Wa kwanza kumkumbuka Kikwete

Wa kwanza kumkumbuka Kikwete

Khaa!! Mie kwa miaka yote 10 nitamkumbuka kwajambo moja kubwa na lenye maana sana kwa ustawi wa nchi yetu. KUMKATA YULE JAMAA akiwa na pesa zake na vibaraka wake..

Ha ha ha!
Hili nadhani ndio jambo kubwa na la msingi sana kwa maslahi mapana ya taifa letu!
 
Ni kweli aliingia na kuruhusu uhuru wa habari,ukatumiwa vizuri bali kuondoka kaondoka na uhuru wake wa habari kwa kutungwa kwa sheria kali za mitandao
 
Familia ya Mwangosi. Wananchi waliopigwa mabomu na kuuliwa na na Polisi huko Arusha nao watamkubuka Kikwete!
 
Atakumbukwa kwa kuondoka madarakani akicha jiji la dar mikononi mwa upinzani
 
Habari zenu!

Pamoja na kwamba sio rahisi na haiwezekani kuridhisha watu wote, pia kukosolewa pale mtu anapoenda kinyume ni sahihi au kukosolewa ili kujijenga zaidi, INARUHUSIWA.

Binafsi, mh rais mstaafu wa awamu ya nne naona amefanya vizuri.

Katika kipindi cha JK nimefanikiwa:

- Kusoma hadi elimi ya juu bila kupitia chuo cha UDSM ambacho kilikuwa ndio chuo kikuu kikubwa kabla ya JK kuingia madarakani, JK kaweka miundo mbinu iliyowezesha hili.

Nina ndugu, jamaa na marafiki ambao wamefanikiwa kupata elimu pia na kuweza kuitumia hiyo elimu ktk kujikwamua kimaisha. JK kaweka mazingira ya kuwezesha vyuo vikuu binafsi na vya serikali kuongezeka. Ni wewe tu!

-Nishati: Bibi yangu kijijini ana umeme siku hizi nyumbani kwake.

-Maji: kuna kisima cha maji mita kama hamsini toka anapoishi bibi yangu kijijini, hii imewezekana wakati wa uongozi wa JK.

-Kwenda kijijini, kutoka Dar likuwa inachukua masaa mengi zaidi ya 14, barabara haikuwa nzuri, sasa ni mkeka!

-JK katuwezesha kujielezea zaidi, freedom of expression imekuwa kubwa sana.

-nk

KWA UJUMLA, JK KAWEKA MIUNDO MBINU MIZURI AMBAYO KAMA ITAENDELEZWA NA KUTUMIWA BASI ANGALAU TUTASONGA MBELE.

JE KWAKO NI KIPI KITU CHANYA KINACHOWEZA KUKUFANYA UMKUMBUKE JK NA UONGOZI WAKE?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania, Mungu wabariki marais wastaafu, na Mungu mbariki RAIS MPYA DR. John Pombe Magufuli.

Siasa tuweke kando, uchaguzi umeisha, tujenge nchi, na kama ni kukosoana eidha kwa sisi kwa sisi au kisiasa, basi tufanye iwe ktk CONSTRUCTIVE CRITICISM.
 
nitamkumbuka kwa kuongeza shule za sekondari, agizo na utekelezaji wa maabara kila shule, barabara nzuri za viwango, academy ya michezo Dar na Mwanza, uwanja wa ndege Songwe, mabasi ya mwendo kasi, treni mpya Dar, n.k
 
Kuvunja record ya kulala angani mda mrefu
 
Nitakuwa mwizi nisiposema huyu bwana, niliweza kusoma nje ya nchi. Si kusoma tu exposure niliyopata imenifanya wkt mwingine nione nchi ina deni kubwa kuwafanyia watu wake. Watz bado hawajui mahitaji yao, ikisabababisha wajanja kula bata zaidi. kwa ama umasikini au kutosoma vya kutosha watz waliowengi.

Asante Kikwete J.M
 
Huu ndio upimbi na kujishauwa, nje ya nchi ni JK ndio amekusomesha? na JK anahusika vipi na exposure yako? mbona umeandika kama boya tu lisilo na exposure yoyote?
 
nitamkumbuka kwa kuongeza shule za sekondari, agizo na utekelezaji wa maabara kila shule, barabara nzuri za viwango, academy ya michezo Dar na Mwanza, uwanja wa ndege Songwe, mabasi ya mwendo kasi, treni mpya Dar, n.k
Asante sana, umeweka vitu ambavyo nilivisahau ila vinanigusa na kuninufaisha pia mimi, ndugu, jamaa na marafiki zangu.
 
Leo nilidhani Ukawa wangeenda kumuaga JK kwa namna alivyo wapandisha thamani, kakuza demokrasia saana, uhuru wa kuongea, kafanya mazungumzo nao mno na kuvumilia ( Subra).
Leo hawataki muaga mtu aliye upa upinzani fursa ya kukua, basi kama haitoshi walimtukana 10 yrs. Na hakujibu kitu huyu ni zaidi ya rais kwani hata hawa manabii wa sasa huwa na mihemko na kuwatusi watu.
Tanzania inamuaga JK kama shujaa wa Africa, huyu hakua rais wa nchi tu bali ni msimamia Amani wa Africa nzima.
Natamani siku nipate muda wa kuongea nae inshallah nitamwambia mambo mengi ambayo yy alifanya kama wajibu ila yameleta heri nyingi.
Sasa #HapaKaziTu#
 
Attachments

  • 1446721171190.jpg
    1446721171190.jpg
    29 KB · Views: 226

Back
Top Bottom