Vurugu Zanzibar, makanisa yachomwa moto!

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,182
6,216
Kwa mara ya kwanza kabisa nimekubali kuamini kuwa, tatizo liliopo Zanzibar sio Muungano bali ni dini na wanatumia muungano kama kigezo. Mimi ni muislamu lakini nalipongeza Jeshi kwa kutoa kibano kwa wafanyaji fujo usiku huu huko mjini Zanzibar.

Jumuiya ya UAMSHO itabidi ipigwe marufuku kabisa kwanza inapotosha wananchi ili kufikia malengo yake.

Katika ripoti nilizozipata mpaka hivi sasa ni kuwa wazanzibari ambao obviously ni waislam wenzangu wameenda kuchima moto kanisa moja pale mjini. Kitendo hichi nimekichukia kwa sababu kinaudhalilisha uislam na kufanya uonekane ni dini yenye wafuasi wajinga kabisa.

Katika dini ya uislam tumefundishwa kuheshimu dini za wenzetu, lakini sasa wamevuka mipaka hata mungu wanampinga! Sio jambo la ustaarabu kabisa na kama wamo waislam humi watakaochangia, nawapa LIVE yoyote atakayesapoti kitendo hicho ni mjinga na haijui dini! Katika historia ya mtume saw sijawahi kuona sehemu ambayo mtume alivamia tu wakiristo au mayahudi na kuwachomea moto Nyumba zao za ibada!

MAKANISA YAHESHIMIWA KAMA VILE WEWE MUISLAM UNAVOTAKA MSIKITI UHESHIMIWE! Leo hii lau kama ungeskia msikiti umechomwa moto na wakiristo mungekuwa na hasira sana, basi na hai wakiristo na wao wana hasira ivo ivo! HESHIMA NI KITU CHA BURE!

TATIZO LA WAZANZIBARI NINELIGUNDUA SIO MUUNGANO BALI NI UDINI. Na watu wanaburuzwa tu na iyo UAMSHO, na ndio maana wanafunzi wa zenji wapiga drift ya 360 katika mitihani yao

547304_399447393432296_100001011158863_1105765_1604109665_n.jpg

Kanisa lililochomwa moto

577110_399446403432395_100001011158863_1105757_514010925_n.jpg

Gari la askofu lililochomwa moto
 
Tunashukuru kwa taarifa. Umeweza kujua ni kanisa gani lilichomwa? Najua kuna kanisa kwenye eneo lilikuwa linatumiwa kama soko la watumwa. Ni kanisa la kihistoria. Lakini hata kama litakuwa ni kanisa jingine, ni jambo la kusikitisha maana linasambaratisha jamii na kujenga chuki baina ya watu wa dini hizi mbili. Wote tutaangamia.
 
Hali si nzuri huko Zanzibar, jana usiku kanisa la TAG limechomwa moto eneo la Kariakoo huko Unguja.

Source: Wapo Radio
 
ktk maandiko yametabiriwa haya, Wala msishangae shetani yu kazini. Dini yao inawatuma kutenda hayo ili waingie peponi! Kwa hiyo tusishangae haya! Yatakuja mengi sana maana yalitabiriwa ktk biblia. Yatupasa kumshukuru MUNGU kwa kila jambo.
 
sasa kanisa limewakosea nini Wazanzibar!? Mi nafikiri hiki kitu si cha kufumbia macho hata kidogo, inabidi hatua ichukuliwe, kwa hivyo vitendo vinavyofanywa na wahuni wachache, walianza kuchoma moto mabar, wakachoma moto nyumba za Watanganyika sasa wanapoelekea ni pabaya. Huu uhuni hauwezi kuvumilika hata kidogo. Hatuwezi kuchekea upumbavu wa namna hii.
 
Baada ya kutawanywa jana majira ya saa nne za usiku Wazanzibar na wanaUamsho kwa pamoja wanaodai zanzibar huru wanaendelea na fujo za hapa na pale huku maeneo ya mji mkongwe na viunga vyake kumekua na uchomaji wa matairi ya gari na rapsha,zogo n.k hukui askari wakipiga mabomu,nawaasa wale mnaokwenda kanisa la mkunazini na la minara miwili kuwamakini na ukizingatia kanisa la kariakoo limeshapigwa kiberiti.
 
Leta bia ya baridi hapa nipoze machungu ya kuchomewa kanisa
Inaelekea umefurahi sana,PhD?Agiza wisik kabisa!Sijambo lakufurahisha hata kidogo,Linaleta picha mbaya sana na muelekeo ambao hatima yake...........!
 
Nashawishika kuamini sasa kuwa Kero ya Muungano huko Zanzibar inatumika kama kichaka cha kutekeleza mipango ya kikundi/vikundi vyenye misimamo ya kidini.

Kwa nini kila Vuguvugu la Muungano linapochipua Makanisa huchomwa?
 
Watanganyika na Wazanzibar tumechangamana vya kutosha. Huku Tanganyika Wazanzibar pia wapo lakini si busara wala si haki kulipa kisasi dhidi yao. Nashauri Serikali ilinde raia na mali zao kwa nguvu zote.
 
Tumezidi nasisi kunanini kule znz tunachowang'ang'ania,. Wache waende nafikiri njia ya kuchoma makanisa so nzuri ndugu zangu daini haki kwa njia zingine
 
Mimi nilishasema, Katika dunia kunanguvu mbili zinazo pingana, Mungu wa kweli yupo na Shetani yupo victim ni sisi wanadamu.

Mungu wa kweli alituumba na anatupenda sana, Shetani ni muhalibifu yeye alikosea tangu mwanza kabisa sasa kinachofanyika ni kupotosha watu ili waende nae motoni.

Chakushangaza watu huwa hawafikilii na kujiuliza Je! shetani anatumia mbinuzipi kupata watu maana yeye shetani ni mpinzani wa Mungu yaani ataki mapenzi ya Mungu kwa wanadamu yatimie yeye anapotosha na kudanganya.

Swali la kujiuliza kwanini Waislam hawana shida na wahindu na wapagani n.k lakini wakisikia Ukristo hawawapendi wala hawawataki kabisa nikipi kiko nyuma ya pazia.

Kwanini hawaubiri kuwaambia wapagani waje kwao na kwanini wanapinga ukristo tu! je Ukristo unaweza ukawa ndio dini ya haki ?

Mpaka hapo kama kuna mtu mwenye kuelewa anaweza akajua a to z kwanini makanisa yanachomwa.
 
nilishasema sana huko nyuma kwamba kero za muungano zinatumiwa kama kichaka na kikundi cha watu fulani wenye msimamo mkali kupitishia hoja zao za udini...kuchomwa kwa kanisa badala ya jengo la serikali kunadhihirisha hilo...!

hii ina ukweli...udini ndio tatizo kubwa...udini ni MOTO muungano ni PETROLI...
 
unaweza kutueleza kwa maneno machache kwa nini waislam wa zanzibar wana hofu kubwa sana na kanisa?

Wanaogopa jina la Yesu likitamkwaga mapepo na majini yao huwa yanatoroka so they think burning churches is the solution as also they thnk he stays in the buildings! Mtachoma makanisa ila Yesu anaeishi ndani ya wamwabuduo atadumu milele. Burning churches makes christians more stronger as they are in the battle and its not physical one...spiritual one. VITA VYETU SIO VYA DAMU NA NYAMA ILA NI VYA ROHONI TUKIPAMBANA NA HAO WAKUU WA GIZA.....!
 
Back
Top Bottom