Vyeti vya uraia na yaliyonikuta - a true story

Mie sina chama na kwetu hakuna upuuzi huu wa wajumbe wa nyumba kumi kwani hatuamini katika ukomunisti wa chama na serikali ku monitor wananchi kama ng'ombe.

Chama gani tena, kwani mabalozi wote ni wa CCM?

Hivi kwa akili ndogo tu, hii kata yetu ya manzese ina individuals 109,208 (makisio), sasa bila wajumbe hivi huyo mwenyekiti wa mtaa ataweza kuwatambua watu wote hao?

Tumieni akili wakuu, serikali inawategemea wajumbe hao. Hata Bank ukienda kuomba mkopo, itataka upate udhamini kwa serikali ya mtaa na wanaomba hivyo kwa kujua kuwa, ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa tu ndio anaweza kuonesha physical location yako. Sasa je, mwenyekiti wa mtaa pale manzese ambapo nyumba za kupanga ni lukuki anaweza kweli kuwajua wakaazi wote bila msaada wa balozi wa nyumba kumi?

Wewe ndio ng'ombe, kwani ng'ombe ndio hajui mamlaka.

Gombea ujumbe na wewe sio kupiga kelele ukomunisti ukomunisti. Sijui kama umewahi kusoma hata darasa moja
 
Chama gani tena, kwani mabalozi wote ni wa CCM?

Na mie nisiye na chama naruhusiwa kugombea ubalozi kama mtu binafsi? Mie sijaona chama kinachonifaa na naona nina mchango.

Hivi kwa akili ndogo tu,

Tatizo linaanzia hapa. Unataka kutumia akili ndogo tu kila wakati.

hii kata yetu ya manzese

Tatizo lingine hili hapa

ina individuals 109,208 (makisio),

Huna hata hakika na unachoandika.

sasa bila wajumbe hivi huyo mwenyekiti wa mtaa ataweza kuwatambua watu wote hao?

Kama huna system hata hao wajumbe hawawezi kuwatambua watu wao, sema jingine.

Tumieni akili wakuu,

Wewe unayetumia akili ndogo ndo unaambia wengine watumie akili?

serikali inawategemea wajumbe hao.

Kwamba serikali inawategemea halisemi lolote kuhusu umuhimu au uhalaliwao kama walivyo sasa.

Hata Bank ukienda kuomba mkopo, itataka upate udhamini kwa serikali ya mtaa na wanaomba hivyo kwa kujua kuwa, ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa tu ndio anaweza kuonesha physical location yako.

Kwa hiyo process za bank ndiyo gold standard siyo?

Sasa je, mwenyekiti wa mtaa pale manzese ambapo nyumba za kupanga ni lukuki anaweza kweli kuwajua wakaazi wote bila msaada wa balozi wa nyumba kumi?

Pale Manzese kabla hujataka kupanda juu huko kwenye kuongelea ustaarabu wa civic duty na citizenship pasafisheni kwanza, mpate kukaa kwa mpangilio kwanza, kabla ya kujitia mna verify address wakati watu wanakaa katika mabanda na vyumba vya kupanga wanahama kila asubuhi. And that goes for all the rest of the Dar slums.

Tatizo kujitia tuna mipango kwa level ya juu ku verify address wakati Watanzania karibu wote address zao ni P.O.Box na Plot number.

Wewe ndio ng'ombe, kwani ng'ombe ndio hajui mamlaka.

To the contrary. Ng'ombe hajui kuuliza mamlaka, ukimtandika vizuri tu anafyata mkia.Wewe ushatandikwa sana hata kuiuliza mamlaka ya serikali huwezi. Serikali ikitaka u verify physical address unakubali tu hata kama unakaa kwenye kiota kilicho juu ya genge la nyanya Manzese huko.

Gombea ujumbe na wewe sio kupiga kelele ukomunisti ukomunisti. Sijui kama umewahi kusoma hata darasa moja

Wanaruhusu tusio na vyama kugombea?
 
Hao wajumbe na mabolozi wa nyumba kumi sikatai kwamba hawakubaliki ila katika mazingira ya watu roho safi na wasiomind vitu vidogovidogo na ndio maana serikali inatambua mpaka vyeti vya ubatizo kama kielezo. Hao viongozi ni wa kichama na si wa kiserikali na hiyo shughuli ni ya kiserikali na ndio maana mwaka 1992 tulipoingia vyama vingi kulikuwa kuna watu wanaitwa makatibu kata ambao walikuwa wanafanya kazi kama watendaji wa chama na watendaji wa serikali wakaondolewa na kuleta position ya Mtendaji wa kata ili afanye kazi za serikali bila bias watu wasiseme ni wa chama flani pia katika ngazi ya mtaa ikawekwa post ya mwenyekiti wa mtaa ambae huwa anachaguliwa na wananchi wa mtaa husika na ambae ndio mwakilishi wa rais ktk ngazi ya mtaa pia kunakuwa na afisa mtendaji wa mtaa ambae anamwakilisha mkurugenzi wa manispaa. Mtandaji wa kata anachukua utambulisho toka kwa mtendaji wa mtaa ambae anafanya kazi kwa karibu na mwenyekiti wa mtaa ambae ni mwakilishi wa wananchi ambae anatambuliwa na sheria mpya ya serikali za mitaa na ndie anaishi na hao wananchi mtaani na anawafahamu watu wake nikiwa na maana yeye kama mwenyekiti ndio anatakiwa atumie mbinu kuhakikisha kwamba yule ni mkazi wake si mjumbe au balozi wa nyumba kumi ambao ni viongozi wa kichama ambao wanawakilisha issues zote related na siasa> Hii imekuja baada ya nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi 1992 lengo ni ku-avoid bias ila kwa issue ya vitambulisho si mbaya kumtumia pia mjumbe kwa kuwa ni issue ya kitaifa. Lakini linapokuja suala kama la uchaguzi mdau wangu Las Mas Bobos hapo inakuwa kasheshe mtu anapotaka kujiandikisha kupiga kura umwambie akalete barua kwa mjumbe au balozi). Huo utaratibu unaotumika Dar ni kile kitu tunachoita mazoea hivyo imetokea utaratibu ndio huo miaka kama minne iliyopita mpaka bank ilikuwa unaambiwa uje na barua ya mjumbe. KWA MUJIBU WA SHERIA YA SERIKALI YA MITAA, SERIKALI INAANZIA KATIKA NGAZI YA mtaa kwa mjini na NGAZI YA kitongoji kwa vijijini, hiyo issue ya mabalozi wa nyumba kumi na wajumbe tunaitumia tu kimazoea ni kama vile issue inatakiwa aifanye Mkurugenzi wa mji,jiji au manispaa mtu anakwenda kwa meya wa mji au mkuu wa wilaya.

