Viwanja vya Pembamnazi-Kigamboni vimetelekezwa

Viwanja vya Pembamnazi-Kigamboni vimetelekezwa

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
919
Reaction score
599
Salama wakuu.

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Mnamo mwaka 2016 serikali iliamua kuuza viwanja Kigamboni eneo la Pembamnazi jijini Dsm. Mpaka Leo hii tarehe 2- 3- 2022 viwanja hivyo havijahudumiwa na serikali kwa kuwekewa miundombinu ikiwemo umeme, maji na kuchongwa barabara ili watu waweze kuvifikia viwanja vyao.

Huu ni mwaka wa sita sasa pamebakia kuwa ni porini. Serikali kupitia wizara ya ardhi toeni tamko rasmi kuhusu eneo la Pembamnazi maana watu wakienda wizarani kuuliza kulikoni wanapewa majibu ya ovyo yanayokatisha tamaa.

Pia watu waliuziwa viwanja hivyo bila ya kuviona. Kwa vile muuzaji ni wizara ya ardhi wananchi wakaamini hawatotapeliwa. Kumbe eneo lenyewe ni pori kubwa lisilokuwa na miundombinu yeyote.

Tunaomba waziri muhusika aende kutembelea Block 1 na Block 2 ili ajionee mwenyewe utapeli waliofanyiwa wananchi.

Pelekeni miundombinu watu wajenge, mji ukue na serikali ipate mapato kupitia kodi.
 
Nilikuwa huko juzi, kiwanja kidogo cha kutosha kujenga nyumba unapata kwa laki tatu, 300k.

Tena ukitaka unalipa kwa awamu mbili.
Kwa pori lile linavyotisha lazima viwanja viteremke bei maana hakuna uwezekano wa kujenga nyumba kule. Labda serikali ipeleke miundo mbinu mfano umeme, maji na viwanja viwekewe barabara ili magari ya vifaa vya ujenzi yaweze kupita
 
Salama wakuu. Moja kwa moja niende kwenye mada.
Mnamo mwaka 2016 serikali iliamua kuuza viwanja Kigamboni eneo la Pembamnazi jijini Dsm. Mpaka Leo hii tarehe 2- 3- 2022 viwanja hivyo havijahudumiwa na serikali kwa kuwekewa miundombinu ikiwemo umeme, maji na kuchongwa barabara ili watu waweze kuvifikia viwanja vyao. Huu ni mwaka wa sita sasa pamebakia kuwa ni porini. Serikali kupitia wizara ya ardhi toeni tamko rasmi kuhusu eneo la Pembamnazi maana watu wakienda wizarani kuuliza kulikoni wanapewa majibu ya ovyo yanayokatisha tamaa. Pia watu waliuziwa viwanja hivyo bila ya kuviona. Kwa vile muuzaji ni wizara ya ardhi wananchi wakaamini hawatotapeliwa. Kumbe eneo lenyewe ni pori kubwa lisilokuwa na miundo mbinu yeyote. Tunaomba waziri muhusika aende kutembelea Block 1 na Block 2 ili ajionee mwenyewe utapeli waliofanyiwa wananchi. Pelekeni miundombinu watu wajenge, mji ukue na serikali ipate mapato kupitia kodi.
Aisee ni kweli, serikali itoe tamko pale. Maana ni pori la nguvu, na barabara ya kuingia kule ni mbaya. Wakati wa Mvua ndio balaa. Wakati ule viliuzwa na Manispaa yaTemeke; nadhani kwa sasa itabidi Manispaa ya Kigamboni iingilie kati kuvifufua vile viwanja.
 
Salama wakuu. Moja kwa moja niende kwenye mada.

Mnamo mwaka 2016 serikali iliamua kuuza viwanja Kigamboni eneo la Pembamnazi jijini Dsm. Mpaka Leo hii tarehe 2- 3- 2022 viwanja hivyo havijahudumiwa na serikali kwa kuwekewa miundombinu ikiwemo umeme, maji na kuchongwa barabara ili watu waweze kuvifikia viwanja vyao.

Huu ni mwaka wa sita sasa pamebakia kuwa ni porini. Serikali kupitia wizara ya ardhi toeni tamko rasmi kuhusu eneo la Pembamnazi maana watu wakienda wizarani kuuliza kulikoni wanapewa majibu ya ovyo yanayokatisha tamaa.

Pia watu waliuziwa viwanja hivyo bila ya kuviona. Kwa vile muuzaji ni wizara ya ardhi wananchi wakaamini hawatotapeliwa. Kumbe eneo lenyewe ni pori kubwa lisilokuwa na miundo mbinu yeyote.

Tunaomba Waziri muhusika aende kutembelea Block 1 na Block 2 ili ajionee mwenyewe utapeli waliofanyiwa wananchi.

Pelekeni miundombinu watu wajenge, mji ukue na Serikali ipate mapato kupitia kodi.
 
Naona buyuni barabara imechongwa na pia kuna umeme, Nina kiwanja buyuni nauza 3m
Barabara inayoelekea Buyuni ni ya vumbi yenye mashimo mengi. Bado haijawekwa lami. Magari ya watu yanaharibika. Hapa panazungumzwa eneo la Pembamnazi
 
Back
Top Bottom