Viwanda zaidi ya 3000 na vilivyokufa vimefufuliwa. Tupeane taarifa ya viwanda hapo ulipo

Kiukweli Kutofanya kazi kwa KIWANDA CHA KOKOTO NYANKALI kunani umiza moyo acheni tu!
 
Kwa mujibu wa mwenyenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni kuwa zaidi ya viwanda vipya 3000 vimejengwa na vya zamani vimefufuliwa. Nchi hii ni kubwa inawezekana hapo hapo ulipo wilayani kwako au mkoani kwako hakuna lakini mkoa au wilaya nyingine vipo.

Hebu tupeane taarifa hapo ulipo wilayani au mkoani je kuna kiwanda kipya kimejengwa hapo? Ni kiwanda cha nini? Je kuna kilichokuwa kimekufa na sasa kimefufuliwa? Ni kiwanda cha nini? Hii itasaidia pia kupeana taarifa za ajira

Mimi hapa Kinondoni/Ubungo hakuna kiwanda kipya kilichojengwa. (Nasema mimi sijakiona kama kipo mnirekebishe) Vilivyokufa kama URAFIKI na UFI havijafufuliwa bado. Ila Ubungo kuna ujenzi wa Flyover na jengo refu la Tanesco linavunjwa
UBUNGO PEKEE
Ufi hoi
Urafiki hoi
Ubungo spinning kwisha kabisa

Morogoro
Mang'ula tools na vingine

Moshi
Kilimanjaro tools

Tanga
Kirani, Mbuni rexona Ashers
Tanga milk
Viwanda vyote vya mkonge

List nj ndefu
 
Hata shetani hawezi kuwa muongo kiasi cha huyu mkolomije, asifikiri watz ni mbu×3 kiasi hicho hivi kweli mchana kweupe anadanya taifa lenye watu zaidi ya mil.50 kuwa kuna v-wonder 3000 vimejengwa na kufufuliwa? Labda mnijuze alisema haya maneno akiwa VIWANJA VYA MILEMBE AU?
 
Haa haa haa no comment,mi niko Tabora naona mauza uza tuu wadau.this is Tanzania.
 
Niko hapa tanganyika perkers mbalizi mbeya.kiwanda kina meneja ila toka kimejengwa hakijawahi hata kuwashwa mitambo .wajanja wanapiga pesa tu.eneo la kiwanda ekali 5000 lakini hakuna production.
 
Hayo matamasha ya uzalendo yanafanyika ili kulisha watu ujinga wa kukubali huo uongo wa mchana kweupe. Viwanda 3000 halafu hata picha hakuna. Hizo nyumba zilizovunjwa picha zake zimejaza server, inakuwaje hivyo viwanda 3000 picha zisionekane? Viwanda vipya kweli vipo ila havizidi 50 na vingejengwa tu hata kama kusingekuwa na hiyo ajenda fake ya viwanda.

Propaganda katika sura ya kizalendo,tunapishana na wachuuzi,hakuna jirani anayetoka nyumbani na kuelekea kiwandani.Mzungu alitupaisha hata kama ilikuwa ni monocrop plantation.
 
Kwa mujibu wa mwenyenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni kuwa zaidi ya viwanda vipya 3000 vimejengwa na vya zamani vimefufuliwa. Nchi hii ni kubwa inawezekana hapo hapo ulipo wilayani kwako au mkoani kwako hakuna lakini mkoa au wilaya nyingine vipo.

Hebu tupeane taarifa hapo ulipo wilayani au mkoani je kuna kiwanda kipya kimejengwa hapo? Ni kiwanda cha nini? Je kuna kilichokuwa kimekufa na sasa kimefufuliwa? Ni kiwanda cha nini? Hii itasaidia pia kupeana taarifa za ajira

Mimi hapa Kinondoni/Ubungo hakuna kiwanda kipya kilichojengwa. (Nasema mimi sijakiona kama kipo mnirekebishe) Vilivyokufa kama URAFIKI na UFI havijafufuliwa bado. Ila Ubungo kuna ujenzi wa Flyover na jengo refu la Tanesco linavunjwa
Umekisahau kile kilchopakana na urafiki fishnet sasa hivi ubungo park
 
bagamoyo kuna viwanda vingi
1. vegeta podrvka- cha kutengeneza spices( viungo vya kupikia)
2. kamal estate ( kuna viwanda vingi ndani yake)
3. kiwanda cha betri
4. kiwanda cha bati
5. kiwanda cha nondo
6. kiwanda cha ngozi
na vingine vingi vipo ni kutembea tu utaviona.

Tunarudia tu hakuna anayebisha kwamba kuna viwanda, ila havifiki 3000+. Ni kweli vipo lakini havizidi 50. Hebu wewe ukiweza jaribu kupiga picha wangalau viwanda 10 tu. Viwanda 3000+ mji mzima wa Dar vijana si wangezizima kwa maelfu kwenda kupiga vibarua. Hata mama lishe tungewaona wakienda kuuza msosi kwa vibarua. Pia tungeona nyumba nyingi za makazi kwa ajili ya watu watakaokuwa wanafanya kazi viwandani. Ingekuwa na nyomi kama ile tunayoonaga watu wakigundua migodi yenye madini ya thamani kubwa.
 
Mimi hapa naona tu hii michezo imeletwa na wachina sijui ni kamali watoto na vijana wamejaa kweli
 
Back
Top Bottom