Gushleviv
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 3,437
- 5,146
Habari zenu Wakuu,
Mimi ni mtumiaji wa Vodacom. Hivi karibuni nimekuwa nikikutana na hali ya salio langu kukatwa kiasi cha Tsh.100 kila baada ya mida flani bila ya ridhaa yangu.
Nikiwapigia Vodacom wananiambia kuwa nakatwa salio sababu nimejisajili kwenye huduma ya "Mdundo". Na zaidi sasa naletewa hadi msg kuomesha kwamba nimejisajili na hiyo huduma.
Naomba kueleweshwa kama kuna yoyote mwenye uelewa juu ya hili suala.
Kwa mtazamo wangu hadi sasa naona kama ni wizi kumsajili mtu kwenye huduma bila ya ridhaa yake na bila kutoa elimu juu ya huduma hiyo.
Isije kuwa ujinga wa wengi unatumika kama fursa kwa wezi wachache.
Iwapo nitagundua kuwa nimeibiwa basi nitawafikisha mahakamani.
Asanteni.