Vurugu za South: Wazungu sio wageni?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Wanalengwa Waafrika tu. Wanateswa na kuuwawa. Wanakimbia na kukimbizwa. Wanaporwa mali zao. Wananyimwa uhuru wa kuishi kule Afrika Kusini. Kwani Wazungu na Waasia waliopo South si wageni? Kwanini weusi kwa weusi tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
Kasome maneno ailyoyatoa mzee Mugabe hivi karibuni utajua kwa nini wasaudhi wanauawa weusi wenzao na si wazungu.
 
Wanalengwa waafrika tu. Wanateswa na kuuwawa. Wanakimbia na kukimbizwa.Wanaporwa mali zao. Wananyimwa uhuru wa kuishi kule Afrika Kusini. Kwani Wazungu na Waasia waliopo South si wageni? Kwanini weusi kwa weusi tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Nitakujibu swali lako kwa swali! Serikali ya Tanzania imewarudisha/waokoa Waarabu/Wahindi wenye Uraia wa TZ ktk nchi ya Yemeni ambako kuna Vita, lakini Raia wa Watz ambao ni weusi walioko AK ambao pia ni kama wako vitani mpaka sasa hivi hakuna masaada wowote kutoka Serikali yetu inayoongozwa na Raisi mweusi, Waziri wa mambo ya Nje Mweusi na 99% ya wakazi wa hapa Bongo ni weusi!

Sasa ukipata jibu ni kwa nini basi labda utaelewa ni kwanini AK weusi wanaua wahamiaji weusi tu lakini Waarabu, Wachina, Wahindi, Wazungu, Machotara wanaachwa!

View attachment 245725 View attachment 245726 View attachment 245727

Dhambi ya Ubaguzi Haitakaa Ikaisha South Africa; Mwanzoni Waafrica walidhani ni Makaburu walikuwa wanawabagua Wazawa wa Kizulu na Makabila Mengine Kumbe siyo hivyo. Ubaguzi wa SA ni wa Kurithi toka Kwa Kaburu Botha hivyo hiyo ndio hali halisi ya SA.
 
Kasome maneno ailyoyatoa mzee Mugabe hivi karibuni utajua kwa nini wasaudhi wanauawa weusi wenzao na si wazungu.

Hata Mugabe naye ni wale wale tu hana tofauti yoyote na Waafrika wengine hata yeye kwake pia ana thamini Wazungu, Waarabu, Wahindi Wachina, Machotara kuliko Watu weusi!
 
Ubaguzi sio kwa Wazungu na Wafrika kubaguana. Kumbe hata Wafrika wenyewe kwa wenyewe wanabaguana, kweli tutafika.
 
Kalikuwa kadoooogo, tumekapa unga sisi wenyewe na sasa kamekuwa LIJOKA KUBWA!!!

Nyerere angethubutu kutuuliza nyakati hizo kuwa tuwasaidie ama tusiwasaidie kupigania uhuru wao kwa kweli tungemwambia "waache wajihangaikie kivyao"

Manake inaonekana sisi tuna macho lakini wenzetu hawana,

Sisi tunaufahamu ubinadamu wenzetu ni wanyama.

Sisi tunajali wao waaala!!!

Hii ni mizigo ya Nyerere.
 
Hii ni mizigo ya nyerere.

Acha kujidanganya Nyerere au sisi na Waafrika kwa ujumla hatujasaidia chochote AK!
 
Hiyo rahisi tu, Mugabe anatoa hotuba zake kwa Kiingereza hata Lugha rasmi ya Zimbabwe ni Kiingereza, ingawaje asilimia > 85% ya Wazimbabwe wanaongea au kuelewa Kishona! kingine?
ili uumie ni lazima utukanwe kwa lugha yako!
 
Acha kujidanganya Nyerere au sisi na Waafrika kwa ujumla hatujasaidia chochote AK!

Kwa taarifa yako tu, aliyewashawishi ANC kufanya mazungumzo na serikali ya Makaburu alikuwa Nyerere. Baadhi ya wanachama wa ANC hata walimtukana Nyerere kwa kupendekeza hilo, lakini Nyerere akashikilia msimamo kwamba kama mtu akikuita muongee ukawa unakataa bila kujua anataka kukuambia nini ni ujinga. Kataa atakachokuambia, sio kumsikiliza.

