"Vua GAMBA, vaa GWANDA" litawatosha bila vipimo!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Vua GAMBA, vaa GWANDA" litawatosha bila vipimo!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uncle Jei Jei, May 10, 2012.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Slogani hii ilitumika juzi kwenye mkutano wa hadhara wa chadema huko Arusha. Lengo kuwakaribisha na "kuwahamasisha" wanachama wapya toka vyama mbalimbali hasa CCM. Napata shida mfumo huu wa "kuvuna"wanachama wapya. Hivi, CDM wanatumia vipimo gani kupima kama kweli wanaokuja wana nia dhabiti ya kuleta maendeleo? Nasema hivi kwa sababu,upepo wa kisiasa ulivyo sasa wanasiasa wengi "maarufu"hasa wa CCM wanahaha, hawajui kesho kutaibuka nini! Cdm, hamuoni kuwa "wapuuzi"wachache, wenye tamaa ya kuendelea na madaraka wanawezakutumia mwanya huu kujipenyeza ili nao 2015 wapate angalau jimbo? Mfano mzuri ni 2010,kwa Arcado Ntagazwa alipotoswa kwenye kura za maoni na CCM, fasta alijiunga Chadema na kuomba tena Jimbo la Muhambwe (kibondo), Dr.SLAA ni shahidi wa kilichowapata wakati wa kumnadi! Wito wangu, CDM kuweni makini na hao wanachama wapya!! "Msije"pokea na wasiofaa!
   
Loading...