Vyeti vya uraia na yaliyonikuta - a true story

Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,604
3,163
Wana Jamvi,

Juzi tarehe 31 July 2012 niliamua niwe mmojawapo wa raia wema kwa kuitikia mwito wa kwenda kujiandikisha. Kwa yanayotangazwa redioni na kwenye magazeti, tunapashwa kwenda kujiandikisha kwa kuonyesha kitu ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba mimi ni raia. Nilikwenda kujiandikisha pale Ubungo Maziwa ambako mwenyekiti wetu wa mtaa anaitwa Jovin Ndimbo. Huyu jamaa anajulikana kwa kupokea rushwa na ofisi yake haiwezi kukupa huduma yoyote bila kutoa pesa.

Nilifika pale kituoni kwenye mida ya saa kumi jioni na kupanga foleni kwa karibu dakika 45 kabla zamu yangu ya kuandikishwa haijafika. Binti aliyekuwa anaandikisha pale ana umri kama wa miaka 22 hivi. Nilipofika akaniuliza barua ya balozi iko wapi? Nikamuuliza balozi yupi huyo? Akaniambia balozi wako wa nyumba kumi. Nikamuuliza balozi wa chama gani? Akaniambia balozi wa CCM. Nikamuuliza balozi wa CCM anaingilianaje na zoezi la watu kuandikishwa uraia?

Yule binti nilimuonyesha passport yangu original na vyeti vyangu vya shule vya ngazi mbali mbali lakini (nilikuwa na copy ya vitu vyote vile vile) alikataa kabisa na kusisitiza kwamba bila barua ya balozi hawezi kuniandikisha. Nilisikitika sana.

Je ni kweli barua ya balozi wa CCM ni mojawapo ya masharti ya mtu kuandikishwa uraia? Hapa balozi wa CCM wanahusikaje? Nilimwambia kama anataka barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa ninaweza kumuelewa lakini balozi wa CCM hapana. Binti alikataa kuniandika na kwa kuwa sikutaka kubisha naye, niliamua kuondoka na hivyo kushindwa kujiandikisha.

Nina wasiwasi huyu Ndimbo ambaye ni mwenyekiti wa mtaa ameamua kuwashirikisha mabalozi na kuwaamrisha kupokea kitu kidogo kabla ya kutoa barua. Baadae nilitaarifiwa kwamba bila Shs. 2,000 balozi hakupi hiyo barua.

Halafu tukiichukia CCM watu wanatushangaa!!!! Je kuna mtu mwingine amekutana na hadha hii?

Tiba
 
Hii hatari wamewaambukiza mpaka hawa sisimizi wadogo. We realy have a long way to go kwa kweli.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mi ninavyojua...kuna watu walikuwa wakipita kila nyumba kuandikisha majina...sasa kama ulikuwapo kwenye ilw list then huna haja ya barua we ni kwenda tu direct ukajaze form...Ila kama hukuandikwa kipindi kile then inabidi uende kwa mjumbe wako(sijui wa nyumba 10 ama mtaa) halafu yeye atakupa barua ambayo inabidi uipeleke katika serikali ya mtaa...then kule unaandikishwa tena kwenye lile daftari. Baada ya hapo sasa unachukua zile copies zako unaelekea shule ya msingi...huko ambako wewe Tiba uliletewa zengwe...huko ndio unakojiandikisha.
 
Duh! Kama ndio hivyo, kuna hatari ya mimi kukosa hicho kitambulisho. Kuna balozi wa ccm hapa mtaani hatuelewani wala hatuongei tangu alipokuja kwangu asubuhi eti anakusanya michango ya ujenzi wa shule za kata! Nilimtimua na kumwambia aende akachukue tra maana wananikata kodi kila mwezi kwajili ya huduma za jamii ikiwemo elimu! Ananichukia na hata nikimsalimia haitiki. Sasa kama ni lazima nikafuate barua kwake, basi kazi ninayo!
 
Inawezekana kabisa mdada haelewi tofauti kati ya balozi wa CCM na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa.

Kaona umemletea ujuaji ofisini kwake, kaamua kukuletea ngumu tu kwa kuwa hataki ku lose face.

Nishakutana nazo sana hizi bongo. Mtu yuko ofisini kwake, hajui kazi, ukimuuliza maswali sana na kuonekana unaelewa issues kuliko yeye anakuwekea ngumu tu.

Hakieleweki mpaka barua ya Balozi wa CCM.

Mtu yuko ofisini kwake.

Noma.
 