Hatimaye, ANC walikubali, na mazungumzo hayo yakazaa kuachiwa huru kwa Mandela na uchaguzi wa Kidemokrasia. Hii ni zaidi ya kambi alizowaruhusu wa South kuweka kule Morogoro (ANC) na Mbozi (PAC), na pia kuwa msemaji wao katika mikutano ya kimataifa kama UN na Commonwealth, kwa mfano Nyerere ndiye alisababisha South kufukuzwa uanachama wa Commonwealth.

Kwa hiyo usituletee hoja juu ya mambo usiyoyajua.
 
ili uumie ni lazima utukanwe kwa lugha yako!

Siyo kweli!
Mbona Ahmedijad(Raisi wa zamani wa Persia) alitukana Wazungu/wayahudi kwa Kipersia na Wazungu walitafsiri? Mbona Kim Jong- Un anatukana Wamarekani kwa Kikorea na Wazungu wanatafsiri? Mbona wa Mynmar wanatukana Wazungu Kimynmar na Wazungu wanatafsiri na kuelewa?

Mbona Ghadafi alikuwa anamtukana Reagan na Wazungu wengine kwa kiarabu na walimuelewa?
 
Tatizo lenu mnalishwa proganda kwa muda mrefu sana na kuamini hizo hadithi, kama vile zilivyo hadithi nyingine kwamba Nyerere aliwafukuza Wazungu na kuleta Uhuru Tanganyika au sijui Wakenya walipata Uhuru kwa sababu waliwapiga Wazungu na Mau Mau n.k!

Apartheid kuisha AK hakuhusiani kwa lolote na Mandela au sijui sisi Waafrika!
Apartheid ilikwisha kwa sababu Wazungu hasa Marekani walitaka iishe na isitoshe muda ulikuwa umefika na sababu kubwa ilikuwa ni kuisha kwa Vita Baridi kati ya Mashariki chini ya Urusi ambapo ANC walikuwa huo Upande na Magharibi chini ya Marekani ambapo makaburu walikuwa huo Upande!

Hivyo huo uhasama ulivyoisha na baadaye ukuta wa Berlini kuangushwa uadui ukaisha na hivyo Makaburu wakaambiwa na Wazungu wenzao ni lazima wamalize Apartheid walivyogoma Wazungu wenzao wakawawekea Vikwazo vya kichumi vilivyoanza kuuma wakasalimu amri na kumtoa Mandela Jela ambaye hata hivyo alikuwa ametayarishwa na Wazungu kuja kupewa Uraisi kama vile Nyerere alivyotayarishwa kuja kupewa Uraisi wa Tanganyika na Wazungu.

Na Mandela kabla hajapewa nchi akaambiwa kwanza akubali masharti yafuatayo moja hakuna kulipa visasi saini hapa akasaini, mbili ni lazima AK ibomowe Mitambo ya Mambo nguvu za Atomiki (Nuclear Bombs) wakasema sawa wakasaini ndiyo wakamtoa na kumpa Uraisi!

Hayo mengine yote ni Hadithi tu kama zilivyo hadithi nyingine nyingi!
 
Nitakujibu swali lako kwa swali! Serikali ya Tanzania imewarudisha/waokoa Waarabu/Wahindi wenye Uraia wa TZ ktk nchi ya Yemeni ambako kuna Vita, lakini Raia wa Watz ambao ni weusi walioko AK ambao pia ni kama wako vitani mpaka sasa hivi hakuna masaada wowote kutoka Serikali yetu inayoongozwa na Raisi mweusi, Waziri wa mambo ya Nje Mweusi na 99% ya wakazi wa hapa Bongo ni weusi!

Sasa ukipata jibu ni kwa nini basi labda utaelewa ni kwanini AK weusi wanaua wahamiaji weusi tu lakini Waarabu, Wachina, Wahindi, Wazungu, Machotara wanaachwa!

Ila wewe mbaguzi. Wawaita hawa weupe? Au ulitaka waokolewe weusi pekee? Nenda kafuatilie sababu za waio Yemen kurudishwa utakuta pengine wameahidi kulipa, au Bakhresa amewalipia!
 
