Vurugu za South: Wazungu sio wageni?

Vurugu za South: Wazungu sio wageni?

Kwa taarifa yako tu, aliyewashawishi ANC kufanya mazungumzo na serikali ya Makaburu alikuwa Nyerere. Baadhi ya wanachama wa ANC hata walimtukana Nyerere kwa kupendekeza hilo, lakini Nyerere akashikilia msimamo kwamba kama mtu akikuita muongee ukawa unakataa bila kujua anataka kukuambia nini ni ujinga. Kataa atakachokuambia, sio kumsikiliza. Hatiamye ANC walikubali, na mazungumzo hayo yakazaa kuachiwa huru kwa Mandela na uchaguzi wa Kidemokrasia. Hii ni zaidi ya kambi alizowaruhusu wa South kuweka kule Morogoro (ANC) na Mbozi (PAC), na pia kuwa msemaji wao katika mikutano ya kimataifa kama UN na Commonwealth, kwa mfano Nyerere ndiye alisababisha South kufukuzwa uanachama wa Commonwealth.

Kwa hiyo usituletee hoja juu ya mambo usiyoyajua.

Hata matangazo yao ya Redio-"Umnkotho We Sizwe" (Mkuki wa Taifa), kwenda Afrika ya Kusini walikuwa wanarusha kutoka Radio Tanzania. Watanzania tulisidia kwa HALI na mali, tulichanga hata kutoa misaada ya nguo na viatu kwa wapiganaji wa South Africa waliokuwa nchini.

Ni kutokana na kutambua mchango ambao Watanzania waliutoa katika ukombozi wa Afrika ya kusini, ndio maana mara tu baada ya Mandela kutoka kifungoni, nchi ya kwanza kutembelea ilikuwa Tanzania. Alikuja kuwashukuru Watanzania kwa mchango wao katika ukombozi wa nchi yake.

Ni bahati mbaya sana kuwa somo la historia lilipuuzwa hivyo kuacha wengi kutokujua tulipotoka. Kwa hali hiyo ni vigumu sana kufanya uchambuzi wa matukio ya sasa kama hujui historia yako.
 
Mm naona away jamaa zetu naona kama awajitambui coz hao waafrica wanaofukuzwa sauth ndo waliyo zaidia sauzi kupata Uhuru Leo hii wanawafukuza kama mbwa dhambi yao nikubwa kuliko wao wanavyofikili na mzimu wa ubaguzi wa mda mrefu kwao ila now wameamua kuweka wazi
 
Niliwahi kusoma makala moja ya Gazeti ilikuwa inazungumzia Mandela alipomwacha Mke wake Winie ilibidi aje Tanzania kwa ajili ya kupumzika na alienda kukaa kwenye mbuga za wanyama huko Arusha akiwa na Barozi Mpungwe kama msaidizi wake,alipokuwa kule alikuwa akitembea na kuonana na wana vijiji wa karibu na maeneo hayo lakini hawakumgundua maana alikuwa anakuwa kama mtu wa kawaida sana kwa maana muonekano wake.

Thabo Mbeki alipokuwa makamu wa Rais naya aliwahi kuagizwa na mandela kwamba anapaswa kumpuzika na aliletwa Tanzania akakaa huko kwenye mbuga za Wanyama pasi watu kujua.Naeleza haya ili sisi watanzania ambao hatujui mambo haya hasa jinsi tulivyoisaidia sana South africa tuache kupinga mambo ambayo kumbe hata hatujui.Kuna mtu amekera sana aliposema ANC hakuwahi kusaidiwa na nchi yeyote ya Kiafrica nimemshangaa sana anaweza ama kuwa mjinga tu hajui anachosema au ni mvivu wa hata kusoma ili ajue mambo.
 
Wanalengwa Waafrika tu. Wanateswa na kuuwawa. Wanakimbia na kukimbizwa. Wanaporwa mali zao. Wananyimwa uhuru wa kuishi kule Afrika Kusini. Kwani Wazungu na Waasia waliopo South si wageni? Kwanini weusi kwa weusi tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Malema aliwahi kuhoji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kupinga ubaguzi kwa kubagua watu,kama unapinga ubaguzi kemea ubaguzi unaofanywa tu usiwaingize wazungu na wadosi.Hao waafrika kusini nao ni wajinga.
 
Hata kama tuliwasaidia tusiwafanye watumwa wa msaada.Mtu ukimsaidia sio lazima na yeye akusaidie
 
Back
Top Bottom