Vodacom Premier League: Yanga yaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,206
103,778
Matokeo: Yanga 1-0 Biashara

Goli pekee lilofungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burkina Faso, Yacouba Sogne lilitosha kuipa ushindi vinara wa ligi Yanga dhidi ya timu ya Biashara ya kutoka Mara.

Uwanja wa taifa leo ni Utopolo na Biashara Utd ya Musoma.

Saa 1 usiku kitanuka. Utopolo itatoboa leo,au ni maumivu yanaendelea?

174398302_316027089888889_2132185446004840486_n.jpg
 
Uwanja wa taifa leo ni Utopolo na Biashara Utd ya Musoma.

Saa 1 usiku kitanuka. Utopolo itatoboa leo,au ni maumivu yanaendelea?
Nyie simba acheni mpira wa kichawi
Yanga tuna kikosi kizuri shida ni huyo babu mliye naye siku hizi alivyoamuliwa awafunge kichawi straikers wetu wote wawe wazito kufunga
Kisa eti hampendi tubebe kikombe/tuongoze ligi
Ukweli ndio huo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ligi kuu Tanzania bara itaeendelea tena leo ambapo mechi kubwa na ya kutazamwa ni kati ya Young Africans na Biashara united

Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa wanaongoza ligi wakiwa na point 51 point 11 mbele ya biashara waliopo nafasi ya nne wakiwa na point 40

Ikumbukwe mara ya mwisho kukutana Yanga walitoka na ushindi wa 1 kwa sifuri goli lililofungwa na mshambuliaji hatari wa kigeni kutoka Ghana Michael Sarpong katika dk ya 68 ya mchezo huo uliopigwa 31/10/2020

Mechi tano za mwisho Yanga kashinda 1 kapoteza 1 na droo 3 wakati biashara kashinda 2 kadroo 2 na kupoteza 1.

Ni mechi muhim kwa Yanga ambao inabidi washinde ili wajikite kileleni kwan sare au kupoteza kutampa nafasi Mtani wake Simba ambaye anahitaji point 3 ili kwenda kileleni na ana mechi kesho dhidi ya mwadui,ikumbukwe simba anazihitaji point 3 za mwadui kwani toka msimu huu kuanza hajawahi kuongoza ligi.

Mchezo utapigwa saa moja kamili jioni

Kaa nami kuanzia sasa nikuletee uchambuzi wa kina na matangazo mubashara ya mchezo huu


NB; KILA LA KHERI WATANI WANGU WA JADI KWANI MKISHINDWA KUPATA POINT 3 LEO KESHO NAWAKIKISHIA TUTAMFUNGA MWADUI NA KUPOTEZA MATUMAINI YENU RASMI YA KUCHUKUA UBINGWA
 
Nawatakia kila la kheri Biashara UTD, wapate ushindi ili nao wakaiwakilishe nchi kimataifa mwakani.
 
Back
Top Bottom