Voda wanataka alama za vidole vya wateja ili kuboresha usajili wa laini

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,495
2,252
Nimepokea ujumbe kutoka Voda kuwa wataanza kukusanya alama za vidole kuboresha SIM card registration. Hili sijui linatoka kwa Voda au serikalini?

Edit Kang: Post hii imekuwa edited na mods, napinga editing hiyo!!

img_20180129_120628-jpg.686739
 
!
!
Hao jamaa ni wapuuzi kweli. Wasubiri vitambulisho vya uraia vitoke halafu kama wanataka waitishe sasa usajili mpya wa kujumuisha fingure print. Sasa kila mtu akitaka hiyo fingure print ni fujo
 
muda wa kutengeneza figisu za ukwapuaji ..
ile mbiniu ya leseni haifai tena? au wamegundua wengi hatuna mandinga
 
Kwa hii sayansi na teke linalokujia watahangaika sana.

Hakuna aliyeweza kuushinda wakati.....
 
Nimepokea ujumbe kutoka Voda kuwa wataanza kukusanya alama za vidole kuboresha SIM card registration. Hili sijui linatoka kwa Voda au serikalini?
Ndugu Mteja, katika kuboresha usajili wa laini za simu, alama za vidole zitatumika kuanzia 5/2/2018. Kwa maelezo zaidi tembelea duka letu la Mlimani city
 
Ni TCRA na sio voda dah kwa kukurupuka wa TZ na ni kwa mitandao yote
 
529b4ea2f2bbb57ee866443da88374f4.jpg
Habarini.

Leo nimeona nishare nanyi jambo muhimu sana kuhusu afya ya kinywa.

Naamini sisi sote huwa tunapiga mswaki kama tunavyo elekezwa na madaktari wa kutibu magonjwa ya kinywa.

Na katika kusafisha kinywa moja ya vitu tunatumia ni miswaki imara na dawa bora ya meno. Kwa wale mlioishi miaka ya nyuma kuanzia sabini mtaungana nami juu ya ukweli kwamba kabla hata ya madawa mengine ya meno haya ya sasa kama whitedent, sensodyme, forever na nyinginezo, alikuwapo dawa moja mwamba ambaye hadi leo hanaga mpinzani wa uhakika. Huyu si mwingine bali ni dawa Colgate.


Hii dawa imekuwapo kwa vizazi ikitetea ubora wake katika kuwa na standard inayotakiwa ya dawa bora ya meno. Kwa hapa afrika, dawa hii yenye hadhi ya kimataifa na yenye soko dunia nzima inatengenezwa hapo South Afrika na kampuni ya Colgate Palmolive.

Ila nasikitika asilimia 90% ya colgate zilizopo madukani ni mzigo kutoka kwa watengenezaji fake ambao hawana kibali kamili cha kutengeneza colgate yenye ubora ule wa kimataifa. Kwa kifupi, Colgate nyingi zilizopo hapa madukani ni feki na ninasikitika sana hata sisi wateja au watumiaji wa brand hii murua tumeshindwa kuchukua hatua na kupiga vita uvamizi huu wa ubora kwa kukubali hizi sumu feki zisambae madukani bila kueleimisha uma wa watanzania juu ya ubora halisi wa Colgate original ambayo imetufanya leo hadi umri huu tuwe na meno imara ambayo hayajaharibiwa na wadudu na kutupa usalama murua ambao unatuwezesha hata kuongea na mpenzi wako mkitizamana usoni kinywa kikiwa swafi kabisa.


Naomba tuelimishane hapa kuwa kuna viashiria ambavyo huonyesha hii dawa si yenyewe.

1. Kwanza, Colgate original huwa na boksi lenye mlango ambao unaweza kufungua na kisha kuifunga yaani haujawekewa gundi.

Colgate feki ipo tofauti, boksi lake milango yake imesilibwa na gundi kabisa, ukichana ni umenunua na si ya kurudisha kwenye shelfu tena.

Nadhani wanafanya hivi ili kuzuia wale wanaoifahamu kama mimi kuibaini kabla hawajainunua. Mfano mimi nikilamba tu pale pale dukani na kuinusa naiweza kuibaini hii ni Colgate feki ila wasio zijua vema wananunua na kuwatajirisha hawa wezi wetu wanaotuuzia dawa feki.

