Nani anayeua Vyama vya Wafanyakazi?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Tangu enzi za Ukoloni vyama vya Wafanyakazi vina na mchango mkubwa kwenye utetezi wa maslahi ya Wafanyakazi.

Dhana ya kwanza ya vyama hivyo ilikua ni kuondoa kero zilizowakumba Wafanyakazi, Mwaka 1922 mjini Tanga kilianzishwa chama cha Wafanyakazi wa umma yaani Tanzania Civil servants Association TCSA chini ya Martin Kayamba ambaye alikua mwenyekiti.

Chama hiki kilihakikisha serikali ya kikoloni inaboresha maslahi ya Wafanyakazi wa umma nchini. Kutamalaki kwa shughuli za chama hiki kikapata uungwaji mkono Tanzania nzima hadi kikavuka mipaka kutetea Wafanyakazi wengine mfano wakulima wa mkonge mashambani na Wengine wengi.

Hali hii ilipelekea chama hiki kuanza kupata msukosuko kutoka Serikalini kwa kuonekana Kama chama Cha kudai Uhuru na sio maslahi ya wafanyakazi Jambo ambalo likapelekea chama kufa na kuundwa vyama vingine ambavyo vilikihusisha moja kwa moja na harakati za ukombozi.

Je TTCSA inatupa somo gani kwenye maendeleo ya vyama vya Wafanyakazi kwa wakati huu?.

Kumekuwa na hoja nyingi kuwa vyama vya Wafanyakazi vimekuwa havina nguvu tena.

Wengine wanasema serikali imeua vyama vya Wafanyakazi huku wengine wakivilaumu vyama vyenyewe kwa kushindwa kujiendesha kwa maslahi jambo ambalo linavipotezea ushawishi kwa wanachama.

Uongozi wa vyama vya Wafanyakazi nchini ni chumvi inayotiririka kwenye kidonda cha mpishi jikoni.
Wengi wao hutanguliza maslahi yao wenyewe katika vyama na kuwaacha wanachama wakiwa hawana msaada wowote.

Matukio ya hivi karibuni ndani ya chama cha waalimu Tanzania, CWT ni ushahidi tosha kuwa vyama vya Wafanyakazi vinajiua vyenyewe kwa kuwa na uongozi usio na uadilifu.

Vyama Kama CWT ambavyo vingeweza kuwa na msaada kwa Wafanyakazi vimegeuka kero kubwa kwa Wafanyakazi kwa kuwakamua mishahara yao pasipo kuwatetea ipasavyo.

Kama Mfanyakazi anakosa kuhawiwa fulana siku ya Wafanyakazi je ataweza kuaikilizwa kero zake? Uongozi Usipo badilika hauwezi kuwatetea ipasavyo na kutatua kero zao.

Kwa upande wa serikali imeshindwa kuweka Mazingira rafiki kwa vyama vya Wafanyakazi ili kuvilinda na kuhakikisha vina kuwa na manufaa kwa watu wake.

Ukivuta picha tukio lililompata Mwenyekiti wa chama Cha madakatari Steven Ulimboka miaka kadhaa iliyopita bàada ya Kutangaza mgomo wa madaktari nchi nzima bado utapata ukakasi kujua nani anaua vyama vya wafanyakazi?.

Vyama vya siasa vimeingilia kazi mahsusi ya vyama vya Wafanyakazi nchini kwa kujivika kilemba cha kuwasemea lakini huwa vinajitokeza tu pale ambapo vina uhitaji wa ufuasi wa watu hao kwa lugha nyepesi vyama vya siasa vipo kwa ajili ya maslahi ya kisiasa sio Kwa ajili ya maslahi ya wafanyakazi moja kwa moja.

Wafanyakazi nao wameingia kwenye mtego kwa kujiingiza kwenye maslahi ya kisiasa na sio maslahi ya kikazi, hivi umewahi kujiuliza kama TLP nchini Tanzania ni chama Cha Wafanyakazi kina mchango gani kwa Wafanyakazi wenyewe?.

Jambo la uhai wa vyama vya wafanyakazi upo mikononi mwa Wafanyakazi wenyewe kuamua ni njia gani waende kisha serikali huweza kuitikia kwa kuangalia nguvu yao. Vyama vya kikomunist vilipata nguvu kwa kuwa na mchango mkubwa kwa wafanyakazi Jambo ambalo likapelekea kukua kwake.

Kuna haja ya kuvinusuru vyama vya Wafanyakazi kwa kuwa na ajenda safi ya Uongozi wake na Sera za serikali katika kuviongoza.
 
Viongozi wa makao makuu ya vyama vya wafanyakazi ndio wanaua vyama vya wafanyakazi, hawa viongozi ni wagombea watarajiwa wa CCM.
 
Back
Top Bottom