Kwanza nitangaze wazi kwamba Mimi ni Kiongizi Mwandamizi wa Chama cha wafanyakazi sekta ya Nishati na Madini (Sekta ya Uziduaji) Tanzania, kinaitwa kwa ufupi NUMET.
Pamoja na kwamba hatuhusiki sana na wafanyakazi wa sekta ya umma ambayo inalalamika sana kwasababu za kutoongezwa mishahara, na masilahi mengine, na sisi pia kwenye sekta binafsi wanachama wetu hawako na furaha kama tulivyotarajia au kama walivyotarajia.
Kuna mambo mengi tunafanya, Lakini kwasababu mbalimbali kuna mambo mengi hatujafanya. Lakini angalau kuna juhudi zinafanyika na baadhi ya wanachama wetu wanashiriki moja kwa moja.
Lakini, ukitafuta kiwango cha wafanyakazi nchini kuridhishwa na huduma zitolewazona vyama vya wafanyakazi nchini kwa ujumla wake, ni kidogo sana.
Jukwaa hili lina watu wenye uelewa wa mambo mengi sana. Mnafikiri vyama hivi vinakwama wapi? Maana kuendelea kulalamika tu bila kutoa suluhu inaweza isisaidie sana kujikwamua kwenye mkwamo huu.
Karibuni tujadili.
Nicomedes M Kajungu
Katibu Mkuu
NUMET
MWANZA HQ
T