Vua gamba vaa gwanda yaendelea kuitesa ccm kwenye uchaguzi wa udiwani kata ya mwawaza-shinyanga mjin

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kwa baadhi ya kata hapa nchini zimeanza kwa kishido huku baadhi ya vyama vya siasa zikiendelea na sera zao za maji taka badala ya kujikita zaidi katika matatizo yanayomsibu Mtanzania Mlalahoi.

Jana majira ya saa kumi na moja jioni nikiwa kwenye viwanja vya shule ya msingi Ugimbagu nikihudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa udiwani wa kata ya Mwawaza,uchaguzi ambao umesababishwa na kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kupitia CCM,nilishuhudia malalamiko toka miongoni mwa wakazi wa kata hiyo kutokana na serikali ya CCM kuwatelekeza na kushindwa kuwapelekea huduma muhimu kama vile maji,zahanati na umeme toka kuumbwa kwa dunia hii.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wanachama wa CCM kuamua kujivua gamba na kuvaa gwanda kwa kurudisha kadi zao za uanachama wa CCM toka 1977.Mbaya zaidi walilaani kitendo cha wanachama wa CCM kwa kuungana na mbunge wao ambaye ni naibu waziri wa madini mh.Steven Maselle kumnywesha pombe baba mzazi wa mgombea toka CDM kisha kumpandisha jukwaani kumkashifu mwanaye kuwa ni jambazi ambalo halifai kupewa kura.

Hali hiyo ilitokana na mgombea huyo wa udiwani kupitia CDM kwa jina la Anthony Peter Mhola kupigwa risasi na kutuhumiwa kuwa jambazi mpaka pale mahakama ilipokuja kuthibitisha hana hatia.Kitendo cha kumtumia mzee huyu kumsaliti mwanaye kipenzi ambaye ndiye anaye angalia maisha ya baba yake kiliwaudhi sana wakazi wa maeneo hayo ya Ugimbagu na kumsababisha mama yake mzazi na Anthony kuamua kurudisha kadi ya CCM.

Akiongea kwa masikitiko makubwa Mkurugenzi wa kamati ya ulinzi na usalama wa CDM taifa mh. Alfred Muganyizi Rwekatare alimuombea kura mgombea huyu kupitia chama cha CDM na kuwataka wananchi wawaone huruma wale wote wanao kishabikia Chama Cha Mapinduzi Kwa kushindwa kumjali mkulima katika kumboreshea bei ya mazao yake huku wakitumia pesa kubwa katika chaguzi mbalimbali kwa kuwanunua na kuhujumu wapiga kura kwa bei ya kutupa.

Akiongozana na makamanda wenzake toka kurugenzi ya sheria na usalama walipokea kadi mbalimbali za wanachama waaminifu wa CCM walizopewa toka mwaka 1977 ,waliamua kujivua gamba na kuvaa gwanda kama itakavyojidhihirsha hapa chini kwenye picha.

Akiomba kura za kutosha na kuwataka wapiga kura wa kata hiyo ya Mwawaza kuwa walinzi wa kura zao,mgombea huyo wa CDM alisistiza kaulimbiu ya CDM ya kuwachagua viongozi miongoni mwao wakazi wa maeneo husika kwani wao wanajuana na shida zao wanaziajua kiasi ni rahisi kufuatilia kwa kuwa tu nao ni miongoni mwa waliotelekezwa na serikali ya CCM toka kuumbwa dunia hii.

Mkutano huu uliongozwa na mwenyekiti wa CDM wilaya ya Shinayanga mjini bi Siri Yasini ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wapiga kura ambao muda wote wa mkutano walionekana na uchungu na maisha yao,kwa kukosa huduma muhimu kama maji ilihali wakilipa kodi kwa maendeleo ya taifa hili.

Kampeni hizo zitaendele tena leo huko sehemu za Negezi,huku CCM nao wakiendelea na kampeni katika vijijj vingine vya kata hiyo.Fuatilia kw umakini matukio ya picha yaliyojiri hiyo jana .
 

Attachments

  • vua gamba.JPG
    vua gamba.JPG
    39.3 KB · Views: 79
  • vua gamba vaa gwanda.JPG
    vua gamba vaa gwanda.JPG
    51.9 KB · Views: 66
Ahsante kamanda, mitaa yangu hiyo!! Nafurahi kuona watu wanaamka kutoka usingizini!! Natumaini elimu ya uraia inazidi kupanuka, watu wanazidi kuelewa nani haswaaa anawalaghai na nani anawatakia mema. Kila la kheri wenye kuwasaidia hawa wananchi specifically viongozi wa CDM pamoja na makamanda mnaotumia muda mwingi kuwasaidia wananchi kujitambua.
Imani yangu ni kuwa kama kila mtu atajua haki zake, wajibu wake na kuona ni nani anaweza kumuongoza kwa hiari yake, tutasaidiana.
 
Mbaya zaidi wanajaribu kuchakachua mpaka akili za wazee kwa kuwalaghai kama utakavyoona kwenye hii video itayokuijia soon
 
Ahsante kamanda, mitaa yangu hiyo!! Nafurahi kuona watu wanaamka kutoka usingizini!! Natumaini elimu ya uraia inazidi kupanuka, watu wanazidi kuelewa nani haswaaa anawalaghai na nani anawatakia mema. Kila la kheri wenye kuwasaidia hawa wananchi specifically viongozi wa CDM pamoja na makamanda mnaotumia muda mwingi kuwasaidia wananchi kujitambua. Imani yangu ni kuwa kama kila mtu atajua haki zake, wajibu wake na kuona ni nani anaweza kumuongoza kwa hiari yake, tutasaidiana.
HIVI CCM AKILI YA KUKAA HADI SAA 6 UNUSU WANAITOA SAYARI GANI. KWA TAARIFA YAO MWEZI 1 ULIOPITA NILIKUWA S'WANGA MUNCIPAAHUKO CCM HAINA CHAKE. CCM WAACHE KUFANYA KAMPENI NAWASHAURI WAJIANDAE KUIBA KURA. NDIO NI LAZIMA IWE KWASABABU UKIZUNGUMZIA HABARI ZA CCM NI LAZIMA UWE MWENDAWAZIMU HASA KTK KIPINDI CHA BAADA YA UCHAGUZI WA NDANI WA CCM. WATU WAMEJERUHIWA VIBAYA NA WANAAPA WALAH CCM SSM WAVURUMUSHWE MAWE POPOTE PALE WALIPO HAWANA ADABU KWA TABIA YA KUWEKANA NA RUSHWA ZA MCHANA KWEUPE Hatahivyo, UVCCM wametakiwa kukaa mbali na uchaguzi huo kwakuwa kwasasa hawana picha nzuri kwa jamii kutokana na kile kinachoendelea katika chaguzi zao. Ningweza kuandika mengi.Lakini nina 'hang-over' ya mkutano wa Lumumba.Kumekucha![/QUOTE]
 
Back
Top Bottom