Vodacom, compensation hii ya bando ni kwa kutuona je?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,180
36,177
1. Kwamba huduma zenu ni kwa muda na kwa MB za bando?


2. Kwamba bando hu expire kwa siku au MB kuisha kutegemea kipi kinakuja mapema?

IMG_20240517_064406.jpg


3. Kwamba mtandao umesua sua kwa takribani wiki nzima, ila nyie fidia yenu ni kwa masaa 24 tu, tena kuanzia usiku wa manane?

4. Hivi ni kwa kutuona je enyi ndugu?

5. Kwamba hamuoni taabu kuuthibitisha usemi wa nabii Issa kuhusiana na ugumu kwa tajiri kuingia mbinguni?

6. Kwa hakika uthibitisho wenu ni wa matendo!
 
Inaonekana wamerefund kutokana na kifurushi ulichonunua siku hizo za changamoto ya internet.

Kama ulinunua cha siku unapewa hivyo hivyo, kwa wiki hivyo hivyo.
 

Attachments

  • C40ED069-54C0-44D3-9C6C-28C6799FE676.jpeg
    C40ED069-54C0-44D3-9C6C-28C6799FE676.jpeg
    90.4 KB · Views: 1
Mimi nimepewa 4GB. Inawezekana wanatoa bundle kwa kulingana na utumiaji na uwekaji wa bundle kwenye Simu. Sasa kama jamaa anatumia Mb 35 za tuzo kwa wiki anataka apewe GB 80? Wanatoa kulingana na unavyotumia na kujiunga.
Umepewa GB 4 ndani ya Saa 24 unajiona mjanja mwisho unakuwa huna kazi nazo unaishia kuangalia chonda ili kukimbizana na muda.
 
Back
Top Bottom