Mkuu usipende kukurupuka na theories zako na kusema huo ndio msimamo wa serikali. Mimi ni karani wa NIDA katika hilo zoezi linalozungumziwa hapa, na nakuhakikishia kuwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI WANATAMBULIWA NA SERIKALI KUU kama sehemu ya serikali ya mitaa.

Wajumbe wa nyumba kumi si lazima watoke CCM. Ni ule uzito tu wa mwitikio kutoka kwa watu wa vyama vingine kuchukua nafasi hizi ndio unasababisha ionekane kuwa hawa ni wajumbe wa CCM badala ya wajumbe wa nyumba kumi.

Yapo maeneo mengi tu ambapo wajumbe wa nyumba kumi wanatoka vyama vya upinzani, sasa mimi sioni shida ilipo ilhali hawa ni muhimu zaidi ktk suala la utambuzi. Nimejitahidi kueleza labda niongezee tu kwa mifano ili ndugu wengine mpate kuelewa.

Serikali kuu inatambua uwepo wa wajumbe wa nyumba kumi na inawatumia kufanikisha operesheni zake nyingi tu, mwenye akili na aelewe na mwenye kutaka kubisha na aendelee kubisha.

1. Askari akitaka kusachi nyumba yako analazimika kumtaarifu mjumbe wa nyumba kumi ili awepo na kushuhudia uhalali wa zoezi hilo na usalama wa mtuhumiwa.

2. Askari hawezi kukutia nguvuni mtaani kwako bila kumtaarifu mjumbe wako juu ya sababu ya kukuchukua isipokuwa kama itadhihirika kuwa unaleta hatari iliyo wazi.

3. Mahakama ikitoa SUMMONS ama wito mwingine wowote ule, wito huo utapitia kwa mjumbe wako wa nyumba kumi. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa hawezi kujua wewe bwana Tiba umepanga chumba cha uwani nyumbani kwa nani kule Tandale, lkn balozi wako atajua.

4. Kwenye hili zoezi la Vitambulisho, NIDA inamlipa posho ya Tshs 10,000 mjumbe wa nyumba 10 kuwaongoza makarani kwenye nyumba zake na kuwasaidia kwa watu watakaogomea kutoa ushirikiano. Hii inadhihirisha serikali inawatambua wajumbe

5. Tarehe 26, tuna zoezi zito la Sensa, kumbukumbu yangu ya Sensa ya mwaka 2002, wajumbe wa nyumba kumi walituongoza kwenye nyumba zao. Hapa nitawapa ufafanuzi kidogo:
-Waweza kumuuliza mtu juu ya mume au mke wake ilhali amemzika juzi tu wewe karani hujui nadhaniutaishia kushangaa mama unayemhoji analia nini, lkn mjumbe ana nafasi ya kukutahadharisha
-Si rahisi mwenyekiti wa serikali ya mtaa kujua kama nyumba fulani ina wapangaji au ni kaya moja tu. Lkn mjumbe ana nafasi ya kuwa na taarifa zaidi.
-Wapo watu wanaficha taarifa za watu wenye ulemavu kwenye kaya zao, lkn mjumbe anaweza kujua taarifa hizi kwani anaishi nao hapo mtaani

Mimi siamini kama serikali haitambui wajumbe wa nyumba kumi. Ni sisi wananchi ndio tunadharau wajumbe kwa kutojua umuhimu wa ngazi yao katika utambuzi.

Kwenye daftari la WAKAZI lililoratibiwa na NIDA, kila individual alipaswa kudhaminiwa na watu wawili ili kuthibitisha ukaazi wake ktk mtaa. Wa kwanza ni MJUMBE na wa pili ni aidha MKUU wA KWAYA (kwa wenye makazi binafsi) au MWENYE NUMBA (kwa wanaoishi kwenye nyumba za kupanga), sasa ndugu zangu wajuaji hebu nielezeni, hivi Mwenyekiti wa serikali ya mtaa angewezaje kuwatambua watu wote wa mtaa wake?

Ndio wajuaji nyinyi nyinyi kesho mtasema kuna Msomali mtaani kwetu haeleweki anaishije lkn mwenyekiti yupo tu bila kujali kuna watu 18,303 katika Mtaa wa Mwongozo uliopo kata ya Makuburi. Yaani kwa akili zenu na mifano na manung'uniko, mnataraji mwenyekiti na wajumbe wake 9 wawajue watu woote hawa 18,000!

Tusipende kuwa wajuaji wajinga. NIDA imetangaza hivi kwenye vyombo vya habari: Ikiwa una mgonjwa, mlemavu au mzee katika kaya yako, RIPOTI KWA BALOZI WA NYUMBA KUMI, AMBAYE MARA BAADA YA KUTHIBITISHA KUTOJIWEZA KWA MHUSIKA ATAUTAARIFU UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA JUU YA UWEPO WA MTU WA HITAJI HILO NA WAO WATAANDAA UTARATIBU WA KUFANIKISHA MTU HUYO KUJAZIWA FOMU NYUMBANI.

Hawakusema uripoti polisi wala mahakamani, wamesema kwa BALOZI WA NYUMBA KUMI. Mamlaka inatambua huyo ndio mtu wa karibu zaidi na wewe kuliko DIWANI na MKUU WA WILAYA. Na ndio maana wamelipwa posho na wamesaini kwenye rejesta ya wakaazi kuwadhamini watu wa nyumba zao.

Kama bado unaamini wajumbe hawatambuliki, niambie kwa nini Serikali inawatumia kwenye mazoezi yao?
 