So, kumbuka, linapokuja swala la boksi ya dawa ya Colgate, usijeukathubutu kununua yenye boksi ambalo mlango wake upo sealed na gundi na hauwezi ifungua na kuifunga na kuirejesha katika shelfu ya dukani hapo.


2. Boksi ya Colgate feki ina maelezo sawa kabisa na Colgate original ila tofauti yake ni kwamba hii feki itakosa Barcodes katika package yake.

Hii ina maana imetengenezwa na watu feki ambao hawakufanikiwa kuipitisha katika mikono safi ya watu wa procurement katika kiwanda chenyewe cha huko South Africa. Kama unabisha tafuta boksi isiyo na barcode halafu ukawalalamikie hao Colgate Palmolive kuwa bidhaa ni feki, watakapohitaji uwatumie hiyo bidhaa watagundua kuwa hiyo boksi ya Colgate haijapitia katika mikono ya maofisa ugavi wao katika hicho kiwanda na kusambazwa, maana wenzetu huwa wanazipa bidhaa zao barcode ili iwe rahisi kutrace inventory yao mara kunapotokea uharibifu wowote.

3. Alama ya ubora ya TBS. Hii huwa tunaambiwa kila uchao kuwa tusinunue bidhaa ambazo hazina hii alama....ingawa zipo ambazo huwa anafoji lakini ni chache sana na kuna udhibiti unafanyika hivi sasa katika kuzuia hii changamoto. Ukitazama boksi za Colgate feki huwa inakosa hii alama, na sababu ipo very obvious, kuwa ni bidhaa feki na hatarishi kwa usalama wa afya ya mwanadamu.

Hizi ni miongoni mwa alama chache nilizobaini na nina washauri wale watumiaji wa colgate original hebu tupige vita udhalimu huu lakini pia tuwakondeshe kwa kutokununua maana kwao hii ni biashara na sio swala la kiafya sasa tukiwakomoa watakosa soko na kutafuta bishara nyingine na kuacha upuuzi wao.

Hapa chini nitaambatanisha picha ya boksi ya Colgate feki ili muweze kutambua.
Ili iweje kama ata mademu wengi fake
Kapicha mkuu
 
halafu line usipoitumia kidogo wanakupokonya wanampa mtu mwengine, mpaka unajiuliza faida ya kusajili line ni nini? imekaa kama ni miradi ya watu wanaiba tu personal information.

bila kusahau simu unapigiwa mtu anajua jina lako na kukuanza kukuhoji maswali ya utafiti, nani ameruhusu mitandao itoe personal information zetu?
 
halafu line usipoitumia kidogo wanakupokonya wanampa mtu mwengine, mpaka unajiuliza faida ya kusajili line ni nini? imekaa kama ni miradi ya watu wanaiba tu personal information.

bila kusahau simu unapigiwa mtu anajua jina lako na kukuanza kukuhoji maswali ya utafiti, nani ameruhusu mitandao itoe personal information zetu?
ujinga
 
halafu line usipoitumia kidogo wanakupokonya wanampa mtu mwengine, mpaka unajiuliza faida ya kusajili line ni nini? imekaa kama ni miradi ya watu wanaiba tu personal information.

bila kusahau simu unapigiwa mtu anajua jina lako na kukuanza kukuhoji maswali ya utafiti, nani ameruhusu mitandao itoe personal information zetu?

Elimu ya privacy bado inahitajika sana kwetu. Personal data watu wanacheza nazo kama wanavyotaka wenyewe.
 
Elimu ya privacy bado inahitajika sana kwetu. Personal data watu wanacheza nazo kama wanavyotaka wenyewe.
Na bado hapo kuna upumbavu wa facebook free, wananyonya info zetu zote wanawapa Facebook.
Lakini hii kama ni mitandao yote basi inatoka serikalini, naona woga wa mtandao umewaingia, muda si mrefu wataanza kublock baadhi ya social networks.
 
Naona kabla ya kupinga tungeelimishwa ubaya wake ili nasi tufaham tusifate mkumbo tu kwa kuwa fulani kasema.
 
Hii nayo Kali!!!!,kwa mm naona inaweza kuw ndo mwisho wa kutumia cm.

Kwn hata usajili wnyew ulioanzishw 2009,tuliambiw kuw ungesaidia ktk kuzuia wzi,na nilipoibiwa nilitoa taarf kw mtandao husika lkn ckusaidika.

So kW hl yamkin ikaw ndo mwsho w me kutumia cm ndg wnajf.
 
Back
Top Bottom