Mkuu Tiba mie naona tatizo liko kwako, kabla ya zoezi la kujaza fomu, hawa makarani walipita nyumba hadi nyumba wakiandika majina ya wakaazi wakiwa na huyo mjumbe wa ccm. Iwapo kwako walipita na labda hukuwapa ushirikiano basi ndio haya yalikukuta.
 
Last edited by a moderator:
Hili zoezi la kuandikisha uraia linaendelea mpaka lini wakuu?
 
Hilo suala la barua au utambulisho wa mabalozi wa CCM nadhani lipo maeneo mengi.....Hata mimi nimekumbana nalo.Lakn nadhani sio fair kabisa kwa watu wasio wanachama wa CCM...lakn ndio hivo tena.Labda tume imepewa utaratibu na mwongozo kuhusu hilo.
 
Mkuu Tiba mie naona tatizo liko kwako, kabla ya zoezi la kujaza fomu, hawa makarani walipita nyumba hadi nyumba wakiandika majina ya wakaazi wakiwa na huyo mjumbe wa ccm. Iwapo kwako walipita na labda hukuwapa ushirikiano basi ndio haya yalikukuta.
Nadhani hujamuelewa mtoa mada.Analalamika kuhusishwa kwa mabalozi wa CCM au wajumbe wa nyumba kumi
...Labda kama kuna uhusiano kati ya wajumbe wa CCM na wajumbe wa serikali za mitaa...hiyo itakuwa kesi nyingine...
 
Mdau Tiba kuna tatizo kubwa sana Dar kuhusu namna mfumo wa serikali unavyofanya kazi tangu mwaka 1992 nchi ilipoingia kwenye vyama vingi. Dar watu wengi including watumishi wa taasisi mbalimbali hawajui namna mfumo wa serikali ya mtaa na serikali kuu inavyofanya kazi japokuwa ni kitovu cha nchi na ndio maana utakuta mabalozi wa nyumba kumi au wajumbe wanakuwa wana sauti wakati kwenye mfumo wa serikali hawajulikani na wakati mwingine unaweza kwenda na barua ya mtendaji wa kata ukaambiwa leta barua ya mujumbe badala ya mwenyekiti wa mtaa au mtendaji wa mtaa ambao wanatambulika kisheria.

Huwa tunawasingizia watu wa vijijini sijui elimu itolewe kwao lakini kiukweli ukienda kijijini haya hata kama kipo Itabagumba, Kebanchbancha, Imalamakoye au Ubenanzomonzi wanajua kabisa kwamba anaetakiwa ku-verify taarifa ni mtendaji wa kijiji au kata but reference inatoka kwa mwenyekiti wa kitongoji but kwa mjini ni mtendaji wa mtaa kama yupo japo miji mingi huwa hawapo au mwenyekiti wa mtaa ambae ataverify ila kuipa nguvu unakwenda kwa mtendaji wa kata ambae anamwakilisha mkuruguenzi wa manispaa. Pole sana haya ndio matatizo yaliyopo Dar wajumbe na mabalozi wana nguvu kama nini mpaka kwenye kuuziana ardhi (somo halijafika kwa watu wengi tangu 1992 tulipoingia vyama vingi wakati vijijini wao hawana shida na hili)
 
Inasikitisha kuona Watanzania wagume kuelewa ni wale wanaojisifu kuwa wamesoma. PASSPORT, DEGREE na sijui nini kingine ulichosema havina nafasi katika kukutambulisha wewe kama individual unaishi mtaa gani. Kwa faida yako na wasiojua wengine nitatumia muda wangu kukueleza/kuwaeleza nini nia ya NIDA kufanya zoezi, jinsi zoezi lilivyoenda na malengo ya mwisho.

Kabla ya kujaza fomu za maombi ya KITAMBULISHO, NIDA kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa, iliandaa zoezi la utambuzi wa kaya na makazi kwa kila mtaa. Makarani wa NIDA wakiambatana na WAJUMBE WA NYUMBA KUMI walipita nyumba hadi nyumba kuwasajili wakazi kwenye DAFTARI LA WAKAZI LA MTAA. (Wajumbe wa Nyumba 10 na sio wa CCM) Nikukumbushe kuwa, wengi wa mnaojifanya mmesoma (ilhali vichwani hamna kitu) mlipuuzia zoezi hili na kuwapa wakati mgumu makarani kwa kutotoa ushirikiano kwenu. Muda uliopangwa uliisha na NIDA iliongeza siku 7 za ziada, na bado wengine mligoma kusajiliwa.

