Vurugu zisizoisha kitongoji ninachoishi Afrika Kusini

Si uje ufungue duka lako Kariakoo hapo maisha yaendelee kwa amani bila bughudha.
Ataishia kwenye process za kuomba Leseni, tax clearance certificate na business registration, hamu itamuisha hapohapo, TRA na Brela ni kichechefu kifupi.

Ukiona Mtanzania anaendesha biashara halali na analipa kodi muheshimu sana, ujuwe huyo ni nunda.
 
Vita ni fita na vita hafina macho, pambana muraa
Unaweza kupambana vipi na binadamu wasiojuwa thamani ya uhai wa binadamu?

Utaratibu wa South Africa ukiishi miaka mitano mfululizo kihalali una haki ya kuomba Uraia, au ukiowa Msouth Africa una haki hiyo.

Watanzania wanaojitambuwa watumie fursa hizo kupata ID ili wapate passport za Kisouth Africa waondoke hapo.

Passport ya South Africa inaheshimika nchi nyingi za mabeberu wanaingia bila viza na wenyewe hawana utamaduni wa kutafuta maisha nje ya nchi yao, Kwahiyo South Africa passport yao bado iko clean kwenye records za mabeberu.

Chukuweni passport muondoke hapo, ndicho walichofanya wajanja waliojitambuwa kitambo tu.

Ukiwa chini ya miaka 30 unachukuwa working holiday viza ya miaka kadhaa UK bila usumbufu wowote kwa Msouth Africa.

Pale Slough Uingereza Makaburu ni kama Nyumbani kwao wamejazana kibao kwa kutumia fursa hiyo, akirudi South Africa na Pound zake ni tajiri.
 
Kesho yake pakatulia sio wao wala sisi kuonekana kiwanja cha vitaa

PART THREE-MWISHO

Mji ulikuwa kimya sanaa hiyo kesho yake ambayo walisema ni kiwanja cha vita kitajaa damu- hakikia na yeyote mabarabarani, kulisikika milio ya magari tu na hakuna yeyte nje kila mmoja alijifungia kwake

Kesho kutwa yake tena kimya na wiki nzimaa ilikuwa kimyaa

My friend tukajadiliana hapa haina haja ya kuambiwa tufungue maduka yaani tujifungulieni tu kwani tumeshawaweza na hawawezi fanya chochote kilee

Tukafungua- wakaanza choko choko siku hiyo hiyo tukasema hatufungi ila tunawaudumia wateja wetu nje? Ya bagla yaani , wateja hawatoingia mpaka ndani dukani tutawahudumia kama maduka ya bongo, huku huwa wanaingia dukani wanachagua vitu then wanakuja tunawapigia mahesabu alaf wanalipa dzain kama ya vimin market vilee,haikuwa hivyo ikawa tunawahudumia kama bongo vilee

Ila kuna wabishi walikuwa wanawaachia waingie wajichagulie na ilikuwa fursa tena kwa vibaka katika wiki hiyo hiyo

Kuna duka wameingia vibaka na kupola pesa na kumpiga shaba mtoto wa kiarabu/kiethiopia na kumuua ila walikuwa wezi tu sio hao wenye mgomo hatimaye wakakamatwa wakaenda jela- sema inasemekana kesi ya kuua sio kesi Kwa South Africa kwamba walikuwa wawili katika upelelezi akaachiwa mmoja Kwa maana yeye siyo aliyempiga bunduki ila mwenzake amenyea ila wanasema anaweza akakaa miaka miwili tu then akatoka ila waethiopia waneapa akitoka asirudi mitaa hii kwani nayeye watampeleka alipompeleka mwenzake yaani watampiga bomba nayeye, yule mmoja tunasikia tu ametoka ila hayupo mitaa hii itakuwa amehamishwa mji

Na uwezi amini hao watoto waliomuua huyo jamaa walishawahi kuja dukani kwetu wakataka waibe tukawashitukia, tukataka tuwachape tumewakolomea tu tukawaacha maana kujenga vichuki vidogo vidogo sio inshu kabsa, maana hata ukiwakazia kuwapa sigala wakilalamika hawana kitu wanaweza wakaja kukupiga bomba yaani chuki tu mwananga sio maisha kabsa south africa hapafai kabsa yaani tupo tu Kwa ajili tumeshaanzisha maisha

