Vuguvugu la "occupy" linasambaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vuguvugu la "occupy" linasambaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanakili90, Oct 16, 2011.

 1. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  16 Oktoba 2011 09:57 Maandamano duniani kote ya kupinga kile waandamanaji wanakiona kama uroho nausimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingiasiku ya pili. Katika miji kadhaa - kutoka Auckland hadi Toronto - waandamanaji walikesha katika mahema kushinikiza wanasiasa wachukue hatua.

  Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga mambo yanayotokea mjini New York, katika mtaa wa masoko ya fedha, ambako maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana kwa wiki
  kadhaa. Mjini London waandamanaji wamelala nje ya kanisa kuu la Saint Paul, katikati ya jiji, baada ya kuondoshwa jana nje ya Soko la Hisa.

  Watu kama 500 walibaki, na wengi wao walilala kwenye mahema kama 70, wengine walikaa juu ya ngazi nje ya kanisa. Wana kauli moja - wamekerwa na serikali ya mseto ya Uingereza kubana matumizi, na wamehamaki kuwa mabenki yanasaidiwa. Biramu moja linasema "mwisho umefika".

  Wanalalamika kuwa demokrasi haifanyi kazi na wanasema watabaki hapo wakiwa ni sehemu ya vuguvugu la dunia. Baadhi yao wanasema wanaweza kubaki hapo hadi Disemba.

  Source:BBC
   
 2. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  tu-i copy nini! Maana ndo kilichobaki.
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  dah! kuna moja leo imeniacha hoi....jamaa walijipanga nje ya stanbic bank wakitaka ku withdraw pesa zao zote......
  lucky me niko huku kwetu kasulu i dont have to worry about a ****ed up world economy!
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaani wewe hapo uko huko vijijini Kasulu na ndipo ukatutangulia kusikia ya mijini sio? Wakati mwingine unapounda uongo ni bora uwekeze walau muda wa kufikiri.

   
 5. y

  yaya JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, siyo ku-kopi (copy), ni occupy, yaani miliki au chukua, hili ni vuguvugu ambalo limeanza kuenea sasa dunia yote ya nchi tajiri sana na zilizoendelea kiviwanda. Ni kwamba wananchi wanaandamana kupinga sera za kifedha (kiuchumi, zinazopendelea mabenki) za nchi zao na kutowajali wananchi wa kawaida ambao wanaathirika kiuchumi kutokana na sera hizo. Lengo la waandamanaji ni kuzitaka serikali zao ku-review sera hizo ili ziwe fair kwa pande zote, wananchi na mabenki. Vuguvugu hilo limepewa jina la Occupy...... halafu unataja jina la mji mnakoandamana. Mfano Occupy Tokyo.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Hivi bongo hakuna corporations?Ama zenyewe si greedy?
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Vyombo vya fedha na mabenki yapo Tanzania. Tena yanawakomoa wateja. Unauliza uroho wa corporations wakati huo ndio mfumo kwao?
  Hili la uroho wa fedha haliko kwa mabenki tu. Tz tunaadhibiwa na tunaathiriwa na "ufisadi" pia. Kigenge cha wezi wanaojichukulia fedha za umma huwa wanaonekana ndio wajanja na wameula kimaisha.

  Ukiweka fedha zako chache benki, siku umekumbuka kuwa uliweka 50,000 elfu zako ,ukienda kutaka kuzichukua unaambiwa;
  "doooh, ulikuwa wapi? Tunakutafuta siku nyingi, una deni la 20,000 kama ada ya akaunti"

  Yaani 50,000 elfu yako imekwenda na maji na deni juu! Unapandwa na hasira lakini unapokumbuka kuwa TZ ni kisiwa cha "amani na utulivu", unageuka kuelekea mlangoni na kwenda kulalamika nyumbani.

  Sera za IMF na World bank zilipoletwa miaka ile, wanasiasa, viongozi wetu walituambia tukaze mikanda na tuchangie huduma za jamii.
  Wao wanajiengezea kima cha mishahara na masurufu, marupurupu.

  Kasumba ya tukaze mikanda na utamaduni wa kutoa na kupokea rushwa umetufanya tuone kila kitu ni sawa tu.

  watanzania tumeacha kujifikiria kama jamii, tunachofanya ni kila mtu kuchumia tumbo lake hata kama ni kuwaumiza watanzania wenzake.
  Hata wale walio waelewa wa mambo badala ya kuuamsha umma na kuchukua hatua , ili kushibisha" tumbo" wanakimbilia kwenye "kula" aka siasa.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hv sisi tunasubiri nini wakuu? kama hata uingereza wamestuka sisi tuna nini mpaka tuwe wavumilivu namna hii?
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Huku kwetu vipi?.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Nadhani viongozi wetu washatulazimishia kufikiri kuwa shida na umasikini ni tamaduni zetu.
   
 11. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa ubongo wa panzi,watu kama faizafoxy,omr,makupa unategemea nini?
  Amin nakwambia, mambo yakibadilika wakina nape wataikimbia nchi,kukwepa malipo ya uwongo wao.
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  "Mzee"
  Tueleze njia mlizotumia mlipokuwa vijana ili zitumike sasa.
   
 13. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mara nyigni maandamano ndo njia mbadala ya kujinasua kutoka mikononi mwa simba wala watu
   
 14. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mhhhhhhhhhhhhhh


   
 15. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Neno democracy limetokana na maneno mawili.Yaani Demon na crasia.Maana ya demon unaijua na crasia ni neno la kilatini lenye maana ya authority.Kwa hiyo democrasia au democracy maana yake ni utawala wa mapepo.Sijui kama unaona jinsi tulivyoingizwa mkenge.Sasa katika utawala wa mapepo unategemea nini.Obviously kilio na kusaga meno.Na bado,matumbo yatauma kwa dhiki zilizopo mbele yetu.
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Licha ya Mabenki kuna wizi mkubwa sana unafanywa na makampuni ya simu hapa Tanzania kwa wateja lakini serikalia kupitia TCRA na Umma wote umetiwa maji na kutota!
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo Nyerere anapokuwa nabii/professor; Thanks Magoba!
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Vodacom
   
 19. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Na Karly Max na Vladimir Lenin wanapokuwa Manabii Wakuu au miungu kabisa, Lol!!...
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Tena yanawakomoa sana kwa kuwatoza riba kubwa kupita kiasi. Sasa hivi nchi nyingi za Magharibi, kama unachukua mkopo kwa fixed rate basi watakupa kati ya 3% mpaka 4% kwa miaka mitano na kama ni variable rate unaweza kupata kati ya 2.5% mpaka 3% lakini nchini kwetu sasa hivi riba ya mkobo kutoka katika mabenk yaliyopo nchini kama sikosei iko juu ya 12% huu ni wizi wa hali ya juu.
   
Loading...