Zoezi la usajili wa kaya na wakazi lilipoisha, likaanza zoezi la ujazaji fomu. Hapa sasa na the so called wasomi mkajitokeza. Tatizo likaja kuwa, ili upate uhalali wa kujaza fomu ya maombi ya kitambulisho, inakupasa uwe umeshaorodheshwa katika daftari la mtaa. Sasa lile si daftari tu kama la rambi rambi kwamba kila anayepita na buku yake anaandika, la hasha. ILIPASA UTHIBITIKE haswa ya kwamba u-mkaazi wa eneo husika. Sasa nani anakutambua kama mkaazi, jibu linakuja MJUMBE WA NYUMBA 10.

Kumbuka kuwa, wakati wa uandikishaji wa mitaani (majumbani) mjumbe alikuwa na hao makarani kwa hiyo wote walioorodheshwa wakati huo, walidhaminiwa na mjumbe. Sasa iweje wewe leo hii uje na vyeti vyako vya shule vikutambulishe? Hivi umesoma nini ikiwa unashindwa kuelewa kuwa cheti chako cha chuo hakiwezi kueleza kama unaishi Keko au Mbagala?

Bwana Tiba, serikali ina ngazi mbali mbali za utendaji. Ngazi ya chini kabisa ni mjumbe wa nyumba 10. Ni ujinga na ni ujuha kudharau mjumbe wako wa nyumba kumi na wala kutomjua kwako hakudhihirishi usomi bali upumbavu. Hivi serikali hiyo hiyo iliyokusomesha ikikuhitaji wewe kwa maoni yako unadhani itamtumia nani kukufikia, ALIYEKUANDIKIA HAYO MAVYETI YAKO AU MJUMBE WA NYUMBA KUMI AMBAYE UPO NAYE MTAANI?

Swala la wajumbe kuwa wa nyumba kumi au wa CCM hiyo ni tafsiri tu iliyoletwa na mazoea ya wakati ule wa chama kimoja. Hapa ninapoishi, mjumbe wetu ni wa CUF na mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni Wilbald Mlamba wa CHADEMA. Sisi tunamtambua balozi wetu kama wa nyumba kumi na sio kwa jina la chama chake.

Najua kwa mentellity ya 'KIUSOMI' hautapenda kunielewa lkn ni kwa faida yako. Wenzio waliokuwa nyumbani mjumbe alikuwapo kuwatambua wakaingizwa kwenye daftari, wewe umekuwa nani utambulishwe na vyeti? Hivi ukinionesha passport yako hiyo itanithibitishiaje kuwa unakaa mtaa husika na hukai mtaa mwingine?

Wapendwa, passport yaweza kukutambulisha umetokea nchi gani na sio mtaa gani au ni nini kigumu kuelewa hapo? Hivi leo nikikupa cheti changu cha chuo kikuu unaweza kukisoma na kuniambia ninakaa nyumba namba ngapi?

Kama humjui mjumbe wako wa nyumba kumi hiyo ni dalili hushiriki hata katika shughuli za maendeleo na kijamii mtaani. Hujui cha kukarabati barabara wala harambee ya kufanya iusafi wa mazingira, na nyie ndio wasomi njaa mnaojivunia vyeti bila kuwa na ufahamu hata mambo madogo.

Adha umeitaka mwenyewe kwa kutoandikwa nyumbani kwako. Nenda kwa mjumbe akuandikie barua ili huyo karani akutambue kuwa wewe kweli ni makazi wa eneo hilo ndio sasa atakuandika kwenye daftari na utaruhusiwa kujaza fomu. Vyeti utavitumia kuomba kazi na kujisifia kwa wajukuu zako kuwa ulimaliza madarasa, na passport utaitumia kujitambulisha utapokuwa nje ya mipaka ya Tanzania.

Halafu ni ADHA ndugu msomi na sio HADHA. Siipendi CCM lkn sio sababu ya kunifanya niwe mjinga kwa kutomtambua mjumbe wa nyumba 10.

Las Mas Bobos
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hujamuelewa mtoa mada.Analalamika kuhusishwa kwa mabalozi wa CCM au wajumbe wa nyumba kumi
...Labda kama kuna uhusiano kati ya wajumbe wa CCM na wajumbe wa serikali za mitaa...hiyo itakuwa kesi nyingine...

KUmbe mko wengi!

Hivi kwa akili tu ya kawaida, mwenyekiti wa serikali ya mtaa anaweza kuwatambua wakaaazi woooote wa mtaa wake?
 