KIKANUKA TENA SERIOUSLY HIYO WALIOSEMA WANAKINUKISHA

tuliambiana tufunge biashara yukafunga, wakakusanyanaa mitaani na kuanza kuchoma mapira wana mapanga na malungu na Safari hii walikuwa wengi sanaa

Sisi kama kawaida tukashituana kuwa vita imerudi tena na uzuri mahojiano ya siku ilee halifika sehemu husika so kulikuwa na asikari maalumu wapo doria

Wakawakamata ma- icon wao kama kumi , kumi na mbili hivi, yaani waliwakamata walee waanzilishi wa vurugu wakawatia ndani lakini tulikuwa tayari kwa vita , yaani tulikuwa tayari kwa chochote

Ila binafs nilishukuru kuona pambano lipo off Kwa leo nilishukuru

Walee wengine wafata mkumbo kuona wenzao wamekamatwa wakakimbia

Tukaambizana kilichoendelea tukatudisha silaha kwenye ala zake

Nna mpaka video ila sitaweza kiwawekea hapa mtandaoni

Vitaa ilisimama hivyoo- wajamaa hawajatoka mpaka leo kesi kila siku inapelekwa mbele wanaenda kama wachochezi wa vurugu

ila ninachokiona ili balaha likirudi tena itakuwa nomaa sanaa yaani watakufa watu yaani hapa nna mpango wa kujichanga kama Mil 10 , nitokomee canada/ popote pazur ila ndio nakichanga

Baada ya hili balaa- kuna baadhi ya wabongo ambao hawakuvunjiwa maduka yao, wameuza biashara zao na kwenda Tanzania kuanza maisha mengine nanasikia wengine waneshapata visa wapo zao canada huko , yaani hapa ndonga linauma nitoke hapa SA nitafute kiwanja kingine- ila ilee kutoka moyonisiogopi chochote kilee sio kuhusu tunavyopondwa watu wa SA wala hayaa maisha ya bastola kila siku sihofii chochote kilee

Ninachohofia kupoteza biashara yangu tu I wish nipate mteja niiuze nitokomee zangu makanada huko

Najifunza vingi sana na ukifikiria nna 29 yaani na naendelea kujifunza

Kuhusu kuuza biashara wasomali na waethiopia hawaogopi chochote ukitaka kuuza wao wananunua tu wao wapo tayari kwa lolote nipo kwenye mafikirio ya kuuza ila ngoja kwanza niangalie upepo


MWISHO

Kuna mengi sijayaweka katika maisha ya kila sikuya South Africa
Nimeshatolewa bunduki mara mbili na kutolewa kisu mara moja ki ukweli ni maisha ya roho mkononi, karibu sanaa SA

ASANTUM- tupo sanaa maisha hayaa ila ikimpendeza M/Mungu atujaalie tutusue twende zetu CANADA HUKO-InshAAllah
Life must go on hao awana tofauti kitabia na black America ngono na wizi chuki kiufupi ni kama ndugu
 
Nitarudi kujibu comments zenu nna jazba sana hapa nikijibu lazima nitapaniki nitawajibu kwa hasira na sitoendelea na hiki kibwanga

PART TWO

usiku kama wa saa saba wazee wa kazi wakaanza kazi yao wakaanza kijisehemu chenye wamalawi wengi full kuwachapa yaani wamewachakaza sanaa usiku ulee na kuwapeleka N2- yaani barabara kubwa kwa maana wapande magari waondoke kwao wengine wamekimbilia kituo cha police unaambiwa police kama hawawaoni raia vilee nomaa ilikuwa, baada ya mda watu tukashituana kwenye group kwamba wazushi wameanza mda huu saa 7 kuganya vurugu Kwa usiku ulee wenye magari ndio waliamka na kupitia baadhi ya watu /raia wageni wenye hasira zao na kuongozana mpaka kituo cha police

Walee wazushi wakawa wanawakimbiza wageni Kwa kuwapiga na magongo usiku huo na walikuwa wanakimbilia kituo cha police basi banah baada ya watu kujaa palee kituo cha police likaanza nomaa, Kwa kuwa police walijifanya kama hawahusiki raia wakigeni waliokuwepo ikabidi wakinukishe na kuungana na walee waliokimbizwa, wamama wakigeni wakaambiwa watulie wanaume wakaanza kazi binafsi usiku huo sijakuwepo mimi nilianza kazi hasubuhi ya kuwabalasa wazushi