Kwa taarifa yako tu, aliyewashawishi ANC kufanya mazungumzo na serikali ya Makaburu alikuwa Nyerere. Baadhi ya wanachama wa ANC hata walimtukana Nyerere kwa kupendekeza hilo, lakini Nyerere akashikilia msimamo kwamba kama mtu akikuita muongee ukawa unakataa bila kujua anataka kukuambia nini ni ujinga. Kataa atakachokuambia, sio kumsikiliza. Hatiamye ANC walikubali, na mazungumzo hayo yakazaa kuachiwa huru kwa Mandela na uchaguzi wa Kidemokrasia. Hii ni zaidi ya kambi alizowaruhusu wa South kuweka kule Morogoro (ANC) na Mbozi (PAC), na pia kuwa msemaji wao katika mikutano ya kimataifa kama UN na Commonwealth, kwa mfano Nyerere ndiye alisababisha South kufukuzwa uanachama wa Commonwealth.

Kwa hiyo usituletee hoja juu ya mambo usiyoyajua.

Hakuna ukweli hapo, ni porojo za mitaani tu.
 
Siyo kweli!
Mbona Ahmedijad(Raisi wa zamani wa Persia) alitukana Wazungu/wayahudi kwa Kipersia na Wazungu walitafsiri? Mbona Kim Jong- Un anatukana Wamarekani kwa Kikorea na Wazungu wanatafsiri? Mbona wa Mynmar wanatukana Wazungu Kimynmar na Wazungu wanatafsiri na kuelewa?

Mbona Ghadafi alikuwa anamtukana Reagan na Wazungu wengine kwa kiarabu na walimuelewa?
check your IQ again.
 
hiyo rahisi tu, mugabe anatoa hotuba zake kwa kiingereza hata lugha rasmi ya zimbabwe ni kiingereza, ingawaje asilimia > 85% ya wazimbabwe wanaongea au kuelewa kishona! Kingine?
tatizo lako pia ni ubaguzi yaani huna tofauti na wazulu au wazungu wabaguzi ama wengine walio na ugonjwa wa ubaguzi.nadhani mwenyezi mungu alituumba ili tuishi kwa kuhurumiana na kukosoana pale tunapokosea ili kurekebishana.ni lazima kupnga uaguzi kwa nguvu zote na huwezi kuzuia ubaguzi kwa kubagua
 
Tanzania tulipoteza muda na rasilimali kusaidia wenzetu kupata uhuru..sasa sisi maskin wao matajir...babu nyerere alitereza ktk hili...
 
Kwa taarifa yako tu, aliyewashawishi ANC kufanya mazungumzo na serikali ya Makaburu alikuwa Nyerere. Baadhi ya wanachama wa ANC hata walimtukana Nyerere kwa kupendekeza hilo, lakini Nyerere akashikilia msimamo kwamba kama mtu akikuita muongee ukawa unakataa bila kujua anataka kukuambia nini ni ujinga. Kataa atakachokuambia, sio kumsikiliza. Hatiamye ANC walikubali, na mazungumzo hayo yakazaa kuachiwa huru kwa Mandela na uchaguzi wa Kidemokrasia. Hii ni zaidi ya kambi alizowaruhusu wa South kuweka kule Morogoro (ANC) na Mbozi (PAC), na pia kuwa msemaji wao katika mikutano ya kimataifa kama UN na Commonwealth, kwa mfano Nyerere ndiye alisababisha South kufukuzwa uanachama wa Commonwealth.

Kwa hiyo usituletee hoja juu ya mambo usiyoyajua.

Huyo jamaa hajui anachoongea hivi makubaliano ya kempton park anajua ANC walikuwa wanamsikiliza nani na alikuwa anawaambia kila jambo la kukubali ama kukataa? Ukombzoi wa Africa Kusini Tanzania imeplay part kubwa sana na watu wetu wamemwaga damu wengi tu na tumetumia pesa nyingi sana kuiomboa africa ya kusini.Tatizo watu hawasomi historia wakajua ila wanazuka na kupinga mambo wasiyo yajua.
 
Back
Top Bottom