Last edited by a moderator:
Na mie nisiye na chama naruhusiwa kugombea ubalozi kama mtu binafsi? Mie sijaona chama kinachonifaa na naona nina mchango.

Wapi ulitaka kugombea ubalozi ukaulizwa chama chako? Kumbe hujui sasa unabisha nini?

Huna hata hakika na unachoandika.

Nafikiri yupo sahihi kusema makisio, sidhani kama unaweza kusema exact number of people wakati wanahama, wanahamia na wanazaliwa na kufa. Tumia akili yako nyingi basi

Kama huna system hata hao wajumbe hawawezi kuwatambua watu wao, sema jingine.
Kukosekana kwa system hakujustify juhudi zisitumike

Kwamba serikali inawategemea halisemi lolote kuhusu umuhimu au uhalaliwao kama walivyo sasa.
Nafikiri una tatizo kichwani. Kwani wapi serikali imesema wajumbe si halali. Au huyu Tiba ndio serikali? Kama haiwatambui, mbona imewalipa posho na kwenye sensa watahusika pia, wa wapi wewe?
Kwa hiyo process za bank ndiyo gold standard siyo?
Hapana, Gold Standard ni haya mawazo yako kuwa mtu anaweza akakukopesha fedha ilhali hajui pa kukupata

Pale Manzese kabla hujataka kupanda juu huko kwenye kuongelea ustaarabu wa civic duty na citizenship pasafisheni kwanza, mpate kukaa kwa mpangilio kwanza, kabla ya kujitia mna verify address wakati watu wanakaa katika mabanda na vyumba vya kupanga wanahama kila asubuhi. And that goes for all the rest of the Dar slums.
Kumbe unajua watu wanahama kila asubuhi, lkn bado ukataka upewe exact figure ya watu wa manzese.

To the contrary. Ng'ombe hajui kuuliza mamlaka, ukimtandika vizuri tu anafyata mkia.Wewe ushatandikwa sana hata kuiuliza mamlaka ya serikali huwezi. Serikali ikitaka u verify physical address unakubali tu hata kama unakaa kwenye kiota kilicho juu ya genge la nyanya Manzese huko.
Siungi mkono ulivyoitwa ng'ombe, lkn naweza kuona similarities za ubongo baina yenu. Ng'ombe ndio hajui kwa nini uzio umewekwa japo anauona. Kutotambua kwa nini wajumbe wapo na bado ukachallenge uwepo wao nia akili za ng'ombe

Wanaruhusu tusio na vyama kugombea?
The answer is yes. Sasa ulikuwa unapiga kelele za nini ikiwa hata namna wajumbe wanavyopatikana hujui. Hawa wajumbe wapo wa CUF (wakazi wa buguruni mashahidi zangu, wapo wa CDM, Kimara pia itanishuhudia kwa hili na wapo wasio na vyama kama Mjumbe Matokeo Logoro wa Makoka. Sasa juu ya nini kuchonga mdomo kwa usilolijua?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usipende kukurupuka na theories zako na kusema huo ndio msimamo wa serikali. Mimi ni karani wa NIDA katika hilo zoezi linalozungumziwa hapa, na nakuhakikishia kuwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI WANATAMBULIWA NA SERIKALI KUU kama sehemu ya serikali ya mitaa.

Wajumbe wa nyumba kumi si lazima watoke CCM. Ni ule uzito tu wa mwitikio kutoka kwa watu wa vyama vingine kuchukua nafasi hizi ndio unasababisha ionekane kuwa hawa ni wajumbe wa CCM badala ya wajumbe wa nyumba kumi.

Yapo maeneo mengi tu ambapo wajumbe wa nyumba kumi wanatoka vyama vya upinzani, sasa mimi sioni shida ilipo ilhali hawa ni muhimu zaidi ktk suala la utambuzi. Nimejitahidi kueleza labda niongezee tu kwa mifano ili ndugu wengine mpate kuelewa.

Serikali kuu inatambua uwepo wa wajumbe wa nyumba kumi na inawatumia kufanikisha operesheni zake nyingi tu, mwenye akili na aelewe na mwenye kutaka kubisha na aendelee kubisha.

1. Askari akitaka kusachi nyumba yako analazimika kumtaarifu mjumbe wa nyumba kumi ili awepo na kushuhudia uhalali wa zoezi hilo na usalama wa mtuhumiwa.

2. Askari hawezi kukutia nguvuni mtaani kwako bila kumtaarifu mjumbe wako juu ya sababu ya kukuchukua isipokuwa kama itadhihirika kuwa unaleta hatari iliyo wazi.

3. Mahakama ikitoa SUMMONS ama wito mwingine wowote ule, wito huo utapitia kwa mjumbe wako wa nyumba kumi. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa hawezi kujua wewe bwana Tiba umepanga chumba cha uwani nyumbani kwa nani kule Tandale, lkn balozi wako atajua.

4. Kwenye hili zoezi la Vitambulisho, NIDA inamlipa posho ya Tshs 10,000 mjumbe wa nyumba 10 kuwaongoza makarani kwenye nyumba zake na kuwasaidia kwa watu watakaogomea kutoa ushirikiano. Hii inadhihirisha serikali inawatambua wajumbe

5. Tarehe 26, tuna zoezi zito la Sensa, kumbukumbu yangu ya Sensa ya mwaka 2002, wajumbe wa nyumba kumi walituongoza kwenye nyumba zao. Hapa nitawapa ufafanuzi kidogo:
-Waweza kumuuliza mtu juu ya mume au mke wake ilhali amemzika juzi tu wewe karani hujui nadhaniutaishia kushangaa mama unayemhoji analia nini, lkn mjumbe ana nafasi ya kukutahadharisha
-Si rahisi mwenyekiti wa serikali ya mtaa kujua kama nyumba fulani ina wapangaji au ni kaya moja tu. Lkn mjumbe ana nafasi ya kuwa na taarifa zaidi.
-Wapo watu wanaficha taarifa za watu wenye ulemavu kwenye kaya zao, lkn mjumbe anaweza kujua taarifa hizi kwani anaishi nao hapo mtaani

Mimi siamini kama serikali haitambui wajumbe wa nyumba kumi. Ni sisi wananchi ndio tunadharau wajumbe kwa kutojua umuhimu wa ngazi yao katika utambuzi.

