Vyombo vya Habari vinamdhulumu Dr. Shika

Hiii kitu haikubaliki nina hakika wapo watu washatengezea pesa kwa ajili ya jina la huyu mzeee jamani tupaze sauti huyu mzeee asaidiwe wanajidai kumpenda wanamhoji wao wanauza magazeti yao hawampi kitu.huyu shigongo anajidaigi kaokoka yéyé alitaka kudhulumiwa na ccm akalia wamlipe bana
 
Mara mia wangemwacha Mzee wa watu aendelee kuishi km mwanzo tu, imekuwa bahati kuja mbele ya jamii, pia imekuwa fursa kwa vyombo vya habari ambavyo havina hurumu kumdhulumu haki yake, inatia hasira na huruma sana yani yamekazana kuujilimbikizia kuliko kusaidia
 
Uko sahihi mkuu, naona babu anatumika kutajirisha watu na yeye akibaki na umasikini uleule unaomkabili. Busara na utu vitumike kumnusuru mzee huyu.
 
"Yaani Babu yeye chakula chake ni maji tu, pale bombani anaenda na kikombe chake, basi"

Hii kauli iliniuma sana! Maskini Mzee wa watu, ningekua lawyer ningeforce king mpaka wote wanamtumia kama ngazi wangemlipa!
Kiukweli hata mimi baada ya kusikia kwamba Dk. anashinda njaa niliumia sana, mwenye namba za Dk naomba aweke hapa nimtumie pesa kidogo japo aweze kula bila kujali mabilioni aliyonayo..

Mimi ni miongoni mwa watu walioguswa na habari ya uyu daktari bila kujali stori iliyojificha nyuma yake..

Mungu ambariki na amlinde Dk. Shika
 
Wanasheria jitokezeni mumsimamie sasa sio kuongea tu humu,,tena we mwanasheria utakua maarufu na utajijengea jina vizuri
Binafsi nipo nje ya mkoa kidogo, lakini swala lipo kwa mzee mwenyewe je ana nia? Anaweza kukubali? Uenda akawa nae anaogopa au asione faida ya jambo lenyewe, kwakua mzee bado hayupo sawa kidogo na uenda ata akaja kukukana mahakamani ukaonekana wewe ndio ulitaka kumtumia upige hela... hapa swala ni tumsaidie tu kwa kuwapigia kelele hawa watu wamlipe hela.
 
Hiii kitu haikubaliki nina hakika wapo watu washatengezea pesa kwa ajili ya jina la huyu mzeee jamani tupaze sauti huyu mzeee asaidiwe wanajidai kumpenda wanamhoji wao wanauza magazeti yao hawampi kitu.huyu shigongo anajidaigi kaokoka yéyé alitaka kudhulumiwa na ccm akalia wamlipe bana
Huyo ndio muhini haswaa, kaenda kumfuata na gari alafu saa ya karudi kamtelekeza babu karudi mwenyewe kwa daladala... washamtumia na wanaingiza mamilioni.
 
Mara mia wangemwacha Mzee wa watu aendelee kuishi km mwanzo tu, imekuwa bahati kuja mbele ya jamii, pia imekuwa fursa kwa vyombo vya habari ambavyo havina hurumu kumdhulumu haki yake, inatia hasira na huruma sana yani yamekazana kuujilimbikizia kuliko kusaidia
Inaumiza sanaaa
 
Back
Top Bottom