Vyombo vya habari vyabadili gia angani

Vyombo vya habari vyabadili gia angani

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
5,286
Reaction score
5,423
Hili jambo nimelifanyia utafiti almost siku tatu zilizopita, nimegundua kua vyombo vyetu pendwa vimepata homa ya dengue baada ya kutishwa na wenye mamlaka sio magazeti, redio wala TV station kote wameufyata.

Nchi nyingine saa hizi tayari wanahabari wangekua road ila kutokana na kutokua na ushirikiano ndo tunaona haya yote,sasa hivi kila chombo kinahimizwa kimsifu mkulu, hatari sana hii.

Niwashauri kwa sasa ili kupata habari za maana bora Star TV au Azam na kwa redio bora Efm.
 
  • Thanks
Reactions: ovi
mie nyamaza nisubiri mkanda huu utakavyokwisha. Kuna kitu kama baraza la habari, Jukwaa la Wahariri, wanalo neno????
 
Nimesiangalia taarifa ya habari jana Channel Ten na ITV sijaona habari inayozungumzia kufungiwa kwa radio station zilizofungiwa jana. Nikajiuliza sana ata Channel ten ambayo Magic Fm ni radio yao?. Kweli tumeshaanza kunyooka.
 
vipindi vya namna ya dinna Marius vitaongezeka sana.
redio zetu zotaongea upuuzi na umbea wa mtaani tu.
 
Mtukufu Rais Dr. J. P Magufuli, Kwa kuwa wewe ndio mwenyekiti wangu nalazimika kukuuliza maswali ambayo naamini hutayachukia.

Wote tunayo kumbukumbu kuwa salamu ya chama chetu cha mapinduzi ilikuwa hivi:-

-Kidumu chama cha mapinduzi,
-Zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm
-Idumu siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Japo salamu hii bado inaonekana kuwa na ushawishi miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla, haikutolewa taarifa rasmi kwamba nini kilisababisha salamu hii pendwa kwa chama ikaacha kutumika.

Kwa kuwa umeshika hatamu za chama, ni vema sasa ukalitolea ufafanuzi jambo hili.
.....kwanini chama cha mapinduzi kisidumu!!!!

Hii "fikra ya mwenyekiti" imepoteza uhalali wa kudumu??? au hofu ya udikteta!!! Nani aliona mbali kiasi hicho.

Siasa ya ujamaa unaisemeaje, bado inatekelezeka? Kama ndio utaifanya itekelezekeje kwenye mfumo wa utitiri wa vyama!!!

Kama hutajali utupe mwongozo pia kuhusu siasa ya nchi yetu, kuna wakati fulani enzi za mwalimu ilikuwa haifungamani na upande wowote! je hali bado iko hivyo hivyo??

Najua maswali haya hutayajibia humu ukumbini, lakini najua utapewa microphone useme na hadhira siku yoyote popote ndani ya mipaka ya nchi yako, hapo hapo chomekea majibu ya maswali haya.

Kwa sasa sisi tunaendelea kuyajadili maswali haya na makada watiifu wa chama ndani ya JF watatetea hoja.
 
Ajira zimekoma kwa secta nyingine lakn kwa vijana wa mtandaon zimeongezeka. Kwa sasa kila bandiko kuna watu wanapitia!! Hapa kama kuna uchochez vile tumkamate au!!
 
Mi nafikiri kabla ya kuuliza hayo maswali ungejiuliza wewe mwenyewe kama uelewa wako wa hayo mambo ni mzuri kiasi gani. Ungefahamu kwanza siasa ya ujamaa ni nini? Ungejiuliza kuwa siasa ya ujamaa haitekelezeki katika mfumo wa vyama vingi? Vyama vya kijamaa vilivyoshika dola katika nchi nyingine zenye vyama vingi vinaendeshwaje? Nchi kutofungamana na upande wowote kulitokeaje? Dunia ilikuwa na pande ngapi? Hivi sasa hizo pande bado zipo au dunia sasa ina pande ngapi? Kuwepo kwa pande kunaathiri vipi siasa za dunia? Ukishayafahamu hayo uje uuulize maswali yako, inawezekana yakawa maswali haya haya, inawezekana yakawa yamebadilika hii itategemea utakavyokuwa umeelewa na upande upi utakuwa umeegemea!
 