Mdau Tiba kuna tatizo kubwa sana Dar kuhusu namna mfumo wa serikali unavyofanya kazi tangu mwaka 1992 nchi ilipoingia kwenye vyama vingi. Dar watu wengi including watumishi wa taasisi mbalimbali hawajui namna mfumo wa serikali ya mtaa na serikali kuu inavyofanya kazi japokuwa ni kitovu cha nchi na ndio maana utakuta mabalozi wa nyumba kumi au wajumbe wanakuwa wana sauti wakati kwenye mfumo wa serikali hawajulikani na wakati mwingine unaweza kwenda na barua ya mtendaji wa kata ukaambiwa leta barua ya mujumbe badala ya mwenyekiti wa mtaa au mtendaji wa mtaa ambao wanatambulika kisheria. Huwa tunawasingizia watu wa vijijini sijui elimu itolewe kwao lakini kiukweli ukienda kijijini haya hata kama kipo Itabagumba, Kebanchbancha, Imalamakoye au Ubenanzomonzi wanajua kabisa kwamba anaetakiwa ku-verify taarifa ni mtendaji wa kijiji au kata but reference inatoka kwa mwenyekiti wa kitongoji but kwa mjini ni mtendaji wa mtaa kama yupo japo miji mingi huwa hawapo au mwenyekiti wa mtaa ambae ataverify ila kuipa nguvu unakwenda kwa mtendaji wa kata ambae anamwakilisha mkuruguenzi wa manispaa. Pole sana haya ndio matatizo yaliyopo Dar wajumbe na mabalozi wana nguvu kama nini mpaka kwenye kuuziana ardhi (somo halijafika kwa watu wengi tangu 1992 tulipoingia vyama vingi wakati vijijini wao hawana shida na hili)

Haya ya wajumbe kutojulikana ndio nasikia na wewe. Na nafikiri usiyeelewa hapa ni wewe na huyu mwenzio unayezidi kumpotosha. Chain ya utambuzi huanzia kwa hao unaosema hawajulikani. Kwa mfano, kama umeambiwa upate barua ya dhamana ya Afisa Mtendaji wa Kata, itakulazimu kufuata hatua zifuatazo:
1. Uende kwa mjumbe wa nyumba kumi akuandikie barua ya utambulisho. Afisa Mtendaji wa mtaa atahitaji ushahidi toka kwa mjumbe wako kuwa anakufahamu. (Nikukumbushe kuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa na Kata ni waajiriwa wa Serikali kuu na wanaweza wakawa si wakazi wa eneo husika)
2. Baada ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wako kuridhika (baada ya kupata uthibitisho wa mjumbe wa nyumba kumi) atakupa barua ya kukutambulisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata kuwa umetokea kwenye mtaa wake. Na yeye ndio atakusikiliza.

Nitashangaa sana kama Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kata atakuandikia barua ilhali hajui unakaa nyumba gani wala uchochoro gani. Hebu tutumie akili zetu vizuri wakuu
 
Naomba mtambue Balozi wako wa nyumba 10 wala usijali ametokea Chama gani kwani yeye ndio anajua km kweli mwenye Nyumba wako kakupangisha, hata km umejenga lazima umtambue balozi wako kwani kati ya nyumba 10 mojawapo ni yako na 9 zilizobaki zote anazisimamia yeye. Fika kwake tu atakapogoma ndio kamshitaki kwa Mtendaji kuwa hakutambui kwa maugomvi yenu mengine
 
hvyo ulikua na maana gan ulipoanza kumuuliza yule dada kua anahitaji barua ya baloz wa chama gan?nina wasiwasi na wrong perception ktk maelezo yko
 
hvyo ulikua na maana gan ulipoanza kumuuliza yule dada kua anahitaji barua ya baloz wa chama gan?nina wasiwasi na wrong perception ktk maelezo yko

Hawa ndio wale wajuaji wanaotaka kuleta kujua kwao kwenye kila jambo. Yeye kaanza na kumuuliza mjumbe wa chama gani.

Mwingine nae anasema DADA ALISHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA MJUMBE NA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA, hivi huyo mwenyekiti anawezaje kuwatambua wananchi wote kama mabalozi wa nyumba 10 hawatawatambulisha kwake!

Nchi yetu ina safari ndefu sana na hizi shule za kata na vyuo vya baba kanasa. Imefikia sehemu mtu anaona ni fahari kutomtambua mjumbe wake wa nyumba kumi.

Wasomi kwa faida yenu, hata Mkuu wa Wilaya anamtegemea Mjumbe wa nyumba kumi kukutambua wewe. Tusijivunie uvichwa maji eeeeeh
 
Back
Top Bottom