Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya hali ilivyo katika vyuo vikuu vyetu vya umma. Ninazo hoja sita, leo nitawasilisha mbili na zingine nitawasilisha ndani ya juma hili.
Kwa hivi sasa vyuo vikuu vingi vya umma vinakabiliwa na idadi ndogo sana ya Maprofesa (Full professor) na Maprofesa waandamizi (Associate Professor). Mchakato wa kupanda madaraja kwa wana taaluma katika vyuo vikuu vya umma bado umegubikwa na utata mwingi ndani ya tasisi zenyewe. Michakato imekaa kipembe tatu kutokana na kukosekana ama kuwepo kwa miongozo iliyojaa utata na hivyo kulazimu yule au wale waliopewa dhamana kutafsiri kadri ya uelewa wao na hivyo kukosekana uelewa wa pamoja.
Pamoja na changamoto hizo, vyuo vikuu vya umma muda si mrefu hadhi yake itashuka kwa kiwango kikubwa sana. Nafananisha kushuka huku ni sawa na namna vyuo vikuu vya umma Uturuki vilivyoporomoka au mfanao wa shule zetu kongwe kama Msalato na zinginezo zilivyoporomoka na kuoneka shule binafsi ni bora zaidi ya shule hizo. Profesa mmoja ni sawa na wahadhiri wasaidizi 20 au 25. Kwa hii sasa Maprofesa wengi wamalizapo muda wao wa nyongeza wa miaka 5 ndiyo basi tena na wengi wao wanachukuliwa na kwenda katika vyuo vikuu vya binafsi. Hali ya mabadiliko haya ilianza tu pale awamu ya tano ya serikali yetu ilipoingia madarakani.
Maprofesa ni hazina kubwa sana. Kwa wenzetu Ulaya hawafanyi hivi hata kidogo na ndiyo maana vyuo vyetu vinakosa wabobezi na hivyo kuishia kufundisha tu bila ya kufanya tafiti. Naomba sana ikikupendeza Mheshimiwa Rais Samia (Mama yetu) litizame jambo la ku-retain hawa maprofesa kwani kutokufanya vile hadhi ya vyuo hivi itashuka sana maake hawa wanaosalia (Juniors) wanahitaji kusimama juu ya mabega ya hawa watu. Nitatoa mfano hai mmoja: kwa mshika dau yeyote wa elimu ebu apate nafasi na atembele chuo cha Marian pale Bagamoyo na uone mabadiliko kiliyonayo sasa. Chuo hiki ni chuo ni private institution.
Mitaala ya Vyuo Vikuu
Panahitajika uharaka sana wa kufanya mageuzi makubwa katika mitaala ya vyuo vikuu hapa nchini ili kuendana na Dunia ya sasa. Malengo ya vyuo vikuu ni matatu ambayo ni ufundishaji (teaching), tafiti (research)na utoaji huduma kwa jamii (Public consultancy). Katika malengo hayo matatu, lengo la kwanza ndiyo linalofanyika kwa sasa. Tunahitaji kubadili vyuo vikuu vijikite katika tafiti zenye tija kwa Taifa na si hiki kinachofanyika sasa.
- Ajira za Maprofesa katika vyuo vikuu vya umma na hali halisi ilivyo hivi sasa katika vyuo hivi
- Mitaala ya Vyuo Vikuu