Usiogope kuitwa Kafir! Anayekuita hivyo ni mwanadamu wala si Mungu! Mungu aliyekuumba anajua kuwa wewe si Kafir! Achana na wasiojua wanachokifanya, wanaficha udini mgongoni mwa Muungano! Sijasikia dini ikiunganisha Taifa! Kama ingekuwa hivyo Somalia na nchi nyingine za Kiarabu wasingeendelea kuchinjana!
nime-highlight kabisa kwa wino mwekundu kuonyesha uzito wa ujumbe.Wakati virugu zikiendelea kujitokeza huko Zanzibar ni vizuri Watanzania kutambua na kukumbuka yafuatayo:- 1. Muungano kati ya Tanganyika na visiwa vya Unguja na Pemba ndio ulio pelekea kupatikana kwa nchi ya Tanzania. 2.Mafanikio yanayopatikana kutokana na muungano ni mengi kuliko matatizo. 3. Ni jukumu la kila mtanzania kupigania na kudumisha amani iliyopo. ANGALIZO- Tusiruhusu kikundi au baadhi ya watu kuvunja amani na muungano uliodumu kwa zaidi ya nusu karne.