Vyeti vya uraia na yaliyonikuta - a true story


Mkuu asante kwa ufafanuzi mzuri. Haya hayajanikuta mimi tu kuna mtu mwingine huko naye ameshuhudia watu wanaulizwa barua za balozi wa CCM.

Tiba
 
mie naishitabata washanicharge elfu 2 ajili ya kujiandikisha sabab ya muda siku hiyo sikufanikiwa nkaenda siku mbili baada ya hapo,wakaniambia eti karatasi waliyonipa imechanika so nitoe elf 2 nyingine waibadilishe nikaondoka zango kesho ntajitutumua niende na cheti cha ubatizo ndo nilicho nacho vingine vimepotea nione wataniambia upmnbav gani wakinizingua nakula kona sijiandikishi huo mda wa mtu kuzungukia serikali aza mitaa kila mda anawatu hatuna pesa mifukoni ntaupata wapi af hawa wamama wanaongea utadhani wamekunywa ma.v pambav i hate this country kwakwli
 

Wacha mawazo ya ku support a totalitalian structure. Mjumbe wa nyumba kumi ni style ya wakomunisti ya watu ku keep tabs kwa wananchi wake. Nani ana print subversive material, nani ni "enemy of the state" and some bull like that.

Na kama mjumbe wa nyumba kumi ni muhimu hivyo kwa nini asiwe neutral asiye na chama? Na CHADEMA nao wakisema wana mjumbe wao wa nyumba kumi akamtambua mtu ambaye mjumbe wa CCM hamtambui hapo itakuwaje?

Habari ya mjumbe wa nyumba kumi ilikuwa na mshiko enzi za chama kushika hatamu, ukitaka daftari la kusainiwa kupata unga wa muhogo kilo mbili kwa wiki za ugawaji shurti upitishwe na mjumbe wa nyumba kumi etc.

Sasa hivi katika mfumo wa vyama vingi, huwezi kulazimisha mtu wa CHADEMA aende kwa mjumbe wa CCM.

Ni sawasawa na kulazimisha muislamu atambulishwe na mchungaji wa kanisa la karibu.Utamkosea heshima muislamu huyu na huenda hata salamu zikagongana, muislam anasema "Wasalaam Aleikum" Mchungaji anasema "Bwana asifiwe".
 
Nadhani procedures zinazotumiwa zinaboa lakini ni za muhimu. Hata mimi ckujua kama walipita mtaani kuandikisha. Nilienda na nakala ya vyeti vyote na nikaambiwa natakiwa barua ya mjumbe. Ilibidi niifuate hiyo barua ni nipange ratiba nyingine ya cku ya kwenda kujiandikisha (nimefanikiwa)
Bila kufuata taratibu za wajumbe wa nyumba kumi nadhani kufoji kutazidi.
Passport na cheti cha kuzaliwa sio reliable sana (ukifuatilia utaratibu wa kupata hivyo vitu utagundua kuwa mtu anaweza akafoji information na kuvipata)
 
Nimezaliwa Tanzania!
Nimesoma na kumaliza shule ya msingi na secondary Tanzania!
Cheti chakumaliza masomo yangu nilichopewa nimepewa hapahapa Tanzania!
Wakati naomba maombi ya kupata Passport niliambiwa niambatanishe vyeti vyote vinavyohusu kua mimi ni Mtanzania!
Lilipofika zoezi lakujiandikisha kwenye daftari lakudumu la wapiga kura nilipewa kitambulisho cha kua mimi ni Mtanzania!

CHETI CHA URAIA KUA MIMI NI MTANZANIA NI CHA NINI????? :frusty:
 
Tiba

nenda mara ya pili kuulizia tana lakini mara hii jaribu kurekodi na kamchina kako mazungumzo yako na hao wahusika wa sensa na huyo balozi wa ccm halafu uyabandike hapa jf...hawa watu wanatakiwa waanikwe kwa sababu haiwezekani zoezi hilo hilo la aina moja likaendeshwa kwa njia tofauti tofauti...mimi sikupata shida na ilinichukua kama dk 30 hivi kumaliza zoezi lote na nilikuwa na copy ya passport na ya kitambulisho cha kupigia kura tu...!
 
