Viwanda 4000, mia moja kila mkoa vimemuangusha Rais Magufuli

Viwanda 4000, mia moja kila mkoa vimemuangusha Rais Magufuli

Hata hapo malawi??!!! Corona imeshika kasi kuanzia February, na wao wanajua kila mwaka kuanzia April , huwa tatizo la sukari lazima tu lijitokeze, hapa ni ubabaishaji tu!!!

Hapo Malawi ni plan B. of course ni uzembe na kuishi kimazoea ndio imetufikisha hapa. Sasa ndio walitaka waagize April kimazoea ndio lockdown ikawaangusha. Hiyo ya Malawi haitatosha mahitaji, bado sukari itasumbua sana round hii.
 
Kabla meko hajaingia madarakani sukari kg moja ilikua 2000-2200 mpka 1800 baadhi ya maeneo Ila toka aanzishe kusapoti viwanda vya ndani Bei iko juu kila siku na haina dalili za kushuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa utasapoti viwanda vya ndani kwa maneno tu,? wakati gharama za uzarishaji/kodi bado zipo juu?? Hata hivyo viwanda vya ndani vya sukari bado havina uwezo wa kutosheresha mahitaji ya ndani.
 
Njama za mabeberu...Na wameleta covid-19, kutumaliza SISI peke yetu, ndiyo maana hata vipimo vyao tunavipima kwanza...


Everyday is Saturday......................... 😎
 
nchi kama tanzania imejaliwa ardhi nzuri ya kulima miwa halafu tunaagiza sukari nje ni UPUMMBAFU,
ndio maana nasema nchi inakwenda zig zag style kama mlevi flani hivi
 
It is a sad story ambayo itasimuliwa vizazi na vizazi. Mojawapo ya sifa kubwa ya serikali ya wamu ya tano iliyotikisa dunia ni jinsi ilivyoweza kujenga viwanda vikubwa 4000 ndani ya miaka 4 habari hii pia iliungurumishwa na Profesa Kabudi kwenye United nations general assembly alipokuwa akifafanua mafanikio ya awamu ya tano

Ila sasa sukari jameni, maviwanda yote hayo yameshindwa hadi tunaagiza Malawi? au inakuja via Malawi kama transit? viwanda 4000 vimeshindwa tena kila mkoa uliagiza ujenge viwanda 100 nakumbuka RC mchapakazi mzalendo wa Manyara alitoa amri na Ultimatum kwa wakuu wa wilaya kwamba wajenge viwanda kwenye wilaya zao na waziri Jaffo alisistiza hilo

Hatua kali zichukuliwe kwa wasimamizi na mabosi wa hivyo viwanda katika 4000 hatukosi hata kumi vya sukari.
Wanashindwa kujenga shule za chekechea itakuwa viwanda?

Na viwanda vitajengwa na sekta binafsi ikiwekewa mazingira wezeshi.
 
It is a sad story ambayo itasimuliwa vizazi na vizazi. Mojawapo ya sifa kubwa ya serikali ya wamu ya tano iliyotikisa dunia ni jinsi ilivyoweza kujenga viwanda vikubwa 4000 ndani ya miaka 4 habari hii pia iliungurumishwa na Profesa Kabudi kwenye United nations general assembly alipokuwa akifafanua mafanikio ya awamu ya tano

Ila sasa sukari jameni, maviwanda yote hayo yameshindwa hadi tunaagiza Malawi? au inakuja via Malawi kama transit? viwanda 4000 vimeshindwa tena kila mkoa uliagiza ujenge viwanda 100 nakumbuka RC mchapakazi mzalendo wa Manyara alitoa amri na Ultimatum kwa wakuu wa wilaya kwamba wajenge viwanda kwenye wilaya zao na waziri Jaffo alisistiza hilo

Hatua kali zichukuliwe kwa wasimamizi na mabosi wa hivyo viwanda katika 4000 hatukosi hata kumi vya sukari.
propaganda huwa na mwisho wake.
 
Tambo za viwanda, mafisadi hatuzisikii siku hizi.Refa kapigwa chali soda imeisha povu.Sijui watatuongopea nn kwenye kampeni tunawasubiria, hawana mapya wameshamaliza yote
 
kwenye sukari ilitakiwa iwe kama hivi
MAFUTA.jpg
 
Back
Top Bottom