Vodacom, jamaani Vodacom

mtuwatu

Member
Oct 21, 2009
95
2
Kuna utata wa ajabu sana unaonishangaza hadi leo tangu mwanzo wa mwezi,hawa jamaa wa voda nimekua nao mwaka 5 sasa lakini wamenifanyia mambo ya kushangaza sana - kila ninaposafiri kwenda nchi nyingine kama Dubai napata vema mtandao na natumia salio vizuri kwa service provider wa huko (DU),SA nimetumia vodaSA bila tatizo na nchi zingine za jirani hawana tatizo sana! Mwaka jana niliondoka na voda hiyo kwenda USA nilipokea simu baada ya kuwa nimebond na at&t network provider mkubwa tu wa huko na matumizi hayakuwa mabaya kivilee!
Chakushangaza na bado nawashangaa hawa wafanyabiashara wakubwa ni pale ambapo wanakata hela nyingi sana mtu unapokua nchi za mbali ila hali katika matangazo yao mengi ni kwamba unaweza kupiga simu UK,USA,CANADA na kwingineko kwa 350/=tsh kwa dak. Juzi nimepiga kwenye simu yangu ya hapa hap US ya at&t na sikuipokea maana nilikua hapo hapo afu ikaingia kwenye automatic receiving maching ya voicemail niliposhtukia hivyo nikakata simu maana hamna haja ya kuacha ujumbe ili hali simu zote ni zangu. Ila sikuamini macho yangu nilipoangalia salio na kukuta wamekata 2,566/=tsh kwa sekunde mbilo (0.02). Niliamua kuwapigia network provider wangu wa hapa at&t wakaniambia wao wana mkataba rafiki na kampuni nyingi sana duniani na wao hawahusiki na account ya mteja wa kampuni rafiki kama ilivyo voda maana hata hawajui hata rate ya shilling na $ hivyo provider wangu ndo anahusika na makato yangu - hebu nisaidieni huu ni ungwana jamaani kwa hali hii ilivyo tight mtu anakula 2,566 kwa sekunde 2!!!
 
Mmeshaambiwa Voda mnawatajirisha familia ya Kigogo wa CCM.

Kama huamini, basi subiri wakukate zaidi. Ila unafahamu tena, mtu unapandisha chart ukisema uko Voda.

Pole sana sana. Ila kumbuka mwimbaji wa Zamani wa Vijana Jazz aitwaye Maneti aliimba "umaarufu umeniponza." Mambo ya ukubwa ndiyo hayo.
 
Duh pole mzee,
Kwa kawaida makampuni yote makubwa ya simu yanatengeneza mazingira ya ukiritiba (monopoly) ya kuwabana wateja watulie kwenye huduma zao hata kama ni mbaya au ghali kwa utaratibu wa kutoza gharama zaidi pale unapopiga nje ya mtandao wao, ni kama "penalization rule" (dont even trust roming!). Hii ipo hata kwenye "big supermarkets", Banks nk nk. Ukisikia kuna punguzo/ promosheni hata kwenye bia usiingie kichwa kichwa bana, no free lunch mzee!.

Mfumo huu unaumiza zaidi kwa makampuni ya simu ya ulaya kwa wateja wa huduma za malipo kadiri unavyotumia (pay as you go) pale unapiga kutoka nje ya mtandao wako kwa mfano T-Mobile kwenda Vodaphone au Orange, kwenda O2 nk nk, unaweza kukuta salio katika simu ni kama umepiga mbinguni au kwa kaunta ya polisi station ambapo simu upokelewa kama "radio calls" ( ova...ova...unanipata....!!! ova...)!...

Hakuna "uniform tariffs bana"...kama Tigo ingekuwa ya kimataifa na hizo promosheni zake ya sijui kama ingekufaa...longa longa intenacionale...express yourself.
 
Du! mi nilijua Bongo tu ndo mawasiliano anasa kumbe na huko?hawa jamaa wanajua wanachokifanya,hizo promosheni,offer sijui Extreme hakuna kitu wanachezea psychology zetu tu.Provider wangu juzi juzi kaintroduce ka extreme ka nusu ya jero-ka walalahoi! nikiwa mmoja wao nikafuata maelekezo nijiunge,siku ya kwanza ilikuwa saa1 asubuhi nikajibiwa nafasi zimejaa,siku ya pili nikawahi kidogo saa 12 asubuhi jibu lile,siku ya tatu baada ya game ya Arsenal na Fc.Porto saa 6.30 usiku(Gunners te tete teh!) nikaiweka,jibu nafasi zimejaa nikajiuliza hizo nafasi ni kwa watu wangapi?......wizi mtupu! So tuendelee kuumia tu cause hata wa kuweka mambo sawa ndo hao wanaenda kwenye hizo kampuni kuomba hela za kampeni...nchi ishauzwa hii!
 
Ndo makampuni yetu hayo best. Kotekote ni wizi tu Hapa Kenya mwaka jana tu sms kwa voda ilikuwa bei safi kama Bongo lakini sijui ilikuwaje manake thubutu kusms kwa voda utakoma, achilia mbali kupiga cm utazimia. Me nkitaka kuchat na yeyote home namhamishia salio kidogo anipigie hapo ndo inakuwa safi. Kumbuka haya makampuni pamoja na kwamba yanatoa huduma bado mengi ni ya kuwanyonya wanyonge tu! Pole best!
 
