Vodacom Tanzania ni wezi

sweetdada

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
517
169
Vodacom mlichonifanyia sio sawa. Nilikuwa na 142,000 tarehe 1 April asubuhi. Nikajiunga na red relax ya elfu 50. Leo nimemuunga rafiki bundle la 2500 nacheki balance nakuta 40,000.

Nikapiga call centre wamenambia niliweka la kujirudia. Sijawahi hata siku moja kuweka la kujirudia ina maana ya kwamba mmeniibia elfu 50.

Tafadhali nahitaji kurudishiwa elfu 50 yangu Mchukue hilo bando lenu mliloliweka bila idhini yangu. Huu ni uwizi wa kimachomacho.

Cha kuchekesha mnaniambia kifurushi cha kujirudia kimeungwa saa nne asubuhi. Wakati siku zote mimi kujiunga mwenyewe saa 12 asubuhi haijawahi kufika saa nne ili kuepuka hela kuisha na niweze kuwasiliana. Rudisheni elfu 50 yangu acheni uwizi
 
Skilizia kwanza mwanadada pengine wamefanya labda kwasababu ni april fool
 
Vodacom mlichonifanyia sio sawa. Nilikuwa na 142,000 tarehe 1 April asubuhi. Nikajiunga na red relax ya elfu 50. Leo nimemuunga rafiki bundle la 2500 nacheki balance nakuta 40,000.

Nikapiga call centre wamenambia niliweka la kujirudia. Sijawahi hata siku moja kuweka la kujirudia ina maana ya kwamba mmeniibia elfu 50.

Tafadhali nahitaji kurudishiwa elfu 50 yangu Mchukue hilo bando lenu mliloliweka bila idhini yangu. Huu ni uwizi wa kimachomacho.

Cha kuchekesha mnaniambia kifurushi cha kujirudia kimeungwa saa nne asubuhi. Wakati siku zote mimi kujiunga mwenyewe saa 12 asubuhi haijawahi kufika saa nne ili kuepuka hela kuisha na niweze kuwasiliana. Rudisheni elfu 50 yangu acheni uwizi
Aise pole sana, Vodacom siku hizi wamekuwa wezi sana. Hata mimi walikula salio langu la M Pesa nikashangaa, kuwauliza wananiambia nilicheza bahati nasibu yao ndiyo maana hela imekatwa. Nikauliza bahati nasibu si mpaka ucheze

mwenyewe na uruhusu hela itoke M Pesa, imekuwaje nyie mnanikata moja kwa moja toka M Pesa kitu ambacho kwangu ni haramu kucheza.

TCRA wanahitaji kuwamulika hawa voda, wamekuwa wezi sana. Pia wanakuunga huduma bila ya ridhaa yako mtumiaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu heunda ni kweli, hebu cheki hapo, pamekaribiana sana. Uli click kwenye Tshs 50,000 renewel. Pole sana
Screenshot_20200402-135720_My%20Vodacom%20Tanzania.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda wameajiri wahudumu vilaza sana, kunasiku nilisajili laini mpya kila nikiweka namba ya siri ili ku-activate account ya mpesa ilikua haileti changes zozote

Ikanibidi nipige customer care ili nitatutliwe tatizo langu. Mtoa huduma kwa wateja namuelewesha kua kila nikiweka namba ya siri ili kuwezesha huduma ya mpesa inashindikana

Jamaa akaniambia inashindikana kwasababu umeweka mwaka wa kuzaliwa, mimi nikampinga nikasema hapana nimeweka 3000 sijaweka mwaka wa kuzaliwa

Jamaa akasema hiyo 3000 ni mwaka wa mbeleni hivyo nao ni mwaka wa kuzaliwa vile vile

Nikasema fresh niambie niweke namba ya siri kama ipi

Akasema weka 7890

Nikamjibu nao huo si mwaka wa mbeleni ambao bado hatujaufikia kama huo mwaka wa 3000 ulionikataza mimi

Nikasikia asante kwa kuchagua vodacom nikutakie mchana mwema ahsante, kisha simu ikakatwa
 
Vodacom toka makampuni ya simu yalete option ya kutuma pesa mitandao mingine niliwapiga chini muda natumia airtel hawanaga longolongo nikifeli sana natumia halotel. voda na tigo ni mitandao ya wanyonyaji sana hasa voda.
 
Mkuu heunda ni kweli, hebu cheki hapo, pamekaribiana sana. Uli click kwenye Tshs 50,000 renewel. Pole sanaView attachment 1406630

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mimi kawaida sijiungi saa nne asubuhi na haitawahi kutokea nikajiunga saa nne asubuhi. Wao wanasema saa nne asubuhi ndo renewal imepita wakati kwa ufahamu wangu muda renewal inaitwa ndo muda ule uke uliojiunga mara ya mwisho.

Vodacomni matapeli wa kimataifa sio kwa kuniibia huko 50k kwa usawa huu
 
Halafu hiki kitu wamekianzisha. Ni manunuzi ya kifurushi. Mf. Kifurushi cha Internet 35,0000 GB 10+GB 17 kuanzia saa sita usiku mpaka saa31.59 asubuhi. Wadau hii imekaaje? Kweli tukeshe kwenye internet Usiku kucha?
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vodacom mlichonifanyia sio sawa. Nilikuwa na 142,000 tarehe 1 April asubuhi. Nikajiunga na red relax ya elfu 50. Leo nimemuunga rafiki bundle la 2500 nacheki balance nakuta 40,000.

Nikapiga call centre wamenambia niliweka la kujirudia. Sijawahi hata siku moja kuweka la kujirudia ina maana ya kwamba mmeniibia elfu 50.

Tafadhali nahitaji kurudishiwa elfu 50 yangu Mchukue hilo bando lenu mliloliweka bila idhini yangu. Huu ni uwizi wa kimachomacho.

Cha kuchekesha mnaniambia kifurushi cha kujirudia kimeungwa saa nne asubuhi. Wakati siku zote mimi kujiunga mwenyewe saa 12 asubuhi haijawahi kufika saa nne ili kuepuka hela kuisha na niweze kuwasiliana. Rudisheni elfu 50 yangu acheni uwizi
Duh majamaa majiz nahama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi jana nimeweka vocha yangu mezani....
Naamka asubuhi wamepita nayo....
Na niwao kbsa, hana nyayo zinaonesha ni voda.
 
Sio kweli mimi kawaida sijiungi saa nne asubuhi na haitawahi kutokea nikajiunga saa nne asubuhi. Wao wanasema saa nne asubuhi ndo renewal imepita wakati kwa ufahamu wangu muda renewal inaitwa ndo muda ule uke uliojiunga mara ya mwisho.

Vodacomni matapeli wa kimataifa sio kwa kuniibia huko 50k kwa usawa huu
Hiyo typing error ni 5G

"......Inaitwa ndo muda ule uke uliojiunga mara ya mwisho."

Ila pole mkuu hawa watu ni hatari. Wanatakiwa kujitathmini waone kama bado wanafaa kua watoa huduma.

2020
 
Vodacom nilikuwa nawatetea kiaina nikidhani wana uafadhali ila na mimi yameanza kunikumba sasa. Kiukweli malaika au ndiyo tuseme mashetani ya mitandao yameshawasili yanafanya kazi yake kweli kweli. Hakuna uafadhali kokote kule.
 
Back
Top Bottom