Rais anongoza Taifa kwa matamko ya kukurupuka!Mkuu tatizo la serikali yetu ni kuongozwa na viongozi waliogubikwa na nidhamu ya woga.Binafsi sikuona mantiki ya kila waziri kujinasibu kwenye vyombo vya habari huku wakitoa matamko yenye kila rangi juu ya adhima ya kuhamia Dodoma.Rais kutamka kuwa atahakikisha ametimiza ahadi iliyoahidiwa kwa muda mrefu kuhamia dodoma ndani ya miaka hii iliyosalia alijua kuwa bado anahitaji kudunduliza vijisenti katika bajeti zilizobaki kabla ya kuhitimisha muhula wake wa uongozi.
Tatizo ni kutoelewa kusudio la mkuu wa nchi kuwa hakusema waanze kuhama wala kufurahisha hadhira kupitia matamko yao.Kusema akihama tu waandamizi wake inabidi wafanye hima.Mkuu sasa wameumbuka maana kuna waliosema mwisho wa wiki hizi zilizopita eti watakuwa wametimiza agizo la mkuu kumbe hawakudhani kuwa isingewezekana kwani si kuhama wao tu bali waandamizi wote.Daima kesheni mkiomba utajiri wa FIKRA na uwezo wa kutafakari kabla ya kutenda.Samahani wakuu nimewaza kwa sauti.
Uko sawa sana mkuu. Ni kama ile bomoa bomoaSaa hizi matamko ya dodoma yamekwisha na nina amini hatutoyasikia tena itatafutwa nyimbo mpyaaaa ya kuibuka nayo hii ndo awamu ya tano
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji30] [emoji30] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Naomba mawaziri wote waliomdanganya Rais kuwa wataamia Dom baada ya wiki mbili wachukuliwe hatua kama wadanganyifu
Tumeona Anna Kilango a poll iwajibishwa kwa kudanganya na wao the same bila hivyo ni double standard
Mkuu Mshana nimekubaliana na wewe kwa kiasi lakini kiasi pia natofautiana na wewe.
1. Kiusalama ikitokea vita (Mungu aepushie mbali) kutekwa kwa mji mkuu ni ishara kuwa nchi/Serikali imeangushwa. Dodoma bado inakuwa sehemu nzuri ikitokea cha kutokea. UUwepo wa Dar kama mji mkuu yenye serikali kandokando ya bahari (maji) ni tatizo.
2. Hoja ya kupanua Dar es Salaam ili mji upumuo haina mashiko. Kinachokosekana mji huu ni mipangomiji, serikali kutokuwekeza kwenye makazi na hulka ya kila mtu kuwa na kiwanja chake. Unapopanua mji zaidi unaongeza gharama za uwekezaji kwenye miundombinu. In fact huu mji haukupaswa kuzidi 20 Km radius kutoka mjini kati ili maeneo mengine watu waendelee kulima na kupanda miti.
Kwangu, suala la kuhamisha serikali Dodoma ni nzuri nina tatizo na huu uharaka basi.
Mh jeni ester alisema wizara yake yote wiki hii itakuwa imeshahamia Dodoma
...Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?...
Sheria ya mitandao inakuhusu na vi komenti vyako vya hasira utaishia jera, Punguza Jazba na kashfa mwana JF!Mkuu nimekuelewa mzee.
Tatizo la serikali hii wao kazi yao ni kukurupuka na kutoa matamko tu.
Hawajui wala kutaka kupembua mambo kwa kutumia akili.
Akili ya Magufuli ni sawa na mtoto kaona nzi kwenye bakuli la uji. Badala ya kuchukua kijiko na kutoa yule nzi,atampiga nzi kibao na kumwaga uji wote,mwisho wake kumuunguza.
Yetu sisi macho. Anajifanya kucheza ba maisha ya watu na amani. Ubabe yeye,matamko yasio na tija ni yeye. Huyu mtu ana aakili timamu kweli?
ulipotelea wapi mkuu?Unaweza kuta Raisi alisema akihama yeye wengine watafuata lakini wakati huo huo akampa maelekezo Majaliwa aanze kazi mara moja ya kuhamia Dodoma ,