VODACOM Tanzania wanaiba pesa kwenye line za simu

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,086
34,000
Habarini Wadau.

Mimi ni Mtumiaaji wa line mbili za simu ila kwa mwaka huu mzima tangu uanze nimekuwa nikitumia line ya Vodacom kujiunga na vifurushi ila nikikuwa nikiambiwa Mara kadhaa kuwa Vodacom ni wezi wa pesa za Wateja na sikukubali mpaka iliponikuta Sasa.

Kuna wakati Vodacom walikuwa wananikata 200/= kila ninapoweka Salio, kwa mfano nikiweka 1000/= linabaki 800/= au ukiweka 5000/= inabaki 4800/= hivyo inashindikana kujiunga na vifurushi ninachokitaka.

Niliwapigia Huduma kwa wateja, Dada mmoja akaniambia nimeunganishwa sijui kwenye Huduma ya SOKA LETU, wakati sikuwahi kujiunga wala kuhitaji Huduma hiyo.

Wakanikata tena baada ya wiki 2 nikawauliza wakaniambia nimeunganishwa na Huduma ya Music ilihali sikuwahi kujiunga wala kutaka hizo Huduma.

Sasa juzi nimeweka kifurushi cha 2000/= na sikutumia kabisa line ya voda sikuhiyo, siku inayofuata nimetaka kujiunga nikaambiwa Salio halitoshi. Kutizama salio nakuta 1800/= kidogo niwapigie kuwatukana.

VODACOM ninyi ni wezi wa pesa za wateja wenu.

Acheni wizi na uhuni.
 
Jitahidi kutojiunga huduma yeyote hata ya Bure maana huwa zinakua za Bure kwa siku tatu baadae wanaanza kukata usipojitoa. Lakini wizi wao kwenye data aisee Ile meseji umefikia MWISHO wa matumizi huwa inawahi balaa mpaka unashangaa zimeishaje. Voda ni majizi
 
Siyo wezi , hayo ni majambazi.... Na ukipiga simu yanakwambia eti ulijiunga na muito Kwa mpigaji, mala sijui ulijiunga na hadithi, ukiyaambia hujawahi kufanya hivyo yanasema labda ulibonyeza simu Kwa bahati mbaya au ulimpa simu mtu mwingine akajiunga, mashenzi majambazi makubwa
 
voda wana wateja karibia mil 20, kipi cha maana sana mpaka wawe wanaangalia line yako ya simu peke yake? hawakujui ata, huenda kuna baadhi ya huduma unajiunga ama ni issue za system tu sio kurusha shtuka kubwa ivo kama wanakaa kusubiri uweke 2000
 
Habarini Wadau.

Mimi ni Mtumiaaji wa line mbili za simu ila kwa mwaka huu mzima tangu uanze nimekuwa nikitumia line ya Vodacom kujiunga na vifurushi ila nikikuwa nikiambiwa Mara kadhaa kuwa Vodacom ni wezi wa pesa za Wateja na sikukubali mpaka iliponikuta Sasa.

Kuna wakati Vodacom walikuwa wananikata 200/= kila ninapoweka Salio, kwa mfano nikiweka 1000/= linabaki 800/= au ukiweka 5000/= inabaki 4800/= hivyo inashindikana kujiunga na vifurushi ninachokitaka.

Niliwapigia Huduma kwa wateja, Dada mmoja akaniambia nimeunganishwa sijui kwenye Huduma ya SOKA LETU, wakati sikuwahi kujiunga wala kuhitaji Huduma hiyo.

Wakanikata tena baada ya wiki 2 nikawauliza wakaniambia nimeunganishwa na Huduma ya Music ilihali sikuwahi kujiunga wala kutaka hizo Huduma.

Sasa juzi nimeweka vifurushi cha 2000/= na sikutumia kabisa line ya voda sikuhiyo, siku inayofuata nimetaka kujiunga nikaambiwa Salio halitoshi. Kutizama salio nakuta 1800/= kidogo niwapigie kuwatukana.

VODACOM ninyi ni wezi wa pesa za wateja wenu.

Acheni wizi na uhuni.
Kuna ukwel. Line siitumii kabisa nikiweka hela baada siku kadhaa inapotea.
 
Ukiweka 1000 ukilala ukiamka asubuhi hukuti 1000 ile ile unakuta 988 hivi,kuna vishilingi tayari wanakua wameshapiga panga,wanakua wamekuibia Tsh kadhaa
Wakifanya hivi hataa wakuchukulie Tsh 12 zidisha wateja walionao km labda 1m.utapata wamepata Tsh ngapi kwa huo ujanja ujanja.

Hawajaanza leo hayo mambo
 
Sidhani Kama wote mnastahiri kulalamika wengine ni uzembe wenu!,mtu anatumiwa mi sms huko ya offer hajasoma vizuri anajiunga kwa ku reply ama kwa kubonyeza tu alivyosikia!.
Naomba utaalamu wakujiunga nikiwa sijasoma maelekezo mkuu. Maana haiingii akilini kwamba haujasoma ujumbe halafu ujiunge, code za kujiunga unazijuaje
 
voda wana wateja karibia mil 20, kipi cha maana sana mpaka wawe wanaangalia line yako ya simu peke yake? hawakujui ata, huenda kuna baadhi ya huduma unajiunga ama ni issue za system tu sio kurusha shtuka kubwa ivo kama wanakaa kusubiri uweke 2000
Umesema ni issue za system, wao hawajawahi kukaa na kujiuliza hilo tatizo linasababishwa na nini? Kwamba wote wanaolalamika kwamba wameungwa kinyemela, hawakumbuki kwamba waliwahi kujiunga?
 
voda wana wateja karibia mil 20, kipi cha maana sana mpaka wawe wanaangalia line yako ya simu peke yake? hawakujui ata, huenda kuna baadhi ya huduma unajiunga ama ni issue za system tu sio kurusha shtuka kubwa ivo kama wanakaa kusubiri uweke 2000
Unaamini watu ni wajinga hawajui kama wamejiunga ama hapana? Kama shida ni system si wamjibu kua system ina shida badala ya kumjibu amejiunga na huduma ambazo yeye hazijui?
 
Huo wizi upo! Wanajua watanzania hawawezi kudai hizo 200, Ila VODACOM wanapiga hela ndefu!
Na hata ujaribu kujitoa ni kama option wameshaitoa ya kujitoa!

Wanakera eti ulijiunga, sijawahi kujiunga, wanalazimisha, utakuwa ulijiunga, mtu mzima nijiunge wimbo wa Zuchu ili iweje!?!

Wezi faida za mabilioni, gawio sijui wanatuibia na kujidai kuturudisha!
 
Naomba msaada wakujitoa kwenye mwito wa simu ya vodocom tafadhari, ili wasiendelee kunikata 200 yangu hao niwezi kabisa
 
Back
Top Bottom