Vodacom na wizi wa kifurushi cha siku: Hayatimii masaa 24, hata ukijiunga saa 11:00 jioni ikifika saa 10:59 jioni ya siku hiyohiyo kifurushi kinaisha

markbusega

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
826
846
Kwa kweli kwa kipindi kirefu zaidi ya miaka 2 hii laini ilibaki ya huduma ya MPESA, nilikuwa natumia Halotel, Hlotel walipoharibu kwenye spidi ya data, nikaona nijaribu Voda. Kinachofanya niandike uzi huu ni jinsi huduma zao zilivyo.

Kwanza kabla ya kujiunga na kifurushi cha siku hawasemi kabla kwamba kifurushi cha siku kinaishia saa 10 jioni, pili hata kama wangesema kabla, siku mzima in a saa 24. Iweje siku yao haieleweki ina masaa mangapi?

Pili, hata data unazonunua unashindwa kujua zimeishaje, maana ukijiunga kifurushi cha siku ndani ya dakika 5 unaambiwa kimeisha.
Sijui nani wakutusaidia!

Naomba msaada ni mtandao upi unaunafuu na wenye huduma ya kuridhisha.

Screenshot_20210209-094045.png
 
Nadhani kuna shida kubwa hata MPESA inasumbua sana natumai watatulipa fidia.
 
Empesa nilikua nina ka elfu 23 nikauliza inaweza toka ngapi? Wakasema 20 du nipo nitoe inagoma ikabid hela nihamishie kwenye akaunt yangu ya benk ndio nilitoa 22500
 
Wewe ndo unakosea kununua kifurushi.

Kifurushi cha Bonge la Bando huwa kina fanya kazi kuanzia saa 5 usiku hadi kesho yake saa 10 na dakika 59.

Kuanzia saa 11 kamili hadi saa 4 na dakika 59 usiku hakifanyi kazi ndo maana unapewa MB nyingi sababu ya hizo limitations.

Mfano ukinunua sasa hivi basi kitafanya kazi hadi kesho yake muda kama huu japokua ikifika jioni ya saa 11 unawekwa mapumziko mpaka saa 5 usiku ndo kinaendelea.

Msome masharti na vigezo kabla ya kununua vifurushi.
 
Wewe ndo unakosea kununua kifurushi..
Hayo masharti wewe umeyapata wapi? Au yaliwahi kutangazwa kwenye TV au radio Mimi niliyakosa? Masharti waliyotoa nimeyaweka kwenye screen short hapo, au mengine yakowapi?
 
Hayo masharti wewe umeyapata wapi? Au yaliwahi kutangazwa kwenye TV au radio Mimi niliyakosa? Masharti waliyotoa nimeyaweka kwenye screen short hapo, au mengine yakowapi?
Mkuu kwani haya masharti yalioandikwa hapa hayaeleweki mpaka utoe ushuhuda wa uongo?

Screenshot_20210209-105354_1.jpg
 
Hayo masharti wewe umeyapata wapi? Au yaliwahi kutangazwa kwenye TV au radio Mimi niliyakosa? Masharti waliyotoa nimeyaweka kwenye screen short hapo, au mengine yakowapi?
Nilijaribu tu kukuelewesha nikidhani utaelewa.

Mie naendelea kuchapa kazi maana mie pia ni mtumiaji voda na sijawahi kuibiwa vifurushi.

Angalia screenshot hii

Screenshot_20210209-105933.jpg
 
Hakuna mtandao mtamu kwa Internet kama vodacom,jimixie bundle ya Internet saafi kabisa....... IGB ya voda naangalia mechi 3 za dk 90,IGB Airtel ukimaliza dk 20 bahati........
 
Nadhani kuna shida kubwa hata MPESA inasumbua sana natumai watatulipa fidia.

Nimepiga simu wakanisikiliza wakasema atizo langu litashughulikiwa masaa 96 nikatumiwa na msg ya reference ya cal to be worked on, masaa 96 yamepita nimepokea msg kwamba tatizo lako liko solved, nimechek tatizo bado liko pale pale, yan najiuliza hii call haijafanyiwa kazi sababu gani ?

Na hizi msg za kustart call na kuend call ni automatic nini ? manake wasituchanganye hata sisi tunaijui hii industry ya technology aisee...mpesa mpaka leo inayeyusha
 
Back
Top Bottom