Chona
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 523
- 360
Nadhani sasa wametupa ishara kwamba kinachotakiwa si kuvunja Muungano tu lakini pia wana mahitaji zaidi ya hilo la muungano. Kwahara haraka ni kwamba hata wakristo wahahitajiki Zanzibar na ndio maana makanisa yao yamechomwa moto. Makinisa ni majengo tu hivyo sidhani kama yenyewe tu bila wale wanao yatumia yanatatizo, tatizo ni watumiaji na ili message iwafikie wahusika basi ilibidi yachomwe moto. Hii inanikumbusha usemi aliowahi kusema baba wa taifa kuwa dhambi ya ubaguzi kwa kawaida haina mwisho. Leo wanasema sisi wanzanzibar wao wabara. Lakini kesho watenda kipengele kingine ambacho tayari wameshakionesha nacho ni wao wakristo sie waislam. Kesho kutwa watasema wao wa answar suna na sie wa shia. Mtondo watasema sie wa unguja wao wa pemba. Mtondogoo watasema sie ni wenye uwezo wao maskini na kuendelea na kuendelea kiasi kwamba utakuta si wamoja tena na nivurugu vurugu tupu. Si semi kuwa lazima waukubali Muungano ila sikuona mantiki ya kuunganisha kudai kukataa muungano na kuchoma makanisa ya wakristo. Wakristo ni wachache sana lakini nguvu yao ni kubwa mno waomaji wa biblia wanajua, ni vile tu ni wavumilivu na ni watu wa kusamehe na kusahau, lakini pia hufundishwa kuwapenda wale wanaowachukia. Kwa mantiki hiyo wasidharauliwe kwa uchache wao. Muungano = Uchomaji wa makanisa. Hili halitakaa likakubalika