Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
Kwa mujibu wa mwenyenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni kuwa zaidi ya viwanda vipya 3000 vimejengwa na vya zamani vimefufuliwa. Nchi hii ni kubwa inawezekana hapo hapo ulipo wilayani kwako au mkoani kwako hakuna lakini mkoa au wilaya nyingine vipo.
Hebu tupeane taarifa hapo ulipo wilayani au mkoani je kuna kiwanda kipya kimejengwa hapo? Ni kiwanda cha nini? Je kuna kilichokuwa kimekufa na sasa kimefufuliwa? Ni kiwanda cha nini? Hii itasaidia pia kupeana taarifa za ajira
Mimi hapa Kinondoni/Ubungo hakuna kiwanda kipya kilichojengwa. (Nasema mimi sijakiona kama kipo mnirekebishe) Vilivyokufa kama URAFIKI na UFI havijafufuliwa bado. Ila Ubungo kuna ujenzi wa Flyover na jengo refu la Tanesco linavunjwa