Vodacom acheni wizi wa rejareja

Board member

Senior Member
Sep 24, 2021
103
239
Habari.

Imekua mchezo wenu uliozoeleka siku hizi. Kila nikiweka airtime kabla sijaunga kifurushi lazima mukate kiasi, hali hii inafanya nishindwe kujiunga na package niliyokusudia hadi niongeze airtime nyingine.

Nikiwapigia mnasema mara nimejiunga na huduma gani sijui, wakati mimi sijawahi kujiunga na huduma yoyote kati ya huduma zenu za kipuuzi ambazo kutwa hamuachi kunihamasisha kujiunga nazo.

Tabia hii inakera sana coz inaniharibia bajeti zangu hadi nafikiria kuhama kwenye mtandao wenu.

Natoa wito,, acheni huu utapeli!!
 
Habari.

Imekua mchezo wenu uliozoeleka siku hizi. Kila nikiweka airtime kabla sijaunga kifurushi lazima mukate kiasi, hali hii inafanya nishindwe kujiunga na package niliyokusudia hadi niongeze airtime nyingine. Nikiwapigia mnasema mara nimejiunga na huduma gani sijui,, wakati mimi sijawahi kujiunga na huduma yoyote kati ya huduma zenu za kipuuzi ambazo kutwa hamuachi kunihamasisha kujiunga nazo.

Tabia hii inakera sana coz inaniharibia bajeti zangu hadi nafikiria kuhama kwenye mtandao wenu.

Natoa wito,, acheni huu utapeli!!
Yaani bora nawewe umelisemea Mimi sahizi siwezi nunua vocha ya kukwangua wala airtime yakawaida nikiweka tu unakuta mia hakuna sasa nimeweka airtime elf 2000 mnakata mia 100 nitaiongezea wapi? Voda wanakera kila nikipiga eti sijui umejiunga nini mara labda nipige tafu mie nimejiunga lini? Nikipata muda nitawafuata hapo hapo kwao waniambie, mpawa nimeacha kuweka ukiweka tu ukija kuzitoa zimepungua wapuuzi kabisa
 
Mimi nimesitisha matumizi bila bando tangu waanzishe hii, lakini recently kama week hivi naona wanakata shilling 20 mara 28, watu wa sales ndio mnatafuta pesa ya sikukuu kinguvu?
 
Jaribu kuangalia kama umejiunga na huduma za michezo kama tikisa, soka au tusua mapene ...

Piga *149*83#
 
Nashukuru kwa michango yenu. Ila ni kwamba sijawahi kuruhusu matumizi bila bando, sijawahi kujiunga na huduma yoyote, na simu yangu natumia mwenyewe. Sina mke, sina mtoto, wala sina mtu wa karibu kudhan labda kajiunga na huduma bila ufahamu wangu. Simu yangu natumia peke yangu. SIJAWAHI KUBONYEZA BUTTON YOYOTE KUKUBALI HUDUMA YOYOTE. Yaani kwangu mimi natafsiri kuwa huu ni wizi tu, sina neno zuri la kuita hiki kinachonitokea.
 
Back
Top Bottom