MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Miaka ya 1980, wananchi wa Lebanon walifanya mgomo wa kutotumia simu zao kwa saa 24 dhidi ya kampuni zote za simu za mkononi zilizokuwa zikifanya biasha. Simu zilizimwa. Kampuni zilidhani ni utani. Baada ya saa 24 kukamilika, wananchi waliwasha simu zao na kukuta ujumbe mfupi lukuki, ukiwaomba radhi kwa usumbufu waliokuwa wakiupata kwa muda mrefu. Kwa uzalendo wao, HESHIMA ILIRUDI, DHARAU ZIKAKOMA.
Tukijipanga vizuri, sisi wanyonge ambao ndio wengi zaidi tunaotumia hizi simu, kuliko hao mabepari na vibaraka wao, tunaweza kufanya mgomo kama huo. Amini inawezekana. Kabla ya kufanya hivyo tunaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwaeleza dhamira yetu hiyo, kwamba tutafanya mgomo huo. Kisha inaanza kampeni ya kuwahimiza wadau wote kuzima simu zao siku itakayopangwa. Saa 24 ni sawa na kuanzia saa 6 usiku hadi 6 usiku.
Tukiwanyima mapato kwa muda huo, hasara watakayoipata, ni dhahiri watakomesha wizi wao huo na kurejesha heshima kwetu. Dawa ni kuwagomea, mitandao YOTE, sio Voda pekee. Ninamaanisha Airtel, TTCL, Vodacom, Tigo na Zantel. Sasatel siwahesabu kama mtandao, na hata Benson. Hao wana wateja wachache sana.
Je, waungwana, mnaiweza shughuli hii kazi ianze rasmi?