Viwanja vya Pembamnazi-Kigamboni vimetelekezwa

Sisi vyetu havina mgogoro, vimepimwa halafu wameshirikiana na serikali za kijiji, manispaa na kila eneo

Iwe kheri juu ya hilo,Mkuu kua makini tu sababu hizo serekali za vijiji hao ndo wanaouza hvyo viwanja. Kumekua na kesi juu ya hao wanunuzi walouziwa pamoja hizo serekali za vijiji kwasababu hao wadai wamesema hilo shamba ni la urithi ambalo lina warka wake.
 
Ni mbali, na barabara kuna kipande sio nzuri sana. Kule hamna foleni. Kuna barababa upande mwingine imechongwa yenyewe hutumii lisaa, hatukupita hiyo shortcut kwasababu kulikua na wa kuwachukua njiani
Napenda kutalii sn,naweza kufunga safari kwenda mahali nisipopajua ili kwenda kurefresh mind tu

Siku moja nikapanga kwenda kutembelea buyuni,nasikia kuna beach Kali na samaki,and of course nilienda kuangalia km pananifaa Kwa makazi.Badi rafiki yangu kila nikitembea naona sifiki,hapo nishakata km dakika 50.nikafika sehemu nikauliza hapa panaitwaje nikaambiwa hapa kimbiji,huko unakoenda buyuni bado inabidi tena ukanyage mafuta,nikasema hapana Kwa kweli naishia hapa.Nikapiga lunch kimbiji Nikarudi🤣
Ila kimbiji kuna beach Kali sn,lkn ni kijijini mno,baadae utakuja kuwa mji mzuri sn
 
Kabisa mkuu, mama yangu alishawahi kununua kiwanja, baada ya mwaka mmoja aliuza mara kumi yake. Watu hua wananishangaza sana eti kwanini umenunua kiwanja mbali, sasa nikanunue mikocheni au Mwenge? ukitaka kiwanja mjini inabidi ujipange kwelikweli, ngoja mimi ninunue hivi vya nje ya mj baada ya miaka mitano nauza kiwanja kimoja kinajenga nyumba. Kikubwa hua naangalia gari ifike hadi site, umeme upo na pia kiwe kimepimwa.
True
 
Epukeni matapeli Haswa huko maeneo ya buyuni kuna shamba kubwa ambalo lina kesi tokea miaka ya 2000 hadi hii Leo.
Yaani kuna vigagula wa utapeli WA ardhi huko ogopa,
Mwenye masikio asikie, huko maeneo yamejaa migogoro!
Mmoja anazungusha ukuta mwingine anamwaga mchanga mwingine anamwaga kokoto,
Mwingine ananyanyua nyumba,

Huko mpaka Kimbiji, hizo serikali za mtaa/vijiji ni gelesha tupu! Njaa
 
Ni maeneo gani mkuu? Naomba mfano uwe kuanzia pale kituo cha panton

Kutoka pale pantoni ni mbali mkuu!
Kutoka feri pale unaenda na hii njia ya mji mwema.
Ukifika mji mwema unaacha njia ya kwenda kibada unaenda na njia ya cheka huku buyuni.
 
Nilikuwa huko juzi, kiwanja kidogo cha kutosha kujenga nyumba unapata kwa laki tatu, 300k.

Tena ukitaka unalipa kwa awamu mbili.
Halafu 2035/40 atatokea mtu hapa Dar tayari ana mvi kichwani aliisoma hii post leo ila bado atakuwa analalamika kunyanyaswa na wenye nyumba anazopanga.

Vijana akili zituamke tuendako hali inazidi kuwa mbaya.
 
Kutoka pale pantoni ni mbali mkuu!
Kutoka feri pale unaenda na hii njia ya mji mwema.
Ukifika mji mwema unaacha njia ya kwenda kibada unaenda na njia ya cheka huku buyuni.
Ok. Asante mkuu
 
Back
Top Bottom