Vodacom wanaingilia mpesa ya mteja na kutoa pesa zote kulipia nipige tafu bila hiari ya mtu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Voda wanaingilia mpesa ya mteja na kutoa pesa zote kulipia nipige tafu bila hiari ya mtu

Niwape indhari kuna mtindo voda wamekuja nao, kama unadaiwa nipige tafu mfano 500 ukitaka kununua kifurushi kupitia mpesa mfano kifurushi cha 5000 wanachokifanya ukilipia kwa mpesa wanachukua elfu 5 ulolipia kifurushi kwa mpesa hawakupi kifurushi bali wanaielekeza hiyo 5000 kuja kwenye salio la kawaida wanakata 500 yao halafu hiyo 4500 iliyobaki wanaibakisha kwenye salio la kawaida haya wanafanya bila hiari ya mteja huu ni wizi

Kwanini wasikate pesa wanayodai tu badala yake wanaingia kwenye mpesa na kukomba kiasi chote ulichotarajia kununua kwenye mpesa kisha wanaweka kwenye salio la kawaida bila khiari ya mteja? Huu utaratibu wa kibazazi voda mmeutowa wapi?hii ni too much kwa kweli

Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida...

Tabia mbovu saaana hii wanafanya..!

Wanapaswa kukata deni lao halafu inayobaki waiache MPESA, kitendo cha kuileta kwenye muda wa maongezi sio sahihi

Halaf inakua ni shida pale unapotaka kujiunga na vifurushi ambavyo masharti yake ni kwamba unatakiwa ulipie kwa mpesa tu yaan hivyo vifurushi vinalipiwaga kwa mpesa tuu sasa wanakuwekea hiyo hela kwa salio la kawaida, hapo inakua ishakula kwako maana hautoweza kujiunga tena hicho kifurushi hiyo hela inaishia kudonolewa tu na wao kwenye hilo salio....
 
Mkuu hujanielewa.
Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida
Lipa deni mzee, hii tabia ya kihuni mtaacha lini watanzania? Obligation yako huijui endapo unaingia mkataba wa kukopa? Mi naona hao jamaa hawana tatizo ila wewe ndio mwenye shida mahali flani!

Vodacom, hapo poooa!!!
 
Mkuu hujanielewa.
Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida
Ofcourse kuhamishia salio lote main account sio sahihi
 
Hapa hamjamuelewa mtoa mada ,ni kwamba wanakata ela yao wanaokudai alafu iliyo baki wana amisha yote kuwa salio la kawaida au vocha ambayo mdaiwa haitaji yote kuwa wakati uo...
 
Hii Wanaita kukopa sherehe kulipa matanga. Wakati wa kukopa mnabonyeza tu code then mnabadilisha njia ya kuunga vifurushi mnatumia Mpesa, acha warudishe chao
Ndo ilikuwa lengo lake jamaa wakamfuata huko huko mpesa nimecheka mm km sina salio na beep tu airtel kukopa hapanakwa kwel
 
Ni sawa unaenda dukani kwa mangi. Kwa kuwa ulikopa sukar ya mia5 jana, leo unaenda kwake na elf5 kupata bidhaa ya elf 2 , anakata deni, bidhaa husika anakupa na chenji harudishi anakujazia bidhaa usiyoitaka.
 
Watamuwekea wimbo wa zuchu nampatia sukar km mwito wa simu adi kesho hamna kitu humo akienda customer care sasa hahahah ulibonyeza moja tuma ONDOA kwenda namba fulan
Unaambiwa ulijiunga na huduma ya ringtones
 
Mkuu hujanielewa.
Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida
Ungekua umelipa deni wasingefanya hilo lililofanyika
 
Back
Top Bottom