Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
SERIKALI imetangaza kuvifungia mara moja vituo vya kulele watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu nchini kutokana na kukiuka maadili na Sheria ya Haki za Mtoto, Fikra Pevu inaripoti.
Inaelezwa kwamba, baadhi ya wamiliki wa vituo hivyo wamekuwa hawafuatia Sheria ya Haki za Mtoto, badala yake wanavitumia kwa maslahi yao binafsi.
Tamko la azma ya serikali kuvifungia vituo hivyo limetolewa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amesema vituo vitakavyobainika kuendeshwa vinawanufaisha wamiliki vitafungiwa mara moja.
Soma zaidi hapa => Vituo vya watoto yatima kufungiwa | Fikra Pevu