Kwenye daftari la WAKAZI lililoratibiwa na NIDA, kila individual alipaswa kudhaminiwa na watu wawili ili kuthibitisha ukaazi wake ktk mtaa. Wa kwanza ni MJUMBE na wa pili ni aidha MKUU wA KWAYA (kwa wenye makazi binafsi) au MWENYE NUMBA (kwa wanaoishi kwenye nyumba za kupanga), sasa ndugu zangu wajuaji hebu nielezeni, hivi Mwenyekiti wa serikali ya mtaa angewezaje kuwatambua watu wote wa mtaa wake?

Ndio wajuaji nyinyi nyinyi kesho mtasema kuna Msomali mtaani kwetu haeleweki anaishije lkn mwenyekiti yupo tu bila kujali kuna watu 18,303 katika Mtaa wa Mwongozo uliopo kata ya Makuburi. Yaani kwa akili zenu na mifano na manung'uniko, mnataraji mwenyekiti na wajumbe wake 9 wawajue watu woote hawa 18,000!

Tusipende kuwa wajuaji wajinga. NIDA imetangaza hivi kwenye vyombo vya habari: Ikiwa una mgonjwa, mlemavu au mzee katika kaya yako, RIPOTI KWA BALOZI WA NYUMBA KUMI, AMBAYE MARA BAADA YA KUTHIBITISHA KUTOJIWEZA KWA MHUSIKA ATAUTAARIFU UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA JUU YA UWEPO WA MTU WA HITAJI HILO NA WAO WATAANDAA UTARATIBU WA KUFANIKISHA MTU HUYO KUJAZIWA FOMU NYUMBANI.

Hawakusema uripoti polisi wala mahakamani, wamesema kwa BALOZI WA NYUMBA KUMI. Mamlaka inatambua huyo ndio mtu wa karibu zaidi na wewe kuliko DIWANI na MKUU WA WILAYA. Na ndio maana wamelipwa posho na wamesaini kwenye rejesta ya wakaazi kuwadhamini watu wa nyumba zao.

Kama bado unaamini wajumbe hawatambuliki, niambie kwa nini Serikali inawatumia kwenye mazoezi yao?

Mkuu nashukuru kwa kututoa tongotongo kwamba NIDA inawatambua mabalozi wa nyumba kumi kama sehemu ya watendaji wa serikali. Ninaweza nisiwe na tatizo la kuulizwa barua kutoka kwa balozi kama ulivyosema sehemu kama buguruni kuna mabalozi kutoka CUF na Kimara kuna mabalozi kutoka Chadema, lakini huyu dada alisema anataka barua kutoka kwa balozi wa CCM. Na hapa ndipo tatizo langu lilipo.

Nakushauri usijaribu kutumia nguvu nyingi kutetea mapungufu ya NIDA katika kuendesha ili zoezi. Ni kwa nini si kila kituo cha kuandikisha wanauliza hizo barua za balozi? Kwa nini kunakuwa na double standards wakati vituo vyote vinafanya kazi kwa niaba ya NIDA hiyo hiyo?

Do not be fool to that extent!!!!! Na kwa nini unafikiri wenyeviti wa serikali za mtaa hawawajui wakazi wa maeneo yao? Ni lini serikali iliitisha uchaguzi wa mabalozi wa nyumba kumi kutoka na kumbukumbu zako? Kumbuka hapa unawasiliana na watu wazima na si sahihi kuleta hoja dhaifu hapa!!!!

Tiba
 
Wacha mawazo ya ku support a totalitalian structure. Mjumbe wa nyumba kumi ni style ya wakomunisti ya watu ku keep tabs kwa wananchi wake. Nani ana print subversive material, nani ni "enemy of the state" and some bull like that.

Na kama mjumbe wa nyumba kumi ni muhimu hivyo kwa nini asiwe neutral asiye na chama? Na CHADEMA nao wakisema wana mjumbe wao wa nyumba kumi akamtambua mtu ambaye mjumbe wa CCM hamtambui hapo itakuwaje?

Habari ya mjumbe wa nyumba kumi ilikuwa na mshiko enzi za chama kushika hatamu, ukitaka daftari la kusainiwa kupata unga wa muhogo kilo mbili kwa wiki za ugawaji shurti upitishwe na mjumbe wa nyumba kumi etc.

Sasa hivi katika mfumo wa vyama vingi, huwezi kulazimisha mtu wa CHADEMA aende kwa mjumbe wa CCM.

Ni sawasawa na kulazimisha muislamu atambulishwe na mchungaji wa kanisa la karibu.Utamkosea heshima muislamu huyu na huenda hata salamu zikagongana, muislam anasema "Wasalaam Aleikum" Mchungaji anasema "Bwana asifiwe".

Mkuu nakushukuru kwa mchango wako. Nashangaa ni kwanini huyu jamaa anajaribu kutumia nguvu nyingi kutetea makosa ya NIDA hapa. Na kwa nini sehemu /vituo vingine hawaulizi hizo barua za balozi wakati kwingine wanauliza? Sisi watanzania halisi tutaishia kutoandkishwa lakini wasomali na waethiopia ndio watakuwa wa kwanza kupata vyeti kwa kutoa rushwa kwa hao mabalozi feki wa CCM. Na kama hilo ni agizo la NIDA kwa nini hao mabalozi wanadai shs. 2,000 ili kukuandikia hiyo barua? Je NIDA inawalipa/imewaajiri hao mabalozi?

Tiba
 
hebu tujadili suala la kudaiwa shs 2000 kwa ajili ya kujiandikisha, ni halali, tatizo hili nimelisikia sana.
 
Hamna vyeti wala nini hizi ni siasa za chama cha magamba!!
 
Duh! Ama kweli Kamanda kazi ipo!
Na bila shaka hapa A town ndiyo kiboko!