Taaluma ikiwekwa pemebeni na maslahi yakatangulia mbele,basi usitegemee la maana kokote
 
Ajira zimekoma kwa secta nyingine lakn kwa vijana wa mtandaon zimeongezeka. Kwa sasa kila bandiko kuna watu wanapitia!! Hapa kama kuna uchochez vile tumkamate au!!
mkuu kama wanataka kunikamata waambie wasipata tabu niko hapa kwamsisi maeneo ya kiinsio wakitaka wasipate tabu waulize kwa njilikwa
 
Kama mzazi unajisikiaje siku watoto wako wote wanapokusifu kufuatia vitisho ulivyowapa? Utachekelea ama utahuzunika? Jibu utakalotoa linatuambia jambo fulani kuhusu akili uliyonayo.
 
kwani dhambi ya kutoa taarifa ukiwa ndani ya miiko na katiba nayo tunafyata subiri nifanye maombi MUNGU atende jambo jipya
 
Mi nafikiri kabla ya kuuliza hayo maswali ungejiuliza wewe mwenyewe kama uelewa wako wa hayo mambo ni mzuri kiasi gani. Ungefahamu kwanza siasa ya ujamaa ni nini? Ungejiuliza kuwa siasa ya ujamaa haitekelezeki katika mfumo wa vyama vingi? Vyama vya kijamaa vilivyoshika dola katika nchi nyingine zenye vyama vingi vinaendeshwaje? Nchi kutofungamana na upande wowote kulitokeaje? Dunia ilikuwa na pande ngapi? Hivi sasa hizo pande bado zipo au dunia sasa ina pande ngapi? Kuwepo kwa pande kunaathiri vipi siasa za dunia? Ukishayafahamu hayo uje uuulize maswali yako, inawezekana yakawa maswali haya haya, inawezekana yakawa yamebadilika hii itategemea utakavyokuwa umeelewa na upande upi utakuwa umeegemea!
"Kuegemea", "kujiuliza", siyo swali langu, unajaribu kupiga chenga golini kwako.
Kama unayo majibu mjibie tuu, hizi sio zama za ubabaishaji.
 
Katika ngazi za kuelewa na ufahamu maswali ya moja kwa moja na yenye jibu moja yanawakilisha kiwango cha chini cha ufahamu nacho ni kumbukumbu. Maswali yenye kuhitaji tafakuri, ulinganifu na yanayoonesha uhawilishaji wa maarifa yanawakilisha kiwango cha juu cha ufahamu na fikra. Natamani utoke huko katika maswali yenye kuhitaji kumbukumbu, uje huku kwingine kama utaridhia. Kama utaridhia naamini utajiuliza hayo maswali lakini kama unapenda kubaki huko ulipo basi utaendelea na hivi viswahili vyako vya 'vibanda umiza'
 
Kwa hiyo nawe unakubali fikra za mwenyekiti zisidumu!!?
Kwani zina makosa gani mpaka zisidumu?
 
Ungejiimarisha katika kupata maarifa kama nilivyokuambia wala hutu tumaswali tudogo tudogo tusingekupa shida
 
Nape funga kila chombo cha habariiiii but usithubutu kuigusa JAMIIFORUMS. HUTAKUA NI UCHOCHEZI KIWANGO CHA LAMI
 
Ungejiimarisha katika kupata maarifa kama nilivyokuambia wala hutu tumaswali tudogo tudogo tusingekupa shida
Si utujibu basi hutu tuswali mbona unatatarika mkuu???
Tuswali twenyewe tudogo uliye na akili kubwa ungeshatujibu fasta tumekuwa tugumu?

Usipojibu hako kaswali utalidhihirishia jukwaa kuwa kaswali ni kagumu na kamekushinda

Kinachotakiwa ni kujibu swali langu siyo kujibu post yangu.
Twende kazini
 
Unajua kwenye channel za Azam king'amuzi kuna KBC, sasa wakati wa Olympic Rio ZBC walikuwa wanatangaza hayo mashindano na KBC hivyo hivo. Nadhani KBC walikuwa wakijitahidi kutangaza vizuri kwa maana kulikuwa na watu wao wengi huko. Kilichotokea ni kama vile KBC ilikuwa 'blocked' ili wafuatiliaji walazimike kuangalia na kufuatilia ZBC.Nilijua labda wameiondoa hiyo channel lakini maada ya mashindano naona imerudi.
Hizi ngonjera nataka kuonyesha kwamba vyombo vyetu vya habari sio vya kuaminika hata kidogo na ni kitu cha kusikitisha kwa wenye mapenzi mema na media!
 
Back
Top Bottom