Vodacom wamevujisha taarifa zangu(?) - Kuweni makini na matumizi yenu ya Simu

Status
Not open for further replies.

hidemyid2019

Member
Oct 6, 2019
17
7
Kwanza kabisa naomba kuwasalimu wote,

Baada ya hapo kama kichwa cha uzi kinavyojieleza naomba kueleza jinsi ilivyokuwa hadi mimi kufikia hatua ya kusema kuwa VodaCom wamevujisha taarifa zangu za mawasiliano

Leo majira ya saa nane mchana, niliwasiliana na mwenye nyumba wangu kuhusu tatizo la shoti ya umeme hapa nyumbani, kwanza nilipigia simu hakupokea, nikajua huenda amebanwa na shughuli zingine hivyo nikamtumia SMS ili atakapoiona anitafute, katika sms hiyo nilieleza kuhusu tatizo lililopo.

Baada ya kama dakika 10-15, nikapokea simu (naomba namba iliyonipigia niihifadhi) huyo aliyenipigia akanijulisha kuwa yeye ni fundi umeme ameagizwa aje kutatua tatizo lililopo hapa nyumbani, kwa hiyo nikamwambia sawa nitamsubiri, na hivyo akanihakiishia kufika hapa nyumbani baada ya muda mfupi, lakini ikabidi nimtafute mwenye nyumba kuthibitisha taarifa hizo maana sikuweza kuaminin kama mwenye nyumba amewasiliana na fundi moja kwa moja bila kunipigia mimi nimweleze hali ya tatizo,

Sasa baada ya kuwasiliana na mwenye nyumba akakataa kuwa yeye hajaongea na mtu yeyote kuhusu suala la umeme zaidi ya kupokea sms ambayo mimi nimemtumia, lakini pia mimi sikuwasiliana na mtu yeyote zaidi yake kuhusu suala la umeme lililotokea nyumbani.

Hivyo moja kwa moja nikapata wasiwasi kuwa mawasiliano hayo yamevujishwa na mtandao wa simu ninaotumia (VODACOM), baada ya hapo nikapiga simu huduma kwa wateja kuwaeleza kuhusu malalamiko yangu hayo hata hivyo walichoweza kunijibu hakikuwa na mashiko, kwa kuwa alinijibu tuu kwa kifupi kuwa wao hawana uwezo wa kuona taarifa za mtumiaji wa mtandao wao

Lakini pia kama si VODA waliovujisha mawasiliano haya basi miundombinu yao haina uwezo wa kuzuia wadukuzi wa taarifa za wateja

pia, nikapata wasiwasi mkubwa kuhusu uvujaji wa taarifa zetu watumiaji wa mitandao, kwa kuwa ikiwa taarifa yangu ndogo kama hiyo imevuja, najiuliza swali Je, ni watu wangapi wametapeliwa kwa sababu hii, ni watu wangapi wamevamiwa kwa kuvuja kwa taarifa zao za safari, fedha, biashara n.k,

Tutawezaje kuwa salama kama mitandao ya simu inaruhusu mianya ya taarifa za watumiaji kuvuja na hakuna anayesema, wote tunajua kuwa dunia ya sasa inaongozwa na taarifa/data na kama tutaacha tabia hii iendelee hatuwezi kuwa salama VODACOM BADILIKENI
 
Kwanza kabisa naomba kuwasalimu wote,

Baada ya hapo kama kichwa cha uzi kinavyojieleza naomba kueleza jinsi ilivyokuwa hadi mimi kufikia hatua ya kusema kuwa VodaCom wamevujisha taarifa zangu za mawasiliano

Leo majira ya saa nane mchana, niliwasiliana na mwenye nyumba wangu kuhusu tatizo la shoti ya umeme hapa nyumbani, kwanza nilipigia simu hakupokea, nikajua huenda amebanwa na shughuli zingine hivyo nikamtumia SMS ili atakapoiona anitafute, katika sms hiyo nilieleza kuhusu tatizo lililopo.

Baada ya kama dakika 10-15, nikapokea simu (naomba namba iliyonipigia niihifadhi) huyo aliyenipigia akanijulisha kuwa yeye ni fundi umeme ameagizwa aje kutatua tatizo lililopo hapa nyumbani, kwa hiyo nikamwambia sawa nitamsubiri, na hivyo akanihakiishia kufika hapa nyumbani baada ya muda mfupi, lakini ikabidi nimtafute mwenye nyumba kuthibitisha taarifa hizo maana sikuweza kuaminin kama mwenye nyumba amewasiliana na fundi moja kwa moja bila kunipigia mimi nimweleze hali ya tatizo,

Sasa baada ya kuwasiliana na mwenye nyumba akakataa kuwa yeye hajaongea na mtu yeyote kuhusu suala la umeme zaidi ya kupokea sms ambayo mimi nimemtumia, lakini pia mimi sikuwasiliana na mtu yeyote zaidi yake kuhusu suala la umeme lililotokea nyumbani.

Hivyo moja kwa moja nikapata kujua kuwa mawasiliano hayo yamevujishwa na mtandao wa simu ninaotumia (VODACOM), baada ya hapo nikapiga simu huduma kwa wateja kuwaeleza kuhusu malalamiko yangu hayo hata hivyo walichoweza kunijibu hakikuwa na mashiko, kwa kuwa alinijibu tuu kwa kifupi kuwa wao hawana uwezo wa kuona taarifa za mtumiaji wa mtandao wao

hadi hapa nikapata wasiwasi mkubwa kuhusu uvujishwaji wa taarifa zetu watumiaji wa mtandao huu, kwa kuwa ikiwa taarifa yangu ndogo kama hiyo wamevujisha, najiuliza swali Je, ni watu wangapi wametapeliwa kwa sababu ya tabia hii, ni watu wangapi wamevamiwa kwa kuvujishwa kwa taarifa zao za safari, fedha, biashara n.k,

Tutawezaje kuwa salama kama mitandao ya simu inavujisha taarifa za watumiaji na hakuna anayesema, wote tunajua kuwa dunia ya sasa inaongozwa na taarifa/data na kama tutaacha tabia hii iendelee hatuwezi kuwa salama VODACOM BADILIKENI
Pole ...iwe kweli au sio kweli ila nakampuni ya simu yameajiri kwenye customer care vijamaa very incompetent upstairs, huwa viatoa majibu ya kipuuzi sana kwa issue za msingi kibaya zaidi eti kanamaliza kwa kukuambia "je una tatizo lingine".....hata kama beio cheap labour ila vinauzi zana!
 
Customer care ya tigo hutajuta mkuu sio hao sijui wanaokota mabaamedi?
 
anasema amepewa na mwenye nyumba, lakini mwenye nyumba anasema hajampa taarifa mtu yeyote, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kama sio voda waliovujisha taarifa hizi moja kwa moja basi mifumo yao ya mawasiliano nidhaifu kiasi kwamba inaweza kuingiliwa kirahisi
Yeye fundi anadai amepewa mawasiliano yako na nani? Tuanzie hapo.

Otherwise sioni faida yoyote kwa vodacom tanzania kwa kukutafutia wewe fundi maana wao sio madalali.
 
Je umejaribu jiuliza je kama fundi kaona text ya bossy wako akaamua kujiongeza kufata pesa?.

Je yawezekana fundi anaijua nyumba kila tarehe fulani inapiga shoti au inaanza sumbua?
 
Status
Not open for further replies.
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom