Viwango vya gharama daraja la Kigamboni ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Ulimbukeni wa viongozi wa Tanzania hauna kipimo. Daraja tu ni hivyo jee hizo fly-overs. Nadhani wanaona hiyo tayari ni 'luxury'
Ndiyo maana nikataka kiongozi wa Tanzania awe ameishi muda mrefu Ulaya au Marekani akifanya kazi na siyo mwanafunzi. Ulimbukeni huu ungepungua. Kumbe....hata MAGU hana afadhali kwa walalahoi!
 
Mpaka kesho nazidi kusema Tz hatuna maofisa Mipango. Waliopo, makanjanja tu. Utajengaje daraja moja tu nchini lilipiwe na wakaazi wa eneo hilo? Je, mliwashirikisha mradi huo kabla hamjaanza ujenzi? Mliwaambia kutakuja kuwa na malipo? Si mlijigamba kuwa mnawaondolea mateso? Mbona mmewaongezea mzigo? Au mnataka kuja kulitumia kama kick ya kupatia kura mtakapo kuja sema tumeondoa tozo kwa sababu chama twawala kimekaa na kuona kuwa wananchi wake wanapata shida? Je hizo flyovers nazo mtatoza? Yapo madaraja mengi tu ambayo kama shida yenu ni pesa, yangewaingizieni pesa nyingi tu. Mfano, Wami, magari mangapi yanapita hapo kwa siku? wala msiweke tozo kubwa, shs 200 tu kuvuka. Si mngejenga flyover kila mahali kuondoa msongamano?
Jipangeni upya msiwaonee wana kigamboni.
 
Hilo daraja ni alternative au permanent solution kwa usafiri kwenda satellite city? Kama ni alternative, basi mwenye uwezo, ulazima au dharura ndo apite kwa malipo yaliyopangwa.

Polepole tutazoea, ndio gharama za maendeleo na kuachana na siasa za ujamaa.
 
Daraja limegeuka na kuwa msalaba mzito kwa wananchi.
Naunga mkono hoja, hii nchi haijafikia uwezo wa watu kulipia social service, ambayo ni jukumu la serikali, serikali itafute financing ya kufidia hapo, ikiwezekana watu na magar na kila kitu kipite bure, maana hakuna namna nyingine tena.
Mbona daraja la kirumi, Mkapa na Kikwete hawalipii, kama hoja ni NSSF mbona UDOM hakuna margin kwenye Tuition fee ku compesate private element investment.
 
Sio kweli, una chuki binafsi na Yeriko.
Ni kama saa nne tu zilzopita umeleta uzi wa ''Riba za benki ni majipu makubwa sana". Nikukumbushe, Yeriko alishaleta huo uzi hapa JF kitambo tu, na ukajadiliwa. Leo wewe umeibuka nao kama vile haujawahi kujadiliwa.

Mkuu hawa watu akili zao wameweka nyuma, wanazikalia. Subiri kama ikatokea mkuu wa kaya akasema tozo hizo zipunguzwe, hawa hawa watakuja kumsifia humu ndani, lakini kwa kuwa Yericko Nyerere ndiye aliyeleta hili jambo wanaona atanenepa wakimpa credit.
 
Nadhani itafikia mahali hata lift kwenye majengo Marefu zitaanza kulipiwa na kama huna basi utazunguka kwa kutumia ngazi.

Hapa kuna Mambo mawili:

(1) Tatizo la mashirika yetu ya umma na hata viwanda ni kutoa huduma au bidhaa zake kwa bei kubwa kwa manufaa ya wachache.

Wananchi wengi wanaumia ili wachache wajilipe mishahara minono hata kwenye huduma au bidhaa muhimu na za msingi.
Hua najiuliza ni kwa nini kila kitu kinachotoka nje ni rahisi kuliko vya ndani. Inamaana huko hawataki faida. Mfano ukiagiza gari huko Japani ni bei rahisi lakini likishakanyaga Tanzania basi kodi juu utafikiri tuna viwanda vya magari tunavyovilinda.

Hii nchi thamani ya fedha ni kubwa kuliko utu wa mwanadam. Na ukishakua na serikali inayothaminisha pesa kwa kiwango cha juu kuliko utu wa mwanadam basi tegemea kuwa na watu wenye roho mbaya, wanaoombeana mabaya, wanaofurahia kuona wenzao wanapokutwa na mabaya, wanaoviziana kuangamizana, kuibiana , kuuana kwa malengo ya kupata pesa, ushirikina, madawa ya kulevia, uzinzi kwa tamaa ya wanawake kupata fedha , kwenye dini fedha, kuuziana bidhaa bandia, bidhaa zilizokwisha muda wake kuuzwa tena ili kusaka hela, madalali kila kona kuanzia serikalini, riba kubwa kwenye mabenki na kila aina ya usanii na utapeli.


