Campain Vua Gamba Vaa Gwanda imeanza

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Tanzania Daima 05/05/2012

Operesheni vua gamba, vaa gwanda kuzinduliwa leo



na Grace Macha, Arusha




CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha leo kitazindua operesheni maalumu inayojulikana kama “vua gamba vaa gwanda” iliyolenga kuhamasisha wananchi hususan wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujiunga na chama hicho.

Mbali na uzinduzi huo, viongozi wa juu wa CHADEMA watawapokea rasmi wanachama wapya pamoja na wale waliojitoa CCM hivi karibuni akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, James Millya.

Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Amani Golugwa, alisema operesheni hiyo itazinduliwa kwenye viwanja vya NMC majira ya saa nane mchana baada ya kupata ridhaa ya jeshi la polisi.

“Kwa kweli tunatarajia kupokea wanachama wengi kwani kwenye ofisi zetu za matawi tumepokea wanachama wengi ambao wanahitaji kadi za CHADEMA baada ya kurudisha za CCM sasa sisi tukasema kuwa ni vema zoezi hili tukalifanya kwa pamoja kesho kwenye viwanja vya NMC ili kutuma salamu kwa CCM kuwa sasa wananchi wameamka hawadanganyiki tena na wamechoshwa na ahadi za maendeleo zisizotimia,” alisema Golugwa.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye, akiongea na Tanzania Daima kwa njia ya simu alithibitisha kuwa na taarifa ya mkutano huo na kuwa wametoa kibali.

Wakati huohuo Baraza la Wanawake la Chama hicho (BAWACHA) mkoani hapa limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanawake ndani ya chama hicho ambapo kwa sasa wameanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kufanikisha hilo.

Mwenyekiti wa Bavicha mkoani hapa, Cecillian Ndossi, alisema kuwa mfuko huo utachangiwa na wanawake kwa lengo la kuwezesha zoezi la uhamasishaji kwenye maeneo yote ya mkoa huo hasa yale yaliyo mbali ambayo hayafikiki kwa urahisi kutokana na jiografia ya maeneo husika.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi na wanachama wa CCM kwenye maeneo mbalimbali kujinga na CHADEMA huku wakiushutumu uongozi wa chama hicho tawala kwa kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kushindwa kutatua tatizo la ajira kwa vijana.
 
Tafadhari isambae kamaoparesheni sangala.tunawahitaji na tunaomba mfike muleba kusini kwa pro.tibaijuka
 
Badilisha heading hapo juu, siyo Campaign ni Operation Vua Gamba Vaa Gwanda ingia msituni.


Msako unaendelea
 
"The first step toward change is acceptance." "Once you accept yourself, you open the door to change. That's all you have to do." "Change is not something you do, it's something you allow."- Will Garcia. So I beg my fellow tanzanians to allow the change.
 
Hahahahha, nimeipenda hii operation! hakika CDM will always be smart!!
Siku Chadema wakiwa smart, nahisi ni siku ambayo labda nchi nzima ya Tanzania itahamia kanda ya kaskazini.."ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".."WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Back
Top Bottom