Hao Voda niwezi tu. Tigo ni ya kimataifa pia, Iko huku Majuu na inafanya kazi vizuri sana na kwa unafuu mkubwa.
Ila ni ukweli kwamba roaming charges si mchezo. Tz wanauzi sana, viwango vya simu vinavyotozwa huko ni vyajuu sana ukilinganisha na huku kwa wenzetu. Utafikiri sisi Tz ni matajiri kuliko wote.
 
VODA yupo RA kama team leader halafu kawaweka wachinjaji wenzake makini kutoka chama tawala. Kama ujuavyo RA kwa deal chafu hajambo hivyo nakushauri hama na usiruhusu mtu wa familia yako kujiunga na VODA mnapeleka pesa KUZIMU nakwambia
 
Hao Voda niwezi tu. Tigo ni ya kimataifa pia, Iko huku Majuu na inafanya kazi vizuri sana na kwa unafuu mkubwa.
Ila ni ukweli kwamba roaming charges si mchezo. Tz wanauzi sana, viwango vya simu vinavyotozwa huko ni vyajuu sana ukilinganisha na huku kwa wenzetu. Utafikiri sisi Tz ni matajiri kuliko wote.

Kwahiyo unanishauri nitumie line ya tigo?maanake nipo disipareti kinoma!!!
 
Kuna utata wa ajabu sana unaonishangaza hadi leo tangu mwanzo wa mwezi,hawa jamaa wa voda nimekua nao mwaka 5 sasa lakini wamenifanyia mambo ya kushangaza sana - kila ninaposafiri kwenda nchi nyingine kama Dubai napata vema mtandao na natumia salio vizuri kwa service provider wa huko (DU),SA nimetumia vodaSA bila tatizo na nchi zingine za jirani hawana tatizo sana! Mwaka jana niliondoka na voda hiyo kwenda USA nilipokea simu baada ya kuwa nimebond na at&t network provider mkubwa tu wa huko na matumizi hayakuwa mabaya kivilee!
Chakushangaza na bado nawashangaa hawa wafanyabiashara wakubwa ni pale ambapo wanakata hela nyingi sana mtu unapokua nchi za mbali ila hali katika matangazo yao mengi ni kwamba unaweza kupiga simu UK,USA,CANADA na kwingineko kwa 350/=tsh kwa dak. Juzi nimepiga kwenye simu yangu ya hapa hap US ya at&t na sikuipokea maana nilikua hapo hapo afu ikaingia kwenye automatic receiving maching ya voicemail niliposhtukia hivyo nikakata simu maana hamna haja ya kuacha ujumbe ili hali simu zote ni zangu. Ila sikuamini macho yangu nilipoangalia salio na kukuta wamekata 2,566/=tsh kwa sekunde mbilo (0.02). Niliamua kuwapigia network provider wangu wa hapa at&t wakaniambia wao wana mkataba rafiki na kampuni nyingi sana duniani na wao hawahusiki na account ya mteja wa kampuni rafiki kama ilivyo voda maana hata hawajui hata rate ya shilling na $ hivyo provider wangu ndo anahusika na makato yangu - hebu nisaidieni huu ni ungwana jamaani kwa hali hii ilivyo tight mtu anakula 2,566 kwa sekunde 2!!!

Pole sana ndugu yangu ila kama nimekuelewa sawasawa ni kwamba jamaa wamekwambia unaweza piga simu US kwa Tsh 350.00 lakini sijaona sehemu umeandika kwamba unaweza piga TZ kutoka US kwa bei hiyo hata kama unazo simu zote mbili mbele yako as long as moja ni namba ya TZ Roaming lazima itakukula. Halafu, kumbuka kampuni nyingi unapopiga international wanaround minutes unazotumia kwa 3 minutes incremental inategemea na kampuni. Tafuta Duka la phone Card ndo jibu la kupiga simu bongo tokea US la sivyo utafirisika.
 
Hizi kadi ziishakua za uzushi,hizi african king,the leon,king africa, east africa phn kadi sijui nini nini hizi we acha tu ndug siku hizi wamekuwa wahuni ajabu na wao maanake ya$5 unapata dakika 21.
Sasa hiyo na ku roam ipi itakua afadhali!!?
 
Kaburu yuko kazini , Anakusanya faida kwa kuwatumia wa-Tz wenyewe kwa wenyewe, Hapo hakuna mchezo Kazi ni Kazi, Akili mu kichwa.
 
Mnaichukia voda au safu ya uongozi? Iacheni voda ipumue sasa. Duh!

Kweli mkuu,
Kama ni wizi makumpuni karibu yote ni wezi tu. Mobitel (now tigo) walipokuja ilikuwa hata ukipigiwa simu ukipokea na wewe unakatwa pesa, yaani wote mpigaji na mpigiwa mnalipishwa. Mpaka Tritel (no longer in operation) walipokuja ushindani ukaanza ndo wakaacha huo wizi. Pia inasemekana kuna vigogo wa -kiTZ humo wanashare zao. Zain ndo usiseme, kila mara wanabadili majina na kuuiza kampuni kwa mtu mwingine lengo ni kukwepa kulipa kodi. Pia wameiibia vya kutosha TTCL na kutaka kuiua kabisa wakishirikiana na viongozi wetu wezi akiwemo Mwandosya et al enzi zile akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi. Siijuwi vizuri Zantel.
 
Nina laini ya voda lakini siitumii kwasababu mtandao wao unasumbua haswa muda wa chekatime na gharama zao sio user friendly. N
 
Poleni sana mnao endelea kuwaneemesha mafisadi wa VODA si walala hoi tunaextrimika na tiGo.
 
Back
Top Bottom