(2) Wanyonge wamewekewa fumbo ili wajiongeze wenyewe.
Kama unaona kupita darajani ni gharama basi zunguka au endelea kutumia kivuko kama au upige mbizi.
Kuna watu wanye pesa za kulipa hata laki 50,000 kwenye daraja kwa siku. Nadhani hao ndio waliojengewa hilo daraja na wapo tayari kulipa kwani kwao tatizo ni foleni ya kivuko na sio pesa.
Daraja limejengwa kwa supper market. Kama ukiona huwezi kwenda mlimani city basi nenda kariakoo. Watu wamewekeza pesa zao na wamelenga watu wenye kipato cha juu kwa raha zao.




Nini kifanyike kwenye daraja la kigamboni!!!:

(1) Huduma za kivuko zilizozoeleka ziendelee kama kawaida ili pia kupunguza foleni.

(2) Bei ya kulipia daladala ipungue iwe ni sh. 1000/- kwa kila ruti au iwe 5000/- kwa siku nzima. Hii ni kuwasaidia wanyonge kwani daladala zinatoa huduma ndio maana zinapangiwa bei ya nauli na hata kuombwa kubeba walimu bure na wanafunzi nusu nauli. Hawa wanaumizwa sana na suala la mapato kuanzia sumatra n.k.

Magari madogo na ibaki kama ilivyo .

Pikipiki ipande na kufikia 1000/.
Hii itasaidia kulifanya daraja ama kivuko kuwa ni suala kuchagua. Ukiona daraja ni ghali basi panda kivuko.



ANGALIZO:-
Kama Serikali ya Magufuli ni ya watanzania wanyonge ,yaani wakulima na wafanyakazi basi huduma ya daraja iwe ni sh. Mia tano tu,500/- kwa magari yasiyozidi tani tatu na 1000/- kwa magari chini ya tani 7.
Kuanzia tani 7 kwenda juu yalipe 5000/-
Kuazia tani 7 kwenda juu na yaliyopakia mizigo yalipe sh. 10,000/-.
Baskeli ziwe bure ili kuhamasisha watu matumizi ya baskeli kama chombo cha usafiri cha kubana matumizi.
 
Hakuna haja ya kulipia

serikali tunailipa kodi...ilipe hilo deni kwa nssf


Serikali hapa inafanya udalali na kukwepa majukumu ya kuwahudumia wananchi kwa kodi wanazotoa.

Haiwezekani watanzania walipie njia ya kupiga kwa gharama kubwa namna hiyo. Kama serikai ilikuwa haina fedha, ikaingia mkopo na NSSF, ili takiwa kuwa na uelewa wa uwezo wake wa kulipa gharama za ujenzi wa daraja hilo kuliko kukimbilia kupiga picha na kujitanganza kwamba imejenga daraja wakati daraja limejengwa kwa nguvu za wananchi 100%.

Seriakli iache unafiki wa kuwahadaa watu inawahudumia wakati kwa lugha nyepesi inafanya udalali kati ya wananchi na wafanya biashara kama NSSF.

Ama serikali haikupashwa kuingia mkataba na NSSF wa kujenga daraja bila kujua ghrama hizo itazipata wapi. Au la mkataba ule ulitakiwa uwiane na uwezo wa seriakli wa kulipa madeni ya ndani kutokana na vyanzo vyake vya mapato na si kuwarundikia zigo hilo Watnazania wanaolipa kodi kubwa na kula mlo mmoja kwa siku. Watanzania wasiojua siku wanapougua kama watapona ama watakufa kwa sababu hawana fedha za kujitibu na wanapokuwa nazo huduma hakuna mahospitali.

Serikali iache sanaa za maigizo badala yake ionyeshe nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania. Watanzania walitaka mabadiliko ya maisha siyo mabadiliko ya mtindo wa sanaa. Na hapa sasa wanazidi kuona mabadiliko ya kweli kamwe hayatafanywa na Ccm. Ccm ndicho chanzo na ndiyo pingu ya mateso ya Watanzania.
 
Kama mabasi ya DART nauli yake ilijadiliwa sana mpaka wakakubaliana, iweje leo nauli za daraja zimekuja kama suprise, tunaomba mbunge wetu wa Kigamboni alisemee jambo hili bungeni, vingenevyo ile ndoto ya mji wa kisasa inapotea
 
wanakigamboni mnaenda dar kufanya nini wakati huduma zote zinapatikana huko? maduka yapo, masoko yapo mnataka nini tena bakini huko huko maisha ni popote
 
Mimi nnaona lile daraja wangelitangaza kama sehemu ya utalii wa ndani walau tutaielewa Serikali ,lakini hili la huduma tusahau kabisa ..
 
wanakigamboni mnaenda dar kufanya nini wakati huduma zote zinapatikana huko? maduka yapo, masoko yapo mnataka nini tena bakini huko huko maisha ni popote
Ha ha mkuu umewaza km me, hakuna ULAzima wao kuja huku, km vipi wqpige mbizi,
 
Back
Top Bottom