Viwanda 1,845 vyaanzishwa mwaka mmoja

Viwanda 1,845 vyaanzishwa mwaka mmoja

Ndio chama pekee duniani kilicho tayari kuiona nchi inapukutika chenyewe kinanawiri! 1985 mwlm aliacha viwanda zaidi ya 450 watz mil 29 jmk ameondoka 2015 tuko milion 52 na viwanda chini ya 200 alafu kuna watu wanaisifu ccm.
We ulitaka wasifu chama gani. Huu ni wakati wa kufanya kazi hatuhitaji siasa sisi subirini 2020
 
Viwanda labda vya kuunganisha wachawi ambavyo kuviona lzm na ww uwe mchawi
Serikali iliyojaa porojo ambayo kampeni zake za kutafuta kura zilijaa uongo mtupu sasa inaumbuka
 
Nilimsikia Mh.Waziri wa viwanda kule mjengoni akisema kazi yao ni "KUPIGA SOUND" na kama mtu anamuwekezaji amlete yeye atampa ardhi fasta.
 
viwanda elifu hamsini na nne si haba 54,000 na hapa kwa.mangi bado tunaletewa maziwa mtindi toka kampuni brookside ya kenya ?
 
Serikali imetoa taarifa kuwa katika kipindi cha mwaka moja wa Serikali ya awamu ya tano, vimeanzishwa Viwanda vipya 1800. Hata hivyo Serikali inaarifu kuwa hadi sasa Tanzania ina takribani Viwanda 54,000 vinavyofanya kazi. Kwa takwimu hizi Tanzania ina Viwanda vingi kuliko Shule zote za Msingi na Sekondari nchini. Kwa maana hii, Tanzania ya Viwanda ilianza kabla ya awamu ya tano. Sasa, hivi Viwanda vinazalisha bidhaa gani maana bidhaa nyingi tunazotumia zinatoka nje ya nchi.
Unaleta uchochezi sio? M7 zitakuhusu wewe.
 
Natafuta viza ya Afghanistan mie,sijui balozi lipo wapi ivi??
 
Hivyo viwanda viko wilaya gani na mkoa gani?
Unaambiwa sasa hivi ukifunga ice cream kwenye vifuko vya nailoni unahesabika kama mwekezaji na tayari unakuwa mmiliki wa kiwanda .
 
majaliwabungeni_210_120.jpg

WAZIRI MKUU-MAJALIWA KASIM MAJALIWA.

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja kilichoanzia Novemba mwaka jana mpaka Oktoba mwaka huu ambacho kimeongozwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini Rais John Magufuli, jumla ya viwanda vipya 1,845 vimeanzishwa na hivyo kufanya jumla ya viwanda vyote nchini kufikia 54,422.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiahirisha Mkutano wa Tano wa Bunge la 11.

Waziri Mkuu Majaliwa alifafanua kuwa kwa mujibu wa ripoti iliyotokana na sensa ya viwanda iliyofanyika kuanzia mwaka 2013/14 hadi mwaka jana ilionekana kuwa mpaka Oktoba mwaka jana kulikuwa na viwanda 52,579.

“Ni matumaini ya Serikali kuwa kutokana na juhudi za uhamasishaji zinazofanyika, kasi ya uanzishwaji viwanda na hasa viwanda vidogo na vya kati na vikubwa itaongezeka sana,” alisisitiza Majaliwa katika hotuba hiyo ambayo hata hivyo hakuisoma bungeni kutokana na msiba wa Mbunge wa Dimani, Hafidh Ali Tahir, badala yake ikawekwa katika kumbukumbu rasmi za Bunge.

Alisema katika matokeo ya sensa hiyo hadi kufikia mwaka 2013, Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 49,243 ambapo viwanda vidogo vinavyoajiri mtu mmoja hadi wanne vilikuwa ni asilimia 85.13 na viwanda vidogo vyenye watu watano hadi 49 vilikuwa asilimia 14.02.

Alisema matokeo hayo pia yalionesha kuwa viwanda vya kati vyenye watu 50 hadi 90 vilikuwa ni asilimia 0.35 na viwanda vikubwa vyenye watu kuanzia 100 na kuendelea ni asilimia 0.5.

Hivyo, Asilimia 99.15 ya viwanda vyote nchini ni viwanda vidogo.

Alisema serikali kupitia wizara mbalimbali za kisekta tayari imebainisha maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuchochea uwekezaji kama vile kuendeleza eneo la mji wa Kigamboni na kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji katika mikoa mbalimbali nchini.

“Hatua nyingine ni kuboresha miundombinu kama vile barabara na reli. Mfano mzuri ni ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita nne katika kiwanda kipya cha Kilua Group cha kutengeneza nondo kilichopo Mlandizi, Pwani,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa viwanda mbalimbali nchini na kwa viwanda vilivyopo karibu na bomba la gesi vitaunganishwa na bomba hilo ili vitumie gesi. Aidha, alisema tayari serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kasi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda inaongezeka ili ichangie asilimia 15 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2020.

Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kutambua sekta za kipaumbele kwa kuzingatia viwanda vinavyotumia malighafi za ndani, hususan kwenye sekta za kilimo na maliasili ili kuchochea uzalishaji vijiini na kuongeza ajira; kuandaa mpango mahsusi wa uwekezaji kwenye viwanda kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii na kuhamasisha sekta binafsi, ya ndani na nje ya nchi, kuwekeza kwenye viwanda.

Alisema pia mkakati mwingine ni kutoa elimu na mwongozo kwa serikali ngazi ya mikoa na wilaya kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo yao.


Chanzo: Habari Leo
Kama kweli Tanzania tuna idadi ya Viwanda 49000, kungekuwa na Tatizo la Ajira?
Wanahesabu viwanda au Workshop?
Pengine hata wale watu walioweka Bech pembezoni mwa Nyumba wakichonga Milango na madirisha wanahesabu kuwa ni viwanda?
 
Ila kwa kweli mi hapa ndo sielewi kabisa
Mwanzo walisema viko 52300 na sivioni
Vimeongozeka vimefika 54000 bado sivioni
Ila bila shaka hivi viwanda vitakuwa chini ya ardhi,

Nafikiri hata brenda yangu nikitumia kusaga juice ni kiwanda kinahesabiwa
Teh.. Teh.. We mchina macho madogo huwezi ona hivo viwanda... Teh.. Teh..
 
85% ya viwanda ni vya kuajiri watu wa 4 this is a joke!!!!

Premier amekuwa honesty anyway, ukweli utakuweka huru hongera Kasimu.
 
Back
Top Bottom