Jihad ni nini? Idris Sultan aielezea kiundani

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Anaandika Idris,

Uzuri ni kwamba nimesoma fiqh.
Tuanzie maana ya neno “Jihad”, muhimu sana kuelewa kuwa Jihad sio vita ila ni mapambano.

Jihad inayozungumziwa na Quran kwa bahati mbaya imetafsiriwa vibaya na wengi kwa sababu zao binafsi. Hata ukipambana na ugonjwa, umaskini n.k ni Jihad na inakuhitaji usikate tamaa.

Kwenye upande wa Jihad kama vita za kijeshi kipindi cha mtume Muhammad (S.A.W), alipigana Jihad katika njia nyingi sana na asilimia 90% haikuwa vita za damu bali maongezi ya kutengeneza suluhishi, tunaweza sema kulikuwa na mizozo ila sio vita. Uislam ni amani, hata katika vita tumeweka human rights mbele. Hata wanajeshi wa adui tu hawakuuwawa walipokamatwa.

Jihad nyingi zilikuwa hazihusiani na dini moja kwa moja bali siasa za kulinda mipaka na makubaliano ya matumizi ya barabara za kibiashara kati ya miji. Katika Hijra 11 mtume Muhammad (S.A.W) akiwa kiongozi, 9 zilikuwa Jihad za amani kabisa na 2 tu ndo vita.

Kila muislam anapoamka asubuhi ana Jihad yake binafsi ambayo ana haki ya kuishinda. Kwasababu waislam tuna mavazi thabit basi akitokea kiongozi wa mji amevaa kanzu tutasema waislam wametangaza Jihad ? Hapana. Hata aya za kujilinda zilishushwa wakati wa vita ila kabla hatukurudisha mapambano.

Viongozi wana vita ila uislam hauna. Ndo maana ni muhimu kuchagua viongozi vizuri hasahasa katika dini. Tunataja vita za nchi kila siku ila hatusemi wakristo, wahindu, shinto, buddha wana vita na flani na flani.
 
Back
Top Bottom