Duh! Kama ndio hivyo, kuna hatari ya mimi kukosa hicho kitambulisho. Kuna balozi wa ccm hapa mtaani hatuelewani wala hatuongei tangu alipokuja kwangu asubuhi eti anakusanya michango ya ujenzi wa shule za kata! Nilimtimua na kumwambia aende akachukue tra maana wananikata kodi kila mwezi kwajili ya huduma za jamii ikiwemo elimu! Ananichukia na hata nikimsalimia haitiki. Sasa kama ni lazima nikafuate barua kwake, basi kazi ninayo!
 
Wapi ulitaka kugombea ubalozi ukaulizwa chama chako? Kumbe hujui sasa unabisha nini?

Nafikiri yupo sahihi kusema makisio, sidhani kama unaweza kusema exact number of people wakati wanahama, wanahamia na wanazaliwa na kufa. Tumia akili yako nyingi basi

Kukosekana kwa system hakujustify juhudi zisitumike

Nafikiri una tatizo kichwani. Kwani wapi serikali imesema wajumbe si halali. Au huyu Tiba ndio serikali? Kama haiwatambui, mbona imewalipa posho na kwenye sensa watahusika pia, wa wapi wewe?

Hapana, Gold Standard ni haya mawazo yako kuwa mtu anaweza akakukopesha fedha ilhali hajui pa kukupata

Kumbe unajua watu wanahama kila asubuhi, lkn bado ukataka upewe exact figure ya watu wa manzese.

Siungi mkono ulivyoitwa ng'ombe, lkn naweza kuona similarities za ubongo baina yenu. Ng'ombe ndio hajui kwa nini uzio umewekwa japo anauona. Kutotambua kwa nini wajumbe wapo na bado ukachallenge uwepo wao nia akili za ng'ombe

The answer is yes. Sasa ulikuwa unapiga kelele za nini ikiwa hata namna wajumbe wanavyopatikana hujui. Hawa wajumbe wapo wa CUF (wakazi wa buguruni mashahidi zangu, wapo wa CDM, Kimara pia itanishuhudia kwa hili na wapo wasio na vyama kama Mjumbe Matokeo Logoro wa Makoka. Sasa juu ya nini kuchonga mdomo kwa usilolijua?

Narudia,

Idea nzima ya mjumbe wa nyumba kumi ni kurudisha watu katika ukomunisti na kuwafanya kama watoto wa shule walio chini ya monitor na prefect.

Sasa mie kama nina beef na mjumbe wangu wa nyumba kumi tumeingiliana katika mitkas ananiwekea ngumu inakuwaje hapo?

Hizi ni habari za serikali ku snoop kwa raia wake zishapitwa na wakati.

Wewe kama raia wa Tanzania peleka documents zihakikiwe, zikipita unapewa kitambulisho cha uraia.

Kuna vichochoro kibao havina hata mpango na balozi wa nyumba ishirini, seuze kumi. Watu hawana hata serikali za mitaa, nini balozi wa nyumba kumi.

Na hao mtawafanyaje?

Ukiritimba kushinda Vogon ombudsmen.
 
............ tunapashwa kwenda kujiandikisha kwa kuonyesha kitu ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba mimi ni raia. ...........Tiba

neno sahihi ni "tunapaswa"

My apology, tayari nimerekebisha hiyo tarehe. Inapashwa isomeke 31 July 2012.

Tiba

neno sahihi ni "Inapaswa"

.........Hili serikali haipashwi kukaa na kulifumbia macho hata kidogo.

Tiba

neno sahihi ni "haipaswi"

Otherwise mjadala ni mzuri.......kuna elimu nzuri...i.e..kuhusu utendaji wa serikali yetu.....na hii itatusaidia kwenye kutoa maoni juu ya Katiba yetu..... ya kwamba tunahitaji mfumo gani/upi kwenye uandikishaji wa raia............
 
Ah, hili zoezi kila kukicha yanazuka madudu tu, sijui hata kwa nini waliongeza muda wa kujiandikisha. tungekuwa na topic ingine masikioni sasa hivi... mi ya Malawi inanchanganya kweli na huu ujana tulio nao halafu jobless, si unajua tutakuwa tunakamatwa tu tunapelekwa kwenye mapambano.... MUNGU atulinde kwa kweli lol...!!!
 
Mkuu Tiba, ni rahisi kujifanya mjinga kuliko kuniita mjinga na ikawa. Hebu soma wewe mwenyewe ni nini umeandika hapa

Nilifika pale kituoni kwenye mida ya saa kumi jioni na kupanga foleni kwa karibu dakika 45 kabla zamu yangu ya kuandikishwa haijafika. Binti aliyekuwa anaandikisha pale ana umri kama wa miaka 22 hivi. Nilipofika akaniuliza barua ya balozi iko wapi? Nikamuuliza balozi yupi huyo? Akaniambia balozi wako wa nyumba kumi. Nikamuuliza balozi wa chama gani? Akaniambia balozi wa CCM. Nikamuuliza balozi wa CCM anaingilianaje na zoezi la watu kuandikishwa uraia?

Wewe mwenyewe unakiri kuwa alikuuliza kuwa barua ya balozi wa nyumba kumi. Kwa akili zako zilizoathiriwa na siasa wewe ukauliza, 'BALOZI WA CHAMA GANI?' Na yeye kwa kukusaidia kuelewa akakujibu kwa jina lile la mazoea 'balozi wa CCM'

Nachokiona hapa ni udhaifu wako binafsi kuelewa na hata haya unayobisha ni ujinga tu kutopenda kukubali kuwa ulikosea.

Kwa jinsi ulivyo pathetic and fool, umejifanya kukubali kuwa NIDA wanawatambua wajumbe. Lkn ukiurejea mfano wangu, nimewaweka hata polisi. Nimekueleza kuwa hata mahakama ikikupa summons basi maelekezo yake yatakuwa kuwa uipitishie kwa mjumbe wa nyumba kumi.

Ngoja niirejee main post nikuoneshe kwa nini naamini wewe ni mjinga.
 
Last edited by a moderator:
Narudia,

Idea nzima ya mjumbe wa nyumba kumi ni kurudisha watu katika ukomunisti na kuwafanya kama watoto wa shule walio chini ya monitor na prefect.

Sasa mie kama nina beef na mjumbe wangu wa nyumba kumi tumeingiliana katika mitkas ananiwekea ngumu inakuwaje hapo?

