Asubuhi ya leo tarehe 29.1.2020 nilienda kutoa fedha kwenye kibanda cha M-Pesa. Nilifuata taratibu zote na nikaelezwa kuwa taratibu zimekamilika. Nilisubiri ili nipate ujumbe wa kutoa fedha bila mafanikio. Nilikaa pale kwa muda wa saa moja bila mafanikio na hivyo ikabidi niondoke.
Usiku huu saa 4.15 usiku tarehe 29.1.2020 ndipo nimepata ujumbe unaothibitishwa kuwa nipewe fedha nilizofanyia muamala asubuhi ya tarehe 29.1.2020. Bahati nzuri pale nilipofanyia taratibu za kutolea fedha wananifahamu.
Swali la kujiuliza, kama ningekuwa safarini mfano Sikonge halafu ninaenda Mbeya hizi fedha zangu ningezipataje?. Ninafikiria kwenda Mahakamani ili nidai haki zangu kwa kitendo mlichonifanyia leo.
Badilikeni.