulivyochambuliwa na hata sababu za kutumaliza.

Swala la waafrika na emotional incompetence ni swala la hisia ambazo zimetokana na..... Kama alivyoeleza Jasusi.
Kisha tukubali kwamba sisi waafrika bado tupo karne nzima nyuma. Hata ukija tazama vita ya kwanza na ya pili, sisi waafrika tulipigana bila malengo kabisa. Yani Wafaransa walipigana kulinda nchi yao Waingereza, Korea na hata Wajarumani na Wa-Japanwote walikwenda vitani kwa jina la nchi zao. Sisi tuliburutwa tu na Mjarumani mara Muingereza kama vile wao walipoburutwa enzi zile za utawala wa akina Napoleon na Kaizari....

Kwa hiyo hapa kuna gap kubwa sana ambayto inahitaji sisi tusahau kwanza nje na tuanze kujisafisha wenyewe kwa kuelewa kuwa UMOJA wetu ndio ngao na nguzo yetu.

Umeyaona ya Rwanda na Burundi, leo hii hata sisi wenyewe tunasita kuwakaribisha kwa sababu tunawaona wao kama wanyama vile. Tupo radhi tukiambiwa tujiunge na OIC kuliko Wanya - Rwanda.

safari ni ndefu sana lakini sii kweli kuwa sisi nii binadamu kamili na tunastahili kutendewa maovu yote.
 
Good points Mkandara. Tunahitaji kuthamini na kuona umuhimu wa umoja wetu as a people and as Africans. Kitu kimoja ambacho nimegundua ninaposafiri ni kwamba sisi Waafrika experience zetu ni moja. Awe Mkongo, awe Mnigeria, wote tumepitia experience moja---kutawaliwa--- but we as a people, tukianza kujiona kuwa ni wamoja there is so much we can do for each other and for our countries.
 
Ramani Ya africa Ilichorwa na ......?
 
Hao walio Chora...Dunia...
wakati-Ramani zao walichora wao wenyewe........
Sisi wa Africa tuna wafuata wao....Na tusipo wafuata wao sijui tuta enda wapi?-
Africa itabaki kua Mtoto...kwasababu tuna onekana kua wageni kwa kila jambo...!!!-Hivi kwanza wa Afrika ni watu gani?
Hili Jina Ni La Lugha Gani...???

hata hii Jamboforum ina endeshwa Kiafrica...au sijui vipi?

Jasusi-
Tatizo ni hao walio tutangulia kimaendeleo...wajanja kuliko tunavyo dhani....
Viongozi watambue-Hii misaada Tuna yo pewa pewa Ita tu ghalimu sana Katika vizazi vyetu vyote- tuangalie sana nani anatupa...
Tabia za vizi kwa viongozi..

Hivi Hili Bara Tunalo ishi sikumoja linaweza likawa na Nguvu Kama Marekani?
 
Gigo,
Hapo nakuafiki kabisa. Hakuna hata nchi moja iliyowahi kuendelea kwa kutegemea misaada. Ndiyo maana Mwalimu alibuni sera za ujamaa na kujitegemea. Hata kama hazikufaulu lakini ile haja ya kujitegemea angalau tungeiendeleza.
 
Good point

Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada na wajomba kutoka nje. Wanachofanya ni kuja kusomba mali zetu na kutuacha weupe.
 
Lakin Tuna mambo Mangi ya-kufanya!!
Yatupasa tuwe pamoja...
Kuna mtu mmoja- Nilimsikia akisema-'Si Unapenda Fedha Zangu!.. basi Na mimi Unipende! kam unavyopenda fedah zangu">> haya maneno Yana choma Kimtindo..

Hata hivyo Dunia Ilipofikia Hatuwezi tena- Kujitenga!! la sivyo Tuta jitafutia Maadui wengi-
shida zipo po- Pote Duniani- Mimi naamini hivyo!!
Tufanye Kazi kwa Bidii..
Tupendane...
Tuunganishe Imani zetu..../Akili zetu.

Tushirikiane-lakini sio wote wata kao kua na madhumuni mazuri....
Tujitahidi sasa!!!!..La sivyo bara letu (litabaki/lita taka) kua Kama Jela!!

Wazee tuna hitaji Msaada wenu!! Lakini Tuheshimiane!!!
kwakua wewe ni somi Basi Unahofia sisi wengine Ni Ma- home -Less,
Hizi salaam nawapa tokea kijiweni..

Vijana wanaelekea Kuchoka-
Yaani mnahofia tukiingia madalakani tuna Wafunga Jela?
Hapana!!
Hata si si Tuta fuata Nyao zenu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…