Last edited by a moderator:

mbona unatumia lugha yenye jazba?.kwani ukiongea kwa upole na unyenyekevu hatakuelewa? yote uliyojifunza hapa duniani, ungefundishwa kwa maneno makali namna hii ungelielewa?. kama unafahamu jambo, basi ujisikie fahari kumuelimisha mwingine, na hii fahari uipate pale anapokuonyesha amekuelewa. lakini unaonekana upo ktk msingi wa kumkosoa zaidi tena kwa kuonyesha namna gani hawezi kuwa kama wewe, na si namnagani ungelitaka awe kama wewe.
 
nimemshangaa sana mkuu wangu hapo...angekuja huku mbezi juu watu tunakwenda kujisajili na kujaza form hapohapo na hakuna cha balozi wala nyau yeyote anayethibisha kama unaishi mtaa husika...
 
nimemshangaa sana mkuu wangu hapo...angekuja huku mbezi juu watu tunakwenda kujisajili na kujaza form hapohapo na hakuna cha balozi wala nyau yeyote anayethibisha kama unaishi mtaa husika...

ni kweli. ila tufahamu wakati tunapata matatizo au ukinzani ktkt jambo fulani, twaweza kuona kama haiwezekani kutatuliwa au tunaonewa, lakini ndo hivyo, mtu kaongea , ni swala la kumuongoza afanye nini , na si ku mshambulia, yote ya yote hata hatumjui kwa sura.
 

Lakini nijuavyo mimi Mwenyekiti wa mtaa au kijiji anachaguliwa na wananchi wa mtaa wake
Sasa kama nyinyi mlimchagua wa chama ambacho hukipendi hiyo haimhuusu huyo karani

Tatizo letu wakati wa uchaguzi/upigaji wa kura wa hao viongozi wa chini kabisa huwa hatushiriki na wala hatutaki kuwajua na hata kujua majukumu yao
 

Pole mkuu kwa yaliyokukuta, ndio serikali ya CCM hiyo na vimbwanga vyake!!!

Tiba
 

Asante mkuu kwa ushauri. Hawa jamaa wa ubungo mziwa wametengeza mradi wa kupata pesa kwani hata kwa balozi barua haitoki hivi hivi bila kutoa elfu mbili. Pamoja na passport na cheti cha kupiga kura nilikuwa na vyeti vya shule vile vile lakini binti alisisitiza anataka barua ya balozi wa CCM.

Hiyo ndio Tanzania Bwana, kila mmoja anaamua lake wakati zoezi ni hilo hilo moja!!!

Tiba
 

Mkuu bahati nzuri mwenyekiti wa serikali ya mtaa tunafahamiana vizuri na tumeishi mitaa ile kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Ningetakiwa nilete barua kutoka kwake isingekuwa tatizo, shida binti alisistiza nipeleke barua ya balozi tu, aliseam hiyo ya serikali ya mtaa haitaki!!!! Haya ndio maajabu ya musa!!!!

Tiba
 
Mkuu umejitahidi kueleza vizuri lakini umepoteza point ulipodai wajumbe wa nyumba 10 ni watendaji wa serikali. Hii imeanza lini? Hawa wajumbe wanapatikana vipi? Nipe hayo majibu kwanza, halafu tuendelee!!!!

Tiba

Hii inadhihirisha jinsi usivyo mshiriki wa mambo yanayoihusu jamii yako. Mjumbe wa nyumba kumi huchaguliwa na wananchi na ndio maana hapa kwetu mjumbe wetu ni mwanachama wa CUF na ofisi ya serikali ya mtaa inamheshimu regardless ya chama chake.

Tatizo letu ni kwamba, wengi wetu tuna mentality za ajabu za kudhania kwamba, kujihusisha na mambo ya jamii yako ni dalili ya kutosoma.
 

