Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Kitaifa,-- Serikali inaanzia kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Afisa Mtendaji Hawezi kukusaidia lolote kama hautakuwa na utambulisho wa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa unaoishi, Na mwenyekiti wa serikali ya MTaa pia hawezi kukusaidia kama hautakuwa na Barua ya Mjumbe wa Nyumba Kumi........................, Utaratibu ndio ulivyo, Ile barua ya Mjumbe wa nYumba kumi inaishia Kwa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa, na Barua ya Mwenyekiti wa Seriklai ya Mtaa inaishia kwa Afisa Mtendaji, na Barua ya Afisa Mtendaji ndio inayoingia kwenye Maofisi yote na ndio Barua rasmi ya kiserikali inayokutambulisha ..............................Kama mambo ya Kimahakama, Uhamiaji, nkHaya ya wajumbe kutojulikana ndio nasikia na wewe. Na nafikiri usiyeelewa hapa ni wewe na huyu mwenzio unayezidi kumpotosha. Chain ya utambuzi huanzia kwa hao unaosema hawajulikani. Kwa mfano, kama umeambiwa upate barua ya dhamana ya Afisa Mtendaji wa Kata, itakulazimu kufuata hatua zifuatazo:1. Uende kwa mjumbe wa nyumba kumi akuandikie barua ya utambulisho. Afisa Mtendaji wa mtaa atahitaji ushahidi toka kwa mjumbe wako kuwa anakufahamu. (Nikukumbushe kuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa na Kata ni waajiriwa wa Serikali kuu na wanaweza wakawa si wakazi wa eneo husika)2. Baada ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wako kuridhika (baada ya kupata uthibitisho wa mjumbe wa nyumba kumi) atakupa barua ya kukutambulisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata kuwa umetokea kwenye mtaa wake. Na yeye ndio atakusikiliza.Nitashangaa sana kama Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kata atakuandikia barua ilhali hajui unakaa nyumba gani wala uchochoro gani. Hebu tutumie akili zetu vizuri wakuu