Mziki ulikuwa mnene zilipigwa hapo mpaka polisi wakaingilia Kwa kupiga mabomu na mabunduki juu kiufupi wajinga tuliwaweza Kwa usiku ulee wakakimbia kazi ikaanza tena hasubuhi yake

Saa kumi na moja raia tumeshaamshana na kuanza kupanga tunaanzia wapi tulikuwa wengi sanaa, wazimbabwe ni nomaa aisee hawana mzaha, tulikuwepo wazimbabwe, wabongo, wagana, wanaigeria, wamalawi, waethiopia, wasomali na wamozambiki- kilinuka hiyo hasubuhi sisi tuliamka mapema kumbe na wao walishaamka kwa kutufukuza tuondoke

Tuliwaambia kuwa atayeshindwa vitaa yeye ndiye atakayeondoka, wakuu isikieni tu vitaa ni balaa lingine kabsa yaani sio ya kuiomba hata kidogo M/Mungu nijaalie niondokane na balaa hili nikiwa mzima amini

Tunapanga maandalizi mpaka saa moja, saa moja na nusutukatoka na kuwafata walipo, kuna kajisehemu kuna uwanja ndio wanaposimamaga Kwa mikutano yao na kupanga waanzie nyumba ya nani? Tukawakuta hapo sasa bwanah hawakuamini kama tupo tayari Kwa vita Na tulikuwa wengi kinomaa yaani tukiongozwa na wenye bunduki ila walizificha mpaka waone vitaa inakomaa vipi? Tulikuwa na mapanga na magofu stiki na malungu

Haina kuuliza hiyo wao walikuwa takribani kama 100 hivi wengine waliogopa fujo mziki wa jana usiku walijua hawa wapo seriously, sisi tulikuwa wengi sanaa aisee

Tukawavamia na kuanza kuwapa kichapo na fimbo na Malungu tuliongea kuwa tusiwapige mapanga maana bado tuna muendelezo katika hiki kitongoji

Walijitahidi kupambana lakini na wingi wetu tuliwaweza tuliwachakaza sanaaa baadhi yao tuliwavunja miguu na mikono, tuliwapasua pasua yaani kama lisaa Na nusu tunawapiga tu- ndipo yakaja magari ya asikari wa kawaida yaani police tukawagomea na baada ya kupiga mabomu na kuongeza vikosi vingine ndio tukawaacha walikuwa wanalia tu yaani Kwa hicho kichapo

Mda si mda waandishi ww habari wakaja sehemu ya tukio na kuanza kutuhoji

Wapo walioelezea, kuwa serikali haioni kinachoendelea mpaka mnawaachia wanatunyanyasa kama hivi kama hatutakiwi kweli watangaze na watupe utaratibu tuondoke kiharali na mali zetu kwani na sisi tuna kwetu kinachotufanya tugande hapa ni mali zetu tu na familia zetu, kama hamtuhitaji ni mseme tu na mtuandalie mazingira tuondoke kwa amani sio kutesana kama hivi- ilikuwa hivyo

Mchezo haukuishia hapo

Hapo baadhi ya wageni wengine wapo machakani wamejificha maporini huko wapo walihama mji Kwa kukimbia virugu na vurugu ikiisha watarudi kuendelea na maisha yao kama kawaida

Siku hiyo ikaisha tukajipongeza sanaa , huwa tuna shushuhsu kwenye group lao la whatsapp kuwa kinachoendelea atujulishe kama kawa akatuambia nini? Kinaendelea kuwa wamepanga kesho yake wakinukishe kweli na wameapa kuwa hiyo ndio vita ya bunduki kuwa lazima wafe watu

Tukapata habari , wasomali na waethiopia na wagana na wanaigeria katatutoa hofu- wakatuambia kuwa tuna bunduki tutakuja nazo wakasema Bora watu wafe ili heshima iwepo, Na baadhi ya wabongo waliokuwa Na bastora zisizo Na vibali wakasema watakuja nazo na itakuwa poa tu

Na tukasisitizana kuwa hatutakufa sisi tu kuwa sisi tutakufa na wao pia watakufa

To be continue
Battle field
 
Back
Top Bottom