Hizi ni habari za serikali ku snoop kwa raia wake zishapitwa na wakati.

Wewe kama raia wa Tanzania peleka documents zihakikiwe, zikipita unapewa kitambulisho cha uraia.

Kuna vichochoro kibao havina hata mpango na balozi wa nyumba ishirini, seuze kumi. Watu hawana hata serikali za mitaa, nini balozi wa nyumba kumi.

Na hao mtawafanyaje?

Ukiritimba kushinda Vogon ombudsmen.

Pathetic comments!

Decentralization of power ndio unaita ukomunisti? Kwa hiyo wewe ulitakaje, tuwe na central government ifanye kila kitu?

Kutokuwepo kwa wajumbe na serikali za mitaa baadhi ya maeneo ni udhaifu wa kiutendaji na si justification ya kutowatumia sehemu walipo. Mimi sioni tatizo zaidi ya elimu duni mliyonayo.

Hivi mkienda benki mkaambiwa mlete barua ya serikali ya mtaa, huwa mnajibu kwa kuuliza mwenyekiti wa chama gani?

Shida yenu ni utoto na ndio maana naona introduction ya maneno ya kipuuzi kama 'beef' na mjumbe n.k. Kwani ukiwa na beef na mwenyekiti wako huwa inakuwaje?

Serikali yoyote makini huwachunguza raia wake na hii ni kwa usalama wao wenyewe. Kama mtu akijipenyeza na kutuhujumu, naamini utakuwa wa kwanza kusema ooh, wenzetu Israel mgeni akiingia tu katika mji wamesham-spot. Lkn kwa kuwa mnaishi kama wanyama msiopenda kujua utaratibu, mnadhani hiyo namna watu wengine wataishi pia, kwamba unafanya unavyotaka na hamna wa kumuongoza mwenzie.

Maisha sio tamthilia mkuu, theories za kwenye vitabu angalia namna unavyoziweka katika utendaji.
 
Inasikitisha kuona Watanzania wagume kuelewa ni wale wanaojisifu kuwa wamesoma. PASSPORT, DEGREE na sijui nini kingine ulichosema havina nafasi katika kukutambulisha wewe kama individual unaishi mtaa gani. Kwa faida yako na wasiojua wengine nitatumia muda wangu kukueleza/kuwaeleza nini nia ya NIDA kufanya zoezi, jinsi zoezi lilivyoenda na malengo ya mwisho.

Kabla ya kujaza fomu za maombi ya KITAMBULISHO, NIDA kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa, iliandaa zoezi la utambuzi wa kaya na makazi kwa kila mtaa. Makarani wa NIDA wakiambatana na WAJUMBE WA NYUMBA KUMI walipita nyumba hadi nyumba kuwasajili wakazi kwenye DAFTARI LA WAKAZI LA MTAA. (Wajumbe wa Nyumba 10 na sio wa CCM) Nikukumbushe kuwa, wengi wa mnaojifanya mmesoma (ilhali vichwani hamna kitu) mlipuuzia zoezi hili na kuwapa wakati mgumu makarani kwa kutotoa ushirikiano kwenu. Muda uliopangwa uliisha na NIDA iliongeza siku 7 za ziada, na bado wengine mligoma kusajiliwa.

Zoezi la usajili wa kaya na wakazi lilipoisha, likaanza zoezi la ujazaji fomu. Hapa sasa na the so called wasomi mkajitokeza. Tatizo likaja kuwa, ili upate uhalali wa kujaza fomu ya maombi ya kitambulisho, inakupasa uwe umeshaorodheshwa katika daftari la mtaa. Sasa lile si daftari tu kama la rambi rambi kwamba kila anayepita na buku yake anaandika, la hasha. ILIPASA UTHIBITIKE haswa ya kwamba u-mkaazi wa eneo husika. Sasa nani anakutambua kama mkaazi, jibu linakuja MJUMBE WA NYUMBA 10.

Kumbuka kuwa, wakati wa uandikishaji wa mitaani (majumbani) mjumbe alikuwa na hao makarani kwa hiyo wote walioorodheshwa wakati huo, walidhaminiwa na mjumbe. Sasa iweje wewe leo hii uje na vyeti vyako vya shule vikutambulishe? Hivi umesoma nini ikiwa unashindwa kuelewa kuwa cheti chako cha chuo hakiwezi kueleza kama unaishi Keko au Mbagala?

Bwana Tiba, serikali ina ngazi mbali mbali za utendaji. Ngazi ya chini kabisa ni mjumbe wa nyumba 10. Ni ujinga na ni ujuha kudharau mjumbe wako wa nyumba kumi na wala kutomjua kwako hakudhihirishi usomi bali upumbavu. Hivi serikali hiyo hiyo iliyokusomesha ikikuhitaji wewe kwa maoni yako unadhani itamtumia nani kukufikia, ALIYEKUANDIKIA HAYO MAVYETI YAKO AU MJUMBE WA NYUMBA KUMI AMBAYE UPO NAYE MTAANI?

Swala la wajumbe kuwa wa nyumba kumi au wa CCM hiyo ni tafsiri tu iliyoletwa na mazoea ya wakati ule wa chama kimoja. Hapa ninapoishi, mjumbe wetu ni wa CUF na mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni Wilbald Mlamba wa CHADEMA. Sisi tunamtambua balozi wetu kama wa nyumba kumi na sio kwa jina la chama chake.

Najua kwa mentellity ya 'KIUSOMI' hautapenda kunielewa lkn ni kwa faida yako. Wenzio waliokuwa nyumbani mjumbe alikuwapo kuwatambua wakaingizwa kwenye daftari, wewe umekuwa nani utambulishwe na vyeti? Hivi ukinionesha passport yako hiyo itanithibitishiaje kuwa unakaa mtaa husika na hukai mtaa mwingine?

Wapendwa, passport yaweza kukutambulisha umetokea nchi gani na sio mtaa gani au ni nini kigumu kuelewa hapo? Hivi leo nikikupa cheti changu cha chuo kikuu unaweza kukisoma na kuniambia ninakaa nyumba namba ngapi?