Fuatilia post zake and try to read btn the lines. Kinachomsumbua ni superiority complexion. Anaamini yeye ni mtu fulani asiyehitaji kujinyenyekeza kwa mjumbe wa nyumba kumi kwa kuwa yeye amesoma na in most cases wajumbe hawa ni watu wazee ambao kwa aina ya utumishi wa kazi yenyewe, huwa ni wale wasio na shughuli.

Sina lugha nyingine ya kuongea na mtu wa namna hii ili apate kujua makosa yake.

Au na wewe una akili fupi kiasi udhanie kuwa kwa kuangalia cheti chako cha chuo, karani anaweza kufahamu uhalali wa ukaazi wako katika mtaa husika?
 

Mimi sijakuelewa unakosoa muundo au unaukataa umuhimu wa wajumbe wa nyumba 10?

Hilo jina la WAJUMBE WA CCM ni mapokeo, lkn hapa anayezungumziwa ni Balozi wa Nyumba kumi. Hapa ninapoishi miaka mingi alikuwa ni mama mmoja wa CCM lkn mwaka juzi tulimchagua Babu Muha ambaye ni CUF. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu ni CHADEMA na wajumbe wa serikali ni vyama mchanganyiko. Sasa mimi sijaelewa kinakuuma wapi mjumbe akiwa CCM.

Tuache akili za kitoto. Cha msingi hapo kwenu ni kuitisha uchaguzi mpya wa mjumbe na wewe ugombee kwa tiketi ya chama chako. Sisi tulimchagua Babu Muha wa CUF kwa mapenzi yetu na anatuwakilisha, sasa wewe usiyejua mjumbe wako alichaguliwa na nani unalalamika nini kama sio utoto?

Akili zetu ndio hizi, hatutaki kugombea, hatuendi kuchagua lkn ataechaguliwa tunampinga kwenye majukumu na kujiita wasomi, ndio nini sasa?
 

Ujinga wetu ndio huu, kujaribu ku-complicate kila kitu kwa kuwa tu hakiko in our favor. Sasa sisi kwetu balozi wetu ni mwanachama wa CUF, ina maana na sisi wa CDM tumkatae?

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni CDM, ina maana na wenzetu wa CCM na CUF wamkatae?

Kama una akili zitumie, yule mkuu wa mkoa wenu ni wa chama chako? Kama si wa chama chako, that means hamuivi kiitikadi, je umeshamkataa? Vipi kuhusu diwani na mbunge, wote ni wa chama chako?

Kabla hujabishana jaribu kufikiri. Mimi hapa nazungumzia UMUHIMU WA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI. Hao wajumbe wa CCM unawajua wewe na wasomi wenzio ambao mnadhani cheti na passport kinaweza kukutambulisha unakaa mtaa gani.
 
Mkuu, walipita siku gani? Mimi sikai nyumbani kusubiri kuandikishwa ndugu yangu, nina mihangaiko kibao hapa mjini. Nikitoka saa 12 asubuhi narudi wakati mwingine usiku mwingi.

Tiba

Umeona sasa jinsi akili nyingi na ujuaji unavyoponza? Na haya ndio niliyoyaita majivuno na tambo za USOMI NJAA. Hivi unataka kuniambia mtaani kwenu ni wewe tu ndio mwenye ajira?

Haya ndio madhara ya kutokuwa karibu na jamii inayokuzunguka. Sawa hukuwepo, lkn una majirani na huyo mjumbe wa nyumba kumi alikuwa na makarani waliopita kuandikisha. Nijuavyo mimi, kwa maeneo ambayo watu ni washiriki wazuri wa shughuli za kijamii, hufahamiana na kupeana habari.

Nachokiona, una majivuno na kujitenga kwingi. Sawa, hukujua juu ya hili zoezi kwa kuwa huelewani na mjumbe wako, vipi kuhusu vyanzo vingine vya habari. Suala la NIDA limekuwepo hata hapa jamvini, sasa wewe ulitaka serikali ikutengee karani maalum ili akuvizie siku ambayo hujaenda kwenye shughuli zako au?
 

Mie sina chama na kwetu hakuna upuuzi huu wa wajumbe wa nyumba kumi kwani hatuamini katika ukomunisti wa chama na serikali ku monitor wananchi kama ng'ombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…