Kama humjui mjumbe wako wa nyumba kumi hiyo ni dalili hushiriki hata katika shughuli za maendeleo na kijamii mtaani. Hujui cha kukarabati barabara wala harambee ya kufanya iusafi wa mazingira, na nyie ndio wasomi njaa mnaojivunia vyeti bila kuwa na ufahamu hata mambo madogo.

Adha umeitaka mwenyewe kwa kutoandikwa nyumbani kwako. Nenda kwa mjumbe akuandikie barua ili huyo karani akutambue kuwa wewe kweli ni makazi wa eneo hilo ndio sasa atakuandika kwenye daftari na utaruhusiwa kujaza fomu. Vyeti utavitumia kuomba kazi na kujisifia kwa wajukuu zako kuwa ulimaliza madarasa, na passport utaitumia kujitambulisha utapokuwa nje ya mipaka ya Tanzania.

Halafu ni ADHA ndugu msomi na sio HADHA. Siipendi CCM lkn sio sababu ya kunifanya niwe mjinga kwa kutomtambua mjumbe wa nyumba 10.

Las Mas Bobos

We mtu ni shule halisi!waache hao watu wa kudisplay mavyeti wahangaike!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tiba, ni rahisi kujifanya mjinga kuliko kuniita mjinga na ikawa. Hebu soma wewe mwenyewe ni nini umeandika hapa

Wewe mwenyewe unakiri kuwa alikuuliza kuwa barua ya balozi wa nyumba kumi. Kwa akili zako zilizoathiriwa na siasa wewe ukauliza, 'BALOZI WA CHAMA GANI?' Na yeye kwa kukusaidia kuelewa akakujibu kwa jina lile la mazoea 'balozi wa CCM'

Nachokiona hapa ni udhaifu wako binafsi kuelewa na hata haya unayobisha ni ujinga tu kutopenda kukubali kuwa ulikosea.

Kwa jinsi ulivyo pathetic and fool, umejifanya kukubali kuwa NIDA wanawatambua wajumbe. Lkn ukiurejea mfano wangu, nimewaweka hata polisi. Nimekueleza kuwa hata mahakama ikikupa summons basi maelekezo yake yatakuwa kuwa uipitishie kwa mjumbe wa nyumba kumi.

Ngoja niirejee main post nikuoneshe kwa nini naamini wewe ni mjinga.

Hii itakuwa ni mara ya mwisho kukijibizana na wewe!!! Hivi nani mjinga kati yangu na wewe sasa? Unasema ilikuwa sahihi kwangu mimi kuulizwa barua ya balozi wa CCM? Kwa nini kwenye jibu la swali langu huyu binti akusema balozi wa chama chochote aliyeko kwenye eneo langu? Ili kuzuia nisifungiwe hapa JF (sijwahi kupewa ban tangia nijiunge hapa) lakini naona wewe unataka kusababisha nifungiwe kwani unaonekana una kichwa cha senene kwa kutetea ujinga. Na mbona hutaki kuzungumzia suala la watu kudaiwa watoe shs. 2,000 na mabalozi wa CCM ili kuandikiwa hizo barua za utambulisho? Na je hauoni kwamba kwao mabalozi wa CCM wabachojali ni hizo shs. 2,000 wanazopewa na wala sio uraia wa mtu!!!

Pumbafu kabisa!!!!

Tiba
 
Wana Jamvi,
................................................

Tiba

Juzi tarehe 31 July 2012 niliamua niwe mmojawapo wa raia wema kwa kuitikia mwito wa kwenda kujiandikisha.

Kujiandikisha si suala la uraia wema, ni katika kupata haki yako. Ni kwa faida yako na kamwe usifikiri unaifanyia favor serikali

Kwa yanayotangazwa redioni na kwenye magazeti, tunapashwa kwenda kujiandikisha kwa kuonyesha kitu ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba mimi ni raia

Kwa hiyo ukachukua vyeti vyako vya chuo vikathibitishe kuwa wewe ni raia? Vipi kama ungekuwa umesoma University of Colorado?

Huyu jamaa anajulikana kwa kupokea rushwa na ofisi yake haiwezi kukupa huduma yoyote bila kutoa pesa

Hili sasa ndio lilikuwa suala la kuhoji na kutafakari. Je wanapaswa kulipwa na wanaopokea huduma zao au serikali?
Nilipofika akaniuliza barua ya balozi iko wapi?
She was right. Yeye hakujui na hajui kama kweli unakaa mtaa ule au lah. Sharti lake la uandishi ni kuwaandika wakaazi wa mtaa husika. Uthibitisho huu anao mjumbe wako wa nyumba kumi, kwamba kweli unakaa kati ya nyumba zake.

Nikamuuliza balozi yupi huyo? Akaniambia balozi wako wa nyumba kumi.

Nafikiri mpk hapa ulikuwa umeshamuelewa, lkn ukaamua kuleta ujuaji wako na kujaribu kumchanganya. Anayezungumziwa hapa ni BALOZI WA NYUMBA KUMI. Na haijalishi ana itikadi gani kisiasa.

Nikamuuliza balozi wa chama gani?

Hili lilikuwa swali la kipuuzi. Hivi ukienda benki ukaambiwa ulete barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa, unamuuliza afisa mikopo,
'mwenyekiti wa chama gani?'

Akaniambia balozi wa CCM.

Nafikiri alijibu hivi akidhania utamwelewa vema, kwani sehemu nyingi watu huwaita wajumbe wa nyumba kumi kwa jina la wajumbe wa CCM.

Nikamuuliza balozi wa CCM anaingilianaje na zoezi la watu kuandikishwa uraia?

Hapa ndio panadhihirisha jinsi unavyokurupuka (na naamini si wewe tu, wengi hamfahamu)

NB: Zoezi linaloendelea linahusu VITAMBULISHO VYA TAIFA na sio URAIA. Watu wote wanaoishi Tanzania watapatiwa vitambulisho regardless ya uraia wao. Watanzania, Wageni wakaazi na wakimbizi wote watapatiwa utambuzi. Na hapa narejea ujinga wako wa kwanza kwamba ulichukua vyeti vikakutambulishe kuwa wewe ni raia, si hivyo. Lengo la NIDA ni kufahamu wewe ni nani, upo wapi, unafanya nini na unamiliki nini. Viambatanisho unavyopeleka vinafanya kazi hiyo na sio kuthibitisha uraia wako. Nikikutana na wewe Buguruni sokoni nikakuonesha cheti changu cha form four, utanitambua kuwa mimi ni RAIA?

Je ni kweli barua ya balozi wa CCM ni mojawapo ya masharti ya mtu kuandikishwa uraia?

Hakuna masharti bali ni utaratibu. Yapaswa utambulike na jamii inayokuzunguka. Mjumbe (wa nyumba kumi) ndio mwakilishi wa ngazi ya chini kiserikali. Ndio maana hata leo ukinunua kiwanja au shamba na mjumbe huyu akagonga muhuri na kusaini basi hiyo ni hati ya mauzo inayotambulika hata na mahakama zetu. Nasisitiza ni ujinga kudharau mamlaka hii iliyo karibu nawe.

Mkuu Tiba, mtaa wenu wa Ubungo Maziwa una wastani wa wakaazi 10,150. Kuna nyumba za kupanga takribani 195 (zinazofahamika) ambazo watu wanahama na kuhamia. Je kuna utaratibu mwenyekiti wenu wa serikali ya mtaa anaweza kuwatambua bila kupitia wajumbe wa nyumba kumi?

Si kila ujinga ni wa kuukumbatia na kujifanya wewe ndio unajua zaidi. Hakuna mtu anayekuandikisha uraia hapa. Ikiwa wewe ni Mtanzania basi huna haja ya kuandikishwa na hata usipoandikishwa bado utabakia kuwa ni raia tu. Linaloendelea hapa ni zoezi la USAJILI na UTAMBUZI.

KUTAMBUANA ndio zoezi lenyewe, na kama una akili angalau kidogo, utakubaliana na mimi kuwa mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa hawezi kuwatambua nyinyi wakaazi wote 10,150 hata awe na ubongo wa kisomi kama wako.

Kinachokusumbueni ni dharau. Acha niwatahadharishe kwamba, hata kama mahakama ikiendesha session chini ya mti, atakachoamua hakimu mbele ya picha ya Rais, kitakuweka gerezani kwa muda huo atakaosema. Mjumbe hata akiwa namna gani, ndio mtambuzi wako na sio diwani wala mkuu wa wilaya. Ndio maana ana muhuri ambao akigonga kwenye barua yako, mwenyekiti wa serikali ya mtaa anakupokea. Na kama unaona haya ni matani na ujinga mnaojifunza shuleni, jaribu kuchonga muhuri wa mjumbe na wewe uwe unagonga halafu serikali ikubaini.
 
Last edited by a moderator:
Hii itakuwa ni mara ya mwisho kukijibizana na wewe!!! Hivi nani mjinga kati yangu na wewe sasa? Unasema ilikuwa sahihi kwangu mimi kuulizwa barua ya balozi wa CCM? Kwa nini kwenye jibu la swali langu huyu binti akusema balozi wa chama chochote aliyeko kwenye eneo langu? Ili kuzuia nisifungiwe hapa JF (sijwahi kupewa ban tangia nijiunge hapa) lakini naona wewe unataka kusababisha nifungiwe kwani unaonekana una kichwa cha senene kwa kutetea ujinga. Na mbona hutaki kuzungumzia suala la watu kudaiwa watoe shs. 2,000 na mabalozi wa CCM ili kuandikiwa hizo barua za utambulisho? Na je hauoni kwamba kwao mabalozi wa CCM wabachojali ni hizo shs. 2,000 wanazopewa na wala sio uraia wa mtu!!!

Pumbafu kabisa!!!!

Tiba

Am not arguing with you. I am telling you.

Mimi sizungumzii udhaifu wa mjumbe wako anayechukua 2000 bila kujali uraia wako bali nakuelewesha kuhusu maudhui ya zoezi. Kukiukwa kwake hakumaanishi malengo hayakuwepo. Shida yako huna unachojua zaidi ya kukurupuka.

Majibu ya dada yanalingana na uelewa wake na ninayokupa mimi ni kwa uelewa wangu. Sasa kazi ni kwako kuona kama ninachoongea kinaleta sense au lah. Kuhusu kuniita pumbavu mods hawana sababu ya kukufungia ikiwa watasoma Mithali 9:7-9.

Kama wewe unayeamini kuwa cheti chako cha form four kinaweza kunifahamisha mimi uraia wako unaweza kuniita mimi mpumbavu kwa kuwa wewe unaamini cheti kingeweza zaidi ya mjumbe, mimi sioni tatizo, MODS wakuache tu kwani hayo ni maoni yako.

Na kwa kuwa kazi yangu ni kuelimisha acha nikuongezee hili jambo moja ambalo naona pia hulijui. Hakuna sehemu ambapo kuna wajumbe wawili wa nyumba kumi kiasi dada-karani akwambie mjumbe wa chama chochote. Kama eneo lako mjumbe wake wa nyumba kumi ni mwanachama wa TLP basi hakutakuwa na mwingine. Hapa kwetu mjumbe wetu Babu Muha ni CUF, mimi ni CHADEMA na Mwenyekiti wetu Wilbroad Mlamba ni CHADEMA lkn wajumbe wa kamati za mtaa wote ni CCM.

Endelea kununa na mimi nitaendelea kukuelimisha. Haya ninayokupa hutayapata kamwe kwenye magazeti ya udaku unayoyahusudu
 
Msilete harakati katika mambo ya msingi ya kitaifa, system ya mabalozi wa CCM ipo tangu enzi za TANU ndiyo maana ni rahisi kuitumia kuliko hizo articial system za mabalozi wa CUF na CDM. Hata kuna kasoro ndogo ndogo katika zoezi hili tunapaswa kuziaddress pale pale sio kuanza kutoa malalamiko na shutuma kwa Serikali. Mtendaji mmoja au huyo Dada wa NIDA ambaye nina hakika ana ajira ya mkataba hawezi kufanya mambo ya hovyo ukaja hapa JF kuizodoa Serikali.